Habari za Punde

TANESCO Yakabidha Msaada Wake Kwa Kijana Anayeishi Kwa Msaada wa Mashine ya Oxygen.

Kijana Hamad Awadhi akiwa ameketi na mshine yake pembeni.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KIJANA anayeishi kwa msaada wa mashine ya Oxygen ili kumuwezesha kupumua, Bw. Hamad Awadhi amelishukuru Shirika la Umeme Nchini TANESCO kwa kumpunguzia mzigo wa gharama za umeme kwa kumlipia bili ya umeme wenye gharama ya Shilingi Milioni 1,500,000/=/.
Kijana huyo ambaye anaishi eneo la Ukonga Majumba Sita jijini Dar es Salaam, alisema madaktari walimueleza kuwa mapafu yake yameharibika na hawezi kuishi bila ya kutumia msada wa mashine ya oxygen na kwamba mashine hiyo inayotumia umeme, amekuwa akilipia bili ya umeme shilingi 45,000/= kila wiki.
“Kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka, tumeguswa baada ya kupata taarifa za maradhi yanayokusumbua, tumekuja kukupa pole na kukuombea kwa Mwenyezimungu, lakini sisi kama Shirika linalotoa huduma katika jamii,  tumeona tunaweza kufanya kitu  kidogo hata kama si kumaliza tatizo basi hata kupunguza ili uone kwamba licha ya matatizo yanayokukabili jamii iko nawe na inakujali.” Kaimu Meneja Uhusianbo wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Bi. Leila Muhaji alimueleza Bw. Awadh, wakati alipoambatana na Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala Mhandisi Sotco Nombo kumjulia hali na kumpatia taarifa ya msada kutoka TANESCO.
Bi. Leila alisema, “TANESCO tunafanya kazi ya kutoa huduma ya umeme, tutahakikisha unapata umeme bila kuwaza kwa muda w amiezi 6, tutatoa shilingi Milioni 1,500,000/= ili isaidie katikakipindin hicho.” Alisema Bi. Leila.
Bi. Leila alisema, sambamba na kulipia gharama hizo za umeme TANESCO pia baada ya kupata ridhaa ya mwenye nyumba anamoishi Bw. Awadhi, itamfungia mita yake pekee ya umeme na kumuwekea mfumo wa umeme utakaomuwezesha kujitegemea yeye mwenyewe na hivyo kumpunguzia mzigo wa gharama za kulipia bili ya umeme.
Aidha Kaimu Meneja Uhusiano huyo wa TANESCO, alisema Shirika pia limezingatia ombi lake la kusaidiwa fedha za kumuwezesha kupatiwa matibabu nje ya nchi.
“Sisi kama TANESCO tutachangia shilingi milioni 10 ili kuchangia matibabu yako, fedha hizi hazihusiani na kulipia gharama za umeme hizi fedha ni za kuchangia matibabu yako na tutaziwasilisha, leo tumeona tufike tukupe pole na tukueleze jinsi tulivyoguswa na taarifa ya maradhi yanayokusibu.” Alifafanua Bi. Leila  Muhaji.
Aidha Meneja wa TANESCO Mhandisi Sotco Nombo alisema, baada ya kupata ridhaa ya mwenye nyumba TANESCO itagharimia gharama zote za ufungaji wa mita, na kufunga mfumo wa umeme utakaomuwezesha kutumia umeme wa kwake peke yake bila ya kuingiliana na wakazi wengine katika nyumba hiyo.
“Kama mnavyojua mpendwa Rais wetu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesisitiza suala la uzalendo miongoni mwa watanzania, na sisi tumeona tuungane na watanzania wenzetu ili kumsdaidia Mtaznania mwenzetu anayesumbuliwa na maradhi haya.” Alisema Mhandisi Nombo na kuongeza
“Tutamuwekea umeme wa peke yake, kama mnavyoona hapa kuna wapangaji zaidi ya watano na wote wanatumia mita moja na hakika matumizi lazima yatatofautiana na kama mnavyoona matumizi ya Awadhi sio makubwa kiasi hicho cha kutumia kiasi cha shilingi 45,000 kwa wiki, tumeona tufungue mita ya kwake pekee tunachofanya kwa sasa ni kuwasiliana na mwenye nyumba ili kupata ridhaa yake.” Alifafanua Mhandisi Nombo.
Akitoa shukrani baada ya taarifa hiyo kutoka TANESCO, Bw. Awadhi alisema “Umeme ndio maisha yangu, ndio Mungu wangu wa pili ingawa Mungu hashirikishwi, siwezi kufananisha na Mungu lakini mimi bila umeme ndio basi tena, mashine hii inatumia umeme masaa yote.” Alisema Bw. Awadh.

Aliishukurui TANESCO kwa msada huo mkubwa na kutoa wito kwa watanzania wengine kujitokeza ili kumsaidia.
 Kaimu Meneja Uhusianbo wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Bi. Leila Muhaji (Kulia) akiwa na Meneja wa TANECO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Sotco Nombo, (matikati), akizungumza leo Septemba 5, 2019 mbele ya kijana Hamad Awadhi anayeishi kwa msada wa mashine ya oxygen kumsaidia kupumua wakati walipomtembelea nyumbani kwake Ukonga Majumba Sita jijini Dar es Salaam.
 Kijana Hamad Awadhi akiwa na mipira iliyounganishwa kwenye mashine hiyo.
 Kijana Hamad Awadhi akiwa ameketi na mshine yake pembeni.
Hizi ni mashine mbili tofauti, moja iliyo mbele ni mashine ya Oxygen inayotumia umeme ambayo humsaidia kupumua wakati aanapopata tabu ya kupumua mwenyewe. na nyuma ni mtungi wa oxygen ambao nao huutumia wakati ambapo hakuna umeme.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.