Habari za Punde

Zao la kahawa linahitaji kuhamasishwa kwa wakulima

 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Dkt Makame Ali Ussi akizindua maonyesho ya zao la kahawa  kimataifa huko katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Mangapwani.
 Naibu Waziri  wa Wizara ya Kilimo Tanzania Bara Mhe.Omary T.Mgumba  akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya uzinduzi wa maonyesho ya zao la kahawa  kimataifa huko katika Hoteli ya Sea Cliff Mangapwani,
 Naibu Mkurugezi Mkuu wa Tantrade  Latifa M.  Khamis  akitoa maelezo kuhusu mafanikio ya zao la kahawa kwa Zanzibar kwa waandishi wa habari huko katika uzinduzi wa maonyesho ya zao la kahawa kimataifa huko katika hoteli ya sea cliff Mangapwani
Baadhi ya Washiriki wa maonyesho ya kahawa kutoka nchi mbali mbali wakisikiliza maelezo ya  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugi na Uvuvi Dkt Makame Ali Ussi (hayupo pichani)kuhusu  maonyesho ya zao la kahawa  kimataifa huko katika hoteli ya sea cliff Mangapwani.
Picha na Khadija Khamis Maelezo Zanzibar .

Na Mwashungi Tahir -  Maelezo      
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Dkt Makame Ali  Ussi amesema zao la kahawa linahitaji kuhamasishwa kwa wakulima ili liweze kupata umaarufu na kukuza uchumi wa nchi .
Akizungumza  baada ya ufunguzi wa  maonesho ya zao la kahawa katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff uliopo Mangapwani amesema zao hilo linaweza kukuza uchumi kwa kupata ajira kwa wananchi.
Amewataka wakulima kujishajihisha katika kilimo cha kahawa pamoja  na mazao mengine ya visiwani ili kuondosha uhaba wa chakula nchini.
Naibu waziri wa Kilimo wa Tanzania Bara Mh Omar Mgumba amewataka wakulima wa zao la kahawa kuzidisha bidii katika uzalishaji kwa kuweza  kuengeza kipato katika soko la ndani na nje ya nchi .
Akitoa wito kwa wakulima hao kuzingatie utaalamu walioupata kwa walimu wao ili kuongoza soko la ndani pamoja na kuongeza uzalishaji kwa wingi.
Naibu Mkurugenzi wa TanTrade Latifa  M. Khamis amesema fursa ya mafunzo kwa wauzaji wam kahawa  yataweza kuleta mafanikio kwa wauzaji hao pamoja na sekta ya utalii  kwa kupitia maonesho haya.
Amesema upatikanaji wa wataalamu ulio bora katika utengenezaji kahawa kutaweza kurudisha unywaji wa kahawa visiwani kwa kurudisha utamaduni wa Zanzibar .
Aidha amesema Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara na Viwanda imepokea na kusimamia mafunzo na maonesho kwa lengo la kutoa elimu kwa wauzaji na wapishi wa kahawa na kuweza kuwaimarisha  zaidi katika uandaaji wa kahawa .
“Vijana pendeleeni kunywa kahawa kwani kinywaji hichi kina faida nyingi mwilini na kinasaidia kupunguza mawazo na kutanua akili ”, alisema Naibu Mkurugenzi huyo.
Afisa mtendaji kutoka Uganda Bwana Kamal amesema lengo la kuwafanyia mafunzo wauzaji wa kahawa ni kuwapa utaalamu zaidi wa uandaaji wa kahawa ili kuzidisha kiwango cha watumiaji.
Aliwataka wakulima kutoa mashirikianoya pamoja  ili kuzidi kujipatia soko la ajira kwa vijana nchini kwa kuweza kufanya kazi  katika mahoteli ya kitalii.
Nao  Mwenyekiti wa Umoja wa wauzaji wa kahawa Yussuf Suleiman Ali wa mtendeni Unguja amesema maonesho haya yatawasaidia wafanyabiashara  kutengeneza kahawa yenye kiwango cha ubora na hadhi ya kimataifa
Zaidi ya Nchi 24 wameshiriki  katika maonesho hayo na kuonesha kahawa mbali mbali zikiwa na ladha za kila aina ambapo  maonesho hayo yamefadhiliwa na Wizara ya Biashara na Viwanda, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara TanTrade na Bodi ya Kahawa Tanzania .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.