Habari za Punde

TANESCO YAWATAHADHARISHA WANAOPENDA KUEGEMEA AU KUSHIKA WAYA ZA KUZUIA NGUZO ZA UMEME (STAY WIRE)

NA K-VIS BLOG
NIHATARI kuegemea au kugusa waya zinazoshikilia nguzo za umeme (Stay wire), Meneja wa Afya na Usalama Kazini, Shirika la Umeme Nchini Tanesco, Mhandisi Fredy Kayega (pichani) amesema.

Mhandisi Kayega ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo Desemba 24, 2019 wakati akizungumzia masuala ya usalama katika miundombinu ya umeme ya Tanesco na hatua ambazo wananchi wanapaswa kuzingatia ili kuendelea kufaidi huduma ya umeme bila madhara.

“Napenda kusisitiza kuwa tunaposafirisha umeme kuna waya tunaita Stay wire, waya huu hutumika kushikilia nguzo, waya huu hutoka juu ya nguzo mpaka chini ambapo huchimbiwa ardhini, na huwa kuna kifaa kinafungwa kinachoitwa stay insulator ambapo huhakikisha kwamba ikitokea kwamba ule waya (Stay wire) kule juu ukigusana na vile vyuma vyenye umeme kule juu basi umeme usiweze kushuka hadi chini.”

 Amefafanua na kuonya………………. ikitokea kuna mvua inanyesha na maji yakatiririka kupitia ule waya tunatambau kuwa maji husafirisha umeme kwa urahisi na kwakweli ule waya utakuwa na umeme na mtu anapougusa basi ni wazi kuwa ataathirika moja kwa moja.” Alisema Mhandisi Kayega.

Alisema wapo watu hudiriki kuegemea, na wakati mwingine watoto hutumia kubembea hii ni hatari sana. “Tunaweza kufikiria kuwa waya huu ni waya wa kawaida sana, fikra hizo si sahihi, waya huo unaweza kuleta madhara wakati wowote, Alionya.

Alisema kuna watu wamediriki kujenga humba huku waya huo ukiwea ndani, hii ni hatari waya huu kuna wakati utakuwa na umeme na Ili kuishi vizuri na miundombinu ya umeme ni vema wananchi tukawa mbali na miundombinu hiyo ili kujiepusha na madhara yanayoweza kutokea

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.