Habari za Punde

Mdfumuko wa bei waongezeka mwezi wa Septemba

Na Mwashungi Tahir   Maelezo
Mkuu wa Takwimu za bei kutoka Ofisi ya Mtakwimu aZanzibar Khamis Abdul-rahman Msham amesema mfumko wa bei wa mwaka  umeongezeka kwa 2.2 mwezi wa Septemba 2019,  ukilinganisha na mwezi uliopita wa August 2019 ambapo ulikuwa 2.1.
Ameyaeleza hayo huko katika Ofisi za Mtakwimu ulioko huko Mazizini wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ongezeko  wa mfumko wa bei .
Amesema Kushuka kwa baadhi ya bidhaa muhimu nchini   kupelekea kushuka kwa mfumuko wa bei kutoka   asilimia 0.8 kwa mwezi wa Agosti kulinganisha na asilimia 1.2 kwa mwezi wa Septemba .
Pia amefahamisha kuwa upande wa bidhaa hizo ikiwemo samaki ameshuka kwa asilimia 3.1 tan rice 2,5 ndizi za mtwike 4.7 mchele wa Mbeya 1.9 na sukari 0.3.
Nae Mhadhiri wa uchumi kutoka chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA,
Dkt. Suleiman Msaraka amefahamisha kuwa mabadiliko ya faharisi za bei
yanaendana na wakati uliopo kwa kulinganisha na mwezi kwani bado tupo katika
hali nzuri kama ilivyakadiriwa na Serikali .

Kwa Upande wa Meneja wa Uchumi Benki kuu ya Tanzania Tawi la Zanzibar Moto Ngwinganele Lugobi  amesema  mfumko umeongezeka ila sio sana  na kwa upande wa soko la  Zanzibar  liko vizuri.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.