Na Ali Issa Maelezo
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mohammed Ramia Abdiwawa amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa maduka unaoendelea katika eneo la michezani na maskani ya Kisonge mjini Zanzibar.
Hayo ameyasema leo huko Michenzani wakati aki fanya ziara ya ukaguzi kuangalia maendeleo ya u jenzi wa maduka Mool shoop na Kisonge.
Amesema kuwa ameridhishwa na ujenzi huo kwa hatua uliofikia licha ya kuwa na changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza katika ujenzi huo.
Akizitaja changamoto hizo kwa upande wa jengo la kisonge maskani linalo jengwa na Chama cha Mapinduzi ikiwemo mchanga maalumu ambao wanauhitaji wakati wa kujengea nguzo pamoja na kokoto.
Aidha amesema Serikali tayari imezipatia ufumbuzi changamoto hizo ambapo majengo hayo yanatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2020.
Hata hivyo amewataka vijana wa kizanzibari wachangamkie frusa ya ajira katika ujenzi unao endelea kwani hiyo ndio njia moja ya kupata kipato halali.
Nae mshauri elekezi wa maduka mall shop yanayo jengwa kwa udhamini wa ZSSF Rose Nestory alimwambia Waziri jengo hilo litakuwa na ghorofa tisa, Ambalo litagharimu shilingi bilioni 27.9 hadi kukamilika kwake.
No comments:
Post a Comment