Habari za Punde

Mkutano wa Wadau Kwa Kuhamasisha Takwimu za Kijinsia Wafanyakazi Zanzibar.

Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu za  Kijinsia na Kidemografia na kijamii Khadija Khamis Hamad akitoa hotuba ya ufunguzi wa  Mkutano wa Wadau kwa kuhamasisha Takwimu za Kijinsia Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Zanzibar Ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika ambapo itafikia kilele chake 18/11/2019. 
Na Mwashungi Tahir.
Jamii imetakiwa kuwa na utaratibu wa kufahamu takwimu zilizo sahihi katika maeneo yao na kuhakikisha kwamba takwimu hizo zinatolewa kwa ufasaha ili kuweza kutekeleza majukumu kwa uhakika.
Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa matumizi ya Takwimu za Kijinsia Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu za kidemografia na kijamii bi Khadija Khamis huko katika ukumbi wa  Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Mazizini  ikiwa ni shamrashamra ya wiki ya Takwimu ya Afrika ambapo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 18 Novemba.
Amesema lengo kuu la kuadhimisha siku hiyo ni kuinua uelewa wa jamii kuhusiana na umuhiku wa takwimu katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
Amesema katika kufanikisha juhudi hizo, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu imeweka kamati ya wataalamu ambapo kwa lengo la kusimamia na kuratibu ukusanyaji , uchambuzi na utumiaji wa kijinsia katika sekta zote zilizopo nchini.
Aidha amesema katika kuleta maendeleo  makundi yote yanapaswa kuwa na takwimu sahihi za kijinsia ambazo zitaweza kusaidia kuweka mipango ya maendeleo mijini na vijijini, wanawake na wanaume na watu wenye ulemavu.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Ofisi Mtakwimu Mkuu inachukuwa juhudi ya kuhakikisha kwamba takwimu bora zinapatikana nchini.
“Nawaomba washiriki wa mkutano huu kuhakikisha mnaweka  utaratibu wa kukusanya takwimu zilizo sahihi katika maeneo yenu na kuhakikisha kuwa takwimu hizo zinatumika ipasavyo.” Alisema Mkurugenzi huyo.
Nae Mwezeshaji Ramla Hassan kutoka Ofisi ya Mtakwimu akiwasilisha mada ya takwimu za kijinsia amesema takwimu sahihi husaidia  kutambua fursa na changamoto zilozopo baina ya wanawake na wanaume ili  kuleta mabadiliko katika kuzingatia usawa wa kujinsia.
Nao washiriki wa mkutano huo wamesema mafunzo hayo yatawasidia kukusanya takwimu sahihi katika maeneo yao na kuweza kujipanga kwa kuleta mabadiliko katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo Uzingatiaji wa maswala ya kijinsia katika ukusanyaji wa takwimu pamoja na  takwimu za ukatili na udhalilishaji wa kijinsia .
Mkutano huo ni wa siku moja ambao umewashirikisha Wadau mbalimbali ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kila mtu anahusika Takwimu zenye ubora ni muhimu katika kuhakikisha usimamizi mzuri wa uhamiaji wa lazima katika bara la Afrika”.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.