Habari za Punde

Wananchi wa Kwahani Wameanza Kuhama Kupisha Ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Kisasa za Maendeleo za Mradi wa ZSSF.

Wananchi wa Kwahani wakiwa katika uvunjaji wa Nyumba zao baada ya kukamilika kwa matayarisho na kulipwa Fedha za kukodi nyumba kupisha ujenzi huo unaotarajiwa kuchukua mwaka mmoja mpaka kukamilika ujenzi huo na kurudi katika makazi yao hayo mapya ya Nyumba za Maendeleo ya Mji Mpya wa Kwahani Zanzibar kwa Wananchi wa Nyumba 51 za awamu ya kwanza ya ujenzi huo. 

Mmoja wa Mkazi wa Nyumba za Kwahani Zanzibar Ndg. Ali Hamad Haji akionesha Mkataba wake na Mfuko wa Hifadhi ya Jamiii Zanzibar (ZSSF) na Hati ya Ardhi ya Muda inayoonesha umiliki wa nyumba yake.

Mzee Ali Hamad Haji akiwa na familia yake wakati akijiandaa kuhama katika makazi yake hayo kupisha ujenzi wa Mji wa Kisasa wa Maendeleo Kwahani Zanzibar. Mradi huo unaosimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa awamu ya kwanza itahusisha nyumba 51 kati ya Nyumba 407 katika eneo hilo.   No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.