Habari za Punde

China Yaja na Mkakati Kupambana na Vitendo Vya Ujangili Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke (katikati) akimkabidhi  Kamishna Mhifadhi wa Kanda ya Mashariki, Steria Ndaga moja ya  kompyuta mpakato  kati ya nne  ambazo zimetolewa na Ubalozi wa China kwa ajili ya kusaidia  katika mapambano dhidi ya Ujangili.

Na.lusungu helela

Ubalozi wa China nchini Tanzania  umeunga  juhudi za Serikali ya Tanzania katika  mapambano dhidi ya  ujangili kwa kuziwezesha jamii zinazoishi karibu na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa kuzipa  pembejeo za kilimo ikiwa pamoja na  kuzijengea uwezo wa kulima kisasa ili kuwasaidia wananchi hao kuacha kujihusisha na   vitendo vya ujangili.

Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati Ubalozi wa China nchini ukikabidhi msaada wa pembejeo za kilimo kwa  wananchi wa kijiji cha Mhenda katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro

Ubalozi wa China nchini Tanzania umetoa msaada wa mbegu  za mahindi yenye  ujazo wa kilo 2500, mbegu za alizeti  zenye ujazo wa kilo  150 pamoja  mbegu za choroko zenye ujazo wa kilo 800

Mbali na msaada huo, Ubalozi huo umetoa jumla ya jozi 13 za sare za ulinzi shirikishi, buti 13, komputa mpakato nne pamoja runinga moja

Mhe.Kanyasu amesema lengo la vifaa hivyo ni kuwasaidia wananchi kujikita katika kilimo cha kisasa kwa kutumia mbegu zenye ubora wa hali ya juu.

Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Kanyasu amesema  vifaa hivyo vitatumika katika kutoa elimu kwa wananchi katika mapambano dhidi ya vitendo vya ujangili.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameipongeza Jamhuri ya watu wa China kukomesha soko la meno ya tembo na kuamua kutoa msaada kwa wanavijiji ili nao waweze kuachana na biashara hiyo haramu.

Awali, Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke amesema pembejeo za kilimo walizozitoa itakwenda sambamba na mafunzo yatakayotolewa na wataalam kutoka China watakaowafundisha wanakijiji kulima kwa kisasa ili waweze kuachana na vitendo vya ujangili.

Ameeleza kuwa Ubalozi wa China umeamua kuanza na kijiji hicho ili kuwasaidia wananchi kuweza kuzalisha mazao mengi ili wasiweze kujiingiza katika vitendo vya ujangili.

Amesema China imeamua kuisaidia Tanzania katika mapambano ya vita dhidi ya ujangilli kwa vile watalii wanakuja nchini kwa ajili ya kuangalia wanyama, hivyo vitendo vya ujangili vinakwamisha juhudi za serikali katika kujiletea maendeleo.

Aidha, Balozi huyo ameipongeza Taasisi ya  Kova SUKOS Foundation inayoshughulikia majanga kwa kuratibu tukio hilo ikiwa pamoja na  kujitoa kuhakikisha wananchi wa Mhende wanakabidhiwa misaada hiyo itakayowasaidia katika kujiondoa katika umasikini huku utalii ukizidi kushamiri.

Naye Diwani wa kata ya Mhenda, Ali Athumani amemshukuru Balozi wa China kwa msaada huo na kuahidi kuwa watakuwa mabalozi kwa vijiji vingine vilivyo karibu na Hifadhi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhende kinachopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kabla ya kukabidhi  Pembejeo za kilimo pamoja na  vifaa vitakavyowasaidia Ulinzi shirikishi katika mapambano dhidi ya Ujangili.
Balozi wa China nchini Tanzania,  WaNG KE akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhende kinachopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kabla akiwaeleza wananchi kuwa Mabalozi kwa kujikita katika kilimo kwa kuendesha shughuli za kilimo kwa njia ya kisasa kwa kutumia mbegu za kisasa walizopewa na Ubalozi huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akikabidhi msaada wa runinga  Kamishna Mhifadhi wa Kanda ya Mashariki, Steria Ndaga ambazo zitatumika kwa  ajili ya kutolea elimu kwa njia ya video kwa wananchi wa kijiji cha Mhenda kuhusu athari zinazotokana na vitendo vya Ujangili. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi ya Taifa ya Mikumi, Mathew Mombona kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe.Adam Mgoi
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiteta jambo na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe.Wang Ke kabla ya kukabidhi vifaa vya ujangili pamoja pembejeo za kilimo kwa wananchi wa Kijiji cha Mhende wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akiwa pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang KE wakiwa kwenye pamoja na baaadhgi ya wananchi pamoja na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro.
(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.