Habari za Punde

NNB Yakabidhi Fulana Kwa Ajili ya Maadhimisho ya Sherehe za Kizimkazi Day.

MENEJA Benki ya NNB Tawi la Mwanakwerekwe, Naima Said Shaame, (kushoto) akimkabidhi fulana Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Wilaya ya Kusini Unguja, Kassim Mtoro Abuu, katika makabidhiano yaliofanyika afisi za NNB Malindi (kulia) ni Meneja wa NNB Zanzibar, Abdalla Duchi .(Picha na Abdalla Omar).
NA. SINDA AMRAN (TUDARCO)
MAKAMO wa Rais wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kuadhimisha siku ya Kizimkazi day, ambayo inatarajwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Kassimu Mtoro Abu Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Wilaya ya Kusini Unguja, wakati akipokea msaada wa Fulana uliotolewa na Banki ya NMB huko Ofisini kwao Malindi.
Alisema lengo la kuweka siku hiyo ni kuwaunganisha wananchi wa shehiya za Kizimkazi pamoja na kuweza kupanga mambo yao ya maendeleo kwa lengo la kupunguza changamoto zinazozikabili shehiya hizo.
Katika sherehe hiyo michezo mbali mbali itafanyika ikiwemo resi za ngalawa , michezo ya watoto pamoja na maonyesho ambayo yatakwenda sambamba na siku hiyo.
Mbali na hayo pia kutakuwa na zawadi maalum kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya Taifa.
Alisema tokea kuanzishwa kwa Kizimkazi day kumeleta  faida kubwa ikiwemo kujengwa nyumba za walimu, madaktari, vituo vya afya, biashara ndogo ndogo za akina mama, wajasiriamali  pamoja na kutoa mikopo midogo  kwa wanajamii wa eneo hilo.
Hivyo amewataka wananchi na wazawa wa Kizimkazi kushiriki katika siku hiyo ili kuweza kuleta maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla .
Kwa upande wa Meneja wa NMB Zanzibar Abdallah Duchi, amesema wameamua kutoa ushikiano mkubwa kwenye sherehe hizo kwa lengo la kuleta maendeleo.
Alisema pia watahakikisha wanashiki katika maonyesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kuhusiana na benki hiyo, katika ghafla hiyo jumla ya fulana 230 zimetolewa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.