Habari za Punde

Mbunge wa Viti Maalum Atoa Vifaa Kwa Madrasa ya Ghazal Jang'ombe Zanzibar

Na.Mwandishi Wetu. -Zanzibar.
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Viti Maalum Mkoa wa Mjini Mhe.Asha Abdalla Juma, amewataka walimu na wasimamizi wa madrasa zinazofundisha Elimu ya Dini ya Kiislamu nchini, kusimamia ipasavyo maadili ya wanafunzi wanaosoma katika madrasa hizo.
Rai hiyo ameitoa leo wakati akikabidhi vifaa mbali mbali vikiwemo Mabusati, Misahafu na fedha taslimu kwa madrasa ya Ghazal iliyopo Jang’ombe Zanzibar, ikiwa ni mwendelezo wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Mhe.Asha, aliwakumbusha walimu wa madrasa hizo kuhakikisha wanafunzi wanaowafundisha wanakuwa na maadili mema na kuwaepusha kuingia katika matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikichangia kuporomoka kwa maadili ya watoto na Vijana.
Katika maelezo yake Mbunge huyo Mhe.Asha, alisema maadili ya watoto yaanzia latika kuandaliwa vizuri katika misingi ya dini hivyo ni muhimu madrasa nchini zikajitathimini ni kwa kiasi gani zinasimamia maadili ya wanafunzi wao.
“Tunajua  changamoto zinazowakabili walimu wa madrasa hasa ukosefu wa kipato kwani wengi wenu, mnafanya kazi hizi za kuwalea watoto wetu katika misingi ya kiimani na dini kwa kujitolea bila mishahara wala posho la uhakika, lakini endeleeni nasi tutasaidia kulingana na uwezo wetu.”, alisema Mbunge huyo.
Akizungumzia vifaa alivyotoa Mhe.asha alisema ni mwendelezo wa kutekeleza Ilani ya CCM kwa kuhakikisha makundi mbali mbali    yanapata huduma bora za kijamii.
Kwa upande wa Uongozi wa Madrasa hiyo wamemshukru mbunge huyo kwa mchango wake na kuahidi vifaa vilivyotolewa kuvitunza ili viwasaidie wanafunzi wa madrasa hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.