Habari za Punde

RC Kusini azindua klabu ya wasanii ya UVCCM mkoa wa kusini Unguja

Na Maryam Kidiko / Maelezo.        
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amesema atatumia fursa mbali mbali zilizopo ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja ili kuongeza kasi ya maendeleo katika Mkoa huo.
Hayo ameyasema katika Ukumbi wa Kituo cha Walimu Dunga Wilaya ya Kati wakati akizindua Klabu ya Wasanii ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema Vijana hao ikiwa wataelewa fursa zilizopo katika Mkoa huo watapiga hatua kubwa katika suala la kujiletea maendeleo kwa kila mmoja na kuondoa zana nzima ya kuajiriwa Serikalini.
Hata hivyo amesema ni muhimu kwa Vijana hao kuwatumia Wasaanii wakogwe ili kujifunza vitu vingi vya sanaa kutoka kwao.
Vile vile amelitaka Baraza la Sanaa Zanzibar kuvisajili Vikundi vyote vya Sanaa kutoka Mkoa wa Kusini Unguja kwa muda wa mwezi mmoja ili kupata kujiajiri wenyewe .
Aidha amesema Klabu hiyo ya Wasanii itapofanya vizuri itakuwa ni miongoni mwa klabu zinazoleta maendeleo katika Nchi hivyo lazima kuwe na mashirikiano ili kutimiza lengo hilo.
Nae Katibu wa  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kusini Unguja Aboud Said Mpate amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawataka Vijana waweze kujiajiri wenyewe hivyo tuwape ushirikiano ili kutimiza lengo la Serikali.
Katika Risala ya Wasanii wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)Mkoa wa Kusini Unguja wamesema watatumia vipaji vyao ili kuweza kujiajiri wenyewe.
Sambamba na hayo walisema wanaunga mkono ilani ya chama cha Mapinduzi ili kuleta maendeleo katika Nchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.