Habari za Punde

Umoja wa Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi

Baadhi ya wanachama wa Baraza la Watu wanaoishi na VVU wa KONGA ya Kilombero awakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika ofisi za konga hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na wajumbe wa Baraza la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI wa KONGO ya Wilaya ya Kilombero alipowatembelea kuangalia namna wanavyoendesha shughuli zao za kimaendeleo na kuwajulia hali.
Mkurugenzi wa Utafiti na Tathimini kutoka Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akizungumza jambo kuhusu hali ya Maambukizi mapya kwa wanakonga ya Wilaya ya Kilombero wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko.
Mratibu UKIMWI mkoa wa Morogoro Bi. Ndayahunda Hendry akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na VVU wa Konga ya Kilombero, Halida Ally akisoma taarifa ya Konga hiyo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika konga hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na umoja wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI wa KONGO ya Wilaya ya Kilombero alipowatembelea kuangalia namna tekeleza shughuli zao za kimaendeleo 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akiangalia  baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na wanachanama wa KONGA ya WAVIU iliyopo Kilombero wakati wa ziara yake katika konga hiyo tarehe 17 Oktoba, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.