Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Azungumza na Kusalimiana na Masheikh wa Wilaya ya Magharibi "A" Unguja Ikulu Ndogo Kibweni.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi MheDk Al Hajj Ali Mohamed Shein, akizungumza na Viongozi wa Dini wa Wilaya ya Magharibi "A" Unguja na Viongozi wa Serikali walipofika Ikulu Ndogo Kibweni kumsalimia baada ya kumalizika kwa Sala Eid El Hajj iliofanyika katika viwanja vya Betras Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.

Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Masheikh wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Alhajj Ali Mohamed Shein, wakati walipofika Ikulu Ndogo Kibweni kumsalimia baada ya kumalizika kwa hafla ya Sala ya Eid El Hajj iliofanyika Kitaifa katika Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Khamis Juma Mwalim akizungumza wakati  hafla hiyo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Alhajj Ali Mohamed Shein, kuzungumza na kusalimiana na masheikh hao wa Wilaya ya Magharibi "A" walipofika Ikulu Ndogo Kibweni kumsalimia. baada ya kumaliza Sala ya Eid El Hajj iliofanyika Kitaifa viwanja vya Betras katika Wilaya ya Magharibi "A" Unguja.  
Baadhi ya Mawaziri na Masheikh wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Alhajj Ali Mohamed Shein, walipofika Ikulu Ndogo kumsalimia na kumtakia kheri katika Uongozi wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Alhajj Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mah.Balozi Seif Ali Iddi, wakiitikia dua ikisoma na Kadhi wa Rufaa kutoka Pemba Sheikh Daud Khamis Salum, baada ya kumaliza mazungumzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.