Nahodha wa timu ya Mbega Mwekundu akikabidhiwa vifaa na mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akiwa sambamba na Mwenyekiti wa chama
cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava kwa ajili ya ligi ya Asas Super League 2019/2020.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto ametoa vifaa vya michezo kwa timu mbili zinazoshiriki ligi ya Asas Super League ambazo ni Irole Fc na Mbegu Mwekundu ambazo zinatoka katika wilaya ya Kilolo
Akizungumza wakati wa kukabidhi jezi,viatu na mipira mbunge huyo alisema kuwa ametoa vifaa hivyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri kwenye ligi ya Asas Super League ya msimu wa mwaka wa 2019/2020.
Hivi vifaa viwaongezee hali ya kupambana ili kuhakikisha mnakuwa mabingwa wa league hii ambayo imekuwa na ubora sana tofauti na ilivyokuwa hapo awali,nawaombeni sana hakikisheni mnapambana kupata matokeo chanya kila mechi mnayoicheza”alisema Mwamoto
Mwamoto aliwataka wachezaji wa timu zote mbili kucheza kwa nidhamu ya juu kwa kuwa mpira miguu ndio unataka hiyo.
“Timu ya Mbega Mwekundu na wenzenu Irole Fc hamjaonyesha nidhamu kwenye mechi hii zenu hivyo mnatakiwa kulinda nidhamu yenu ili muwezekufika mbali kisoka” Mwamoto
Mwamoto alisema kuwa jezi na vifaa vingine vyote vina thamani ya kiasi cha shilingi milioni mbili na vyote vimetolewa na ofisi ya mbunge kwa lengo la kuwasaidia timu hizo kwenye ligi hiyo.
Naye Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava alisema kuwa ataendelea kuzichangia timu hizo nauli pamoja na maji ya kunywa kwenye kila mchezo hivyo wachezaji wanapaswa kucheza kishindani ili wapate matokeo.
“Mimi nitatoa laki moja kwa kila mechi ambayo mtashinda hivyo kazi imebakia kwenu kuhakikisha mnashinda michezo yote iliyobakia na kufanikiwa kuingia nane bora” alisema Kuyava
Aidha Kuyava alisema kuwa mbunge wa jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto ameongeza kiasi cha shilingi elfu hamsini kwa kila mechi ambayo watashinda hivyo inakuwa laki moja na nusu kwa kila mchezo watakaoshinda .
Kuyava alimalizia kwa wachezaji na viongozi kuwa na nidhamu kwenye michezo mbalimbali ili kuwa timu bora na yenye ushindani wa kweli.
Nahodha wa timu ya IroleFc akikabidhiwa vifaa na mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akiwa sambamba na Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava kwa ajili ya ligi ya Asas Super League 2019/2020
Mchezaji wa timu ya Mbega Mwekundu akikabidhiwa vifaa na mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akiwa sambamba na Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava kwa ajili ya ligi ya Asas Super League 2019/2020.
Nahodha wa timu ya IroleFc akikabidhiwa vifaa na mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akiwa sambamba na Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava kwa ajili ya ligi ya Asas Super League 2019/2020
No comments:
Post a Comment