Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Fatma Hassan Mrisho wa Chuo cha Kiislamu cha Micheweni Pemba kulia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe.Riziki Pembe Juma, zawadi hizo zilizotolewa na Mfanyabiashara maarufu Zanzibar.Ndg.Said Nassir Nassor Bopar kwenye Chuo hicho.
Mwanafunzi wa Chuo cha Kiislamu Micheweni Ali Imran Mussa akipokea zawadi kutoka kwa Balozi Seif iliyotolewa na Mfanyabiashara Said Nassir Nassor Bopar kutekeleza ahadi aliyowapa Miezi michache iliyopita.
Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Bibi Shadya Shaaban Seif akipokea chakula kutoka kwa Balozi Seif kilichotolewa msaada na Mfanyabiashara Said Bopar kutekeleza ahadi aliyotoa kwa wagonjwa wa Hospitali ya Vitongoji.
Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi zawadi ya Desktop Mwalimu wa Skuli ya Madungu Mohamed Shamte kwa ajili ya Skuli yake baada ya kutoa Wanafunzi wa Daraja la Kwanza Mwaka huu.
Mwanafunzi Rayan Ali Said akipokea msaada wa Miwani kutoka kwa Balozi Seif Ali Iddi iliyotolewa na Mfanyabiashara Said Nassir Nassor Bopar hapo Ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
Picha na – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment