Habari za Punde

MBUNGE MZAVA AWATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUIENZI NA KUITUNZA AMANI



MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava kushoto akimkabidhi Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa ambaye ni Diwani wa Kata ya Majengo(CCM) Mustapha Shengwatu tuzo ya kutambua mchango mkuu huyo wa wilaya katika jamii ya wilaya hiyo juzi uliotunukiwa na Taasisi ya Korogwe Commnunity Foundation wakati wa uzinduzi wake kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo  Magesa Kuboja Sijo
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava kushoto akimkabidhi Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa ambaye ni Diwani wa Kata ya Majengo(CCM) Mustapha Shengwatu tuzo ya kutambua mchango mkuu huyo wa wilaya katika jamii ya wilaya hiyo juzi uliotunukiwa na Taasisi ya Korogwe Commnunity Foundation  wakati wa uzinduzi wake kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo  Magesa Kuboja Sijo
 MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava akizungumza wakati wa uzinduzi huo
 Mkurugenzi wa Taasisi ya  Korogwe Commnunity Foundation Magesa Kuboja Sijo akizungumza wakati wa uzinduzi huo

 Diwani wa Kata ya Majengo(CCM) Mustapha Shengwatu akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava kushoto akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa Taasisi ya Korogwe Community Foundation mmoja wa vijana kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Korogwe
SEHEMU ya waalikwa kwenye uzinduzi wa Taasisi hiyo
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava katika akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vikundi vya Kwaya mara baada ya kuzindua Taasisi hiyo
Kwaya ya Maranatha ya wilayani Korogwe Mkoani Tanga ikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Taaisis ya Korogwe Community Foundation uliofanyika mjini humo
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Timotheo Mzava amewataka watanzania kuendelela kuienzi na kuitunza amani iliyopo hapa nchini kwani ni tunu kubwa .



Mzava aliyasema hayo juzi mjini Korogwe wakati akizundua Taasisi ya Korogwe Community Foundation ambapo alisema kwamba lazima watanzania wasimame imara kwa maombi ili kumuomba mwenyezi Mungu aendelee kuifanya nchi kuwa na utulivu uliopo hivi sasa.



Mbunge huyo aliipongeza Taasisi hiyo ya Korogwe Community Foundation kwa mawazo waliyokuwa nayo ambayo yamezaa kitu kikubwa ambacho kimekuwakutananisha na ndio mambo anayoyatamani kuyaona huku akihaidi kuwaunga mkono kwenye dhamira yao hivyo.



Alisema kwani nchi ikikosa amani nchi hakuna watakaosoma, watakaofanya kazi, watakaozalisha na hivyo kupelekea uchumi kudodora hivyo tuendelea kumuomba mungu aendelee kuitunza na kulitabariki Taifa letu ili kuendelkea kubarikiwa kwenye shughuli zinazofanyika.



“Lakini pia tuendelee kuwaombe viongozi wetu akiwemo Rais na viongozi wengine kuwaombea waendelea kuwa na afya njema na kutimiza majukumu yao kwani wanafanya kazi kubwa sana kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi”Alisema Mbunge Mzava.



“Pia nyie waimbaji pamoja na kuimba kwenye makanisa na shughuli natamani vikundi vya kwaya viwe na Tassisi ambazo zinaweza kuwasaidia jamii na kuwa sehemu ya kujisaidia nyie wenyewe na jamii zenu”Alisema



Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na tukio la utoaji tuzo kwa kutambua mchango wa viongozi wa dini na serikali kutokana na kwamba kama kusingekuwepo na dini nchi isingekuwa na utulivu kama ilivyokuwa leo.



“Mnatusaidia sana sana kwenye kuponya na kulea roho zetu...kutusaidia kuwashika na kutusaidia waumini wetu tunatambua mchango wenu na mnafanya kazi kubwa na nzuri tunaitambua kama mnavyoshirikiana na taasisi ya Korogwe Community iendelee kushirikiana na viongozi wa serikali”Alisema Mbunge huyo.



Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Taasisi ya Korogwe Community Foundation Magesa Kuboja Sijo alisema kwamba taasisi hiyo imekuwa ikifanya mambo mbalimbali ya kijamii wilayani humo ikiwemo kuwasaidia wananchi wanaokumbana na changamoto mbalimbali.



“Lakini kwenye tukio la leo tumekutana hapa kwa madhumbuni makubwa ya kufunga mwaka na uzinduzi wa Taasisi ya Korogwe Community Foundation tulianza kama kikundi na sasa tutafanya kazi Tanzania nzima na tumekusanyika kupongezana na kushikana mikono “Alisema



Hata hivyo alisema pia lengo la pili la kukutana ni kufahamiana watumishi wa mungu hasa waimbaji kwenye Tamasha ikiwemo kuwapongeza watumishi wa mungu wachungaji, maaskofu, mapadre ambao wanafanya kazi kubwa ya kuliombe taifa wakati watu wamelala majumbani.



Naye kwa upande wake akizungumza wakati wa uzinduzi huo Askofu wa Kanisa la Evangelisti Assemblies Of God Majengo wilayani Korogwe Samweli Shemzigwa aliitakia mafanikio mema Taasisi huyo huku akiwatakia heri mwenyezi mungu andelee kuwainua kiuchumi kwa kuweza kupata kibali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.