Habari za Punde

Wazazi Wametakjiwa Kutowafumbia Macho Wanaowadhalilisha Wanawake na Watoto.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Moudline Castico akizungumza na viongozi na wanachama wa jumuiya ya UWT kuhusu kupiga vita vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji wanawake na watoto, wakati wa mkutano wake katika viwanja vya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar.
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Wazazi Mkoa wa Mjini Unguja wakifurahi jambo wakati wa mkutano na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar.Mhe. Maudline Castico.

Na Rahma Khamis Maelezo   3/10/2019                                  
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee Wanawake na Watoto Mh Moudline Castico amewataka wazazi na walezi kutowafumbia macho waume na kuwafichia maovu wanayowatendea Watoto katika suala la udhalilishaji.
Ameyasema huko Amani Mkoa wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa Jumuiya ya wanawake Tanzania kuhusu kupiga vita suala la unyanyasaji na udhalilishaji wa wanawake na Watoto
  Amesema akina mama wanajifanya kuwa na mapenzi ya waume zao na kuwafichia vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji wanavyowafanyia watoto jambo ambalo linakosesha haki na wajibu wa Watoto hao
Amesema wazazi wana muhali katika kukabiliana na suala la unyanyasaji na udhalilishaji katika kutoa Ushahidi na kupelekea kesi kukaa muda mrefu hatimae kufutwa jambo ambalo linarejesha nyuma juhudi za Serekali za kupambana na vitendo hivyo.
  Aidha amesema wazazi wanajukumu kubwa la kuwalea na kuwalinda watoto hivyo wahakikishe kuwa muda wote wako pamoja nao na kujua mienendo yao ili kuwanusuru na vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji unaoweza kujitokeza.
Aidha amefafanua kuwa utafiti uliofanywa mwaka 2015/2016 wa vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji unaonesha kuwa asilimia 10 ya vitendo unyanyasaji na udhalilishaji hivyo kuna  haja ya kupambana ili kuondosha vitendo hivyo.
Hata hivyo amesema kuwa kuna baadhi ya kinamama huwatetea na kuwaficha waume zao wanaofanya vitendo vya udhalilishaji jambo ambalo sio sahihi hivyo ipo haja ya kupewa adhabu kwa pamoja pale tu inapobainika ili kudhibiti vitendo hivyo visiendelee.
Waziri Castico amefahamisha kuwa katika kupambana na vitendo hivyo lazima wazazi na walezi kutowalaza pamoja Watoto wa kike na kiume sambamba na kuwalaza na wageni wanaokuja kutembea ambao hawawajui tabia zao.
Akitoa taarifa kuhusu kupambana na udhalilishaji na unyanyasaji Katibu wa UWT Wilaya ya Amani Asha Mzee Omar  amefafanua kuwa idadi ya kesi zilizoongezeka kuwa ni kesi ya kutoroshwa.kubakwa,ujauzito pamoja na ndoa za utotoni na kukashifiwa kwa mtoto na mtu mzima.
Aidha amesema lengo la kukutana kwao ni kuelimisha umma kuhusu vitendo vya udhalilishaji ambavyo vimekithiri Zanzibar hivyo wameamua kupita kila Skuli Madrasa na jamii kwa ujumla kutoa elimu ili kupambana na vitendo hivyo.
Akielezea changamoto wanazozipata katika kupambana na vitendo hivyo Katibu huyo amesema kuwa kuna baadhi ya wazazi na jeshi la polisi kutokuwa na ushirikiano mzuri katika kutoa Ushahidi na kukaa muda mrefu kesi mikononi mwa jeshi la polisi
Nae Makamo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita amewaasa akina mama kutowapendelea waume zao kwa dhamira kuwa watakosa baadhi ya mahitaji kwa kuwataja au kutoa ushirikiano kwa vyombo husika iwapo ametenda kosa la udhalilishaji na unyanyasaji katika jamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.