NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais
(TAMISEMI) Mheshimiwa Selemani Jafo, amewataka Walimu Wakuu wa Shule za Msingi
kote nchini, kutumia posho maalum ya madaraka ya Mwalimu Mkuu (Responsibility
Allowance) kuziwekeza benki ili hatimaye wajiinue kiuchumi kabla ya
kustaafu.
Mheshimiwa Jafo ameyasema hayo
jijini Dodoma Jumatatu Septemba 30, 2019 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA) ambapo
Wenyeviti wa Walimu Wakuu kutoka mikoa na wilaya waliwawakilisha wenzao.
“Leo hii kwa mara ya kwanza
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi mnapata posho maalum ya madaraka ya Mwalimu
Mkuu (Responsibility allowance), shilingi 200,000/= kila mwezi, unaweza kuamua
posho yako usiiguse na ukaenda Mwalimu Commercial Bank ukawaambia jamani
niwekeeni posho yangu hii nataka baadaye nijenge nyumba.” Aliwaasa walimu……na
kuongeza... “Nyie watu wa benki watafuteni walimu hawa muelewane nao, hatutaki
mwalimu ajenge nyumba mpaka anapostaafu, sasa muwawezeshe walimu wetu wajenge
nyumba,hata kabla ya mambo mengine na nyie watu wa benki mna fursa hiyo na leo
mpo na wenyeviti wa wakuu wa shule wapo, hapa kipa katoka goli liko
wazi…elewaneni nao leo hapa hapa tunataka hawa walimu kutokana na responsibility
allowance mwalimu apate kajumba kake na inawezekana” Alisema Mhe. Jafo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa aliwahakikishia
walimu kuwa benki hiyo ambayo ilianzishwa na walimu miaka mitatu iliyopita
imekuwa ikiimarika siku hadi siku ambapo miundombinu ya benki imekuwa imara
kuna huduma mbalimbali kama vile Mobile banking (kuweka fedha kwenye
akaunti kupitia mtandao wa simu), lakini pia kuweka mawakala kwenye maeneo
mbalimbali ili kuwafikishia huduma kwa urahisi.
“Ninyi wenyewe kama wadau wakwanza
wakubwa mishahara yenu ipitishieni kwenye benki yenu, msiwe kama mtu mmoja
aliyekuwa na hamu ya kuanzisha mgawaha, baada ya kuanzisha mgahawa badala ya
kula kwenye mgahawa wake akawa anakula kwenye mgahawa wa jirani, chombo chenu
mnatakiwa kukitunza kama vile mnavyoitunza taaluma yenu ili baadaye kiwe na
manufaa.” Alisema Bw. MakungwaWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mheshimiwa Selemani Jafo, (kushoto), akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko, Mwalimu Bank, Bi. Leticia Ndongole wakati akiwasili kufungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wenyeviti wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA) kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma Septemba 30, 2019. Walimu kote nchini pamoja na chama chao cha Walimu wanamiliki benki hiyo kwa zaidi ya asilimia 50 ambapo Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Richard Makungwa alitoa mada kuhusu elimu ya fedha na umuhimu wa walimu kutumia huduma za benki yao ili kufikia lengo la kuanzishwa kwake ambalo ni kuinua kipato cha walimu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mheshimiwa Selemani Jafo, akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wenyeviti wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango jijini Dodoma Septemba 30, 2019. "Ameihamasisha benki ya Mwalimu kuytumia fursa ya mkutano huo kuwashawishi walimu kutumia huduma za benki hiyo."
Baadhi ya Wenyeviti wa Walimu Wakuu w aShule za Msingi Tanzania Bara wakisikilkiza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wenyeviti wa Walimu Wakuu w aShule za Msingi Tanzania Bara wakisikilkiza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.
Afisa Mtendaji Mkuu, Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa, akizungumza na wajumbe wa mkutano huo.
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo, akizunguzma jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa baada ya kuhutubia mkutano huo. |
Afisa Mtendaji Mkuu, Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa (katikati), akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA), Bi. Rehema Remole (kushoto) huku Katibu Mkuu wa TAPSHA, Bi.Fatuma Kalembo akishuhudia wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa TAPSHA jijini Dodoma Septemba 30, 2019. Mwalimu Commercial Bank ilitumia fursa hiyo kutoa elimu ya fedha na kuwafahamisha walimu umuhimu w akutumia huduma za benki hiyo ambayo zaidi ya asilimia 50 ya umiliki wa benki hiyo uko chini ya walimu na chama cha walimu Tanzania (CWT)
Bw. Makungwa akizunhuzma jambo na Mwalimu Mselemu kutoka Mkoani Singida. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank, Bi. Leticia Ndongole.
No comments:
Post a Comment