Habari za Punde


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi akijumuika pamoja na Watendaji wa Taasisi zilizochini ya Ofisi yake katika Tafrija Maalum ya Kuuaga Mwaka 2019 na Kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2020 huko nyumbani kwame Kama.
Na.Othman Khamis.OMPR.                                                                                            
Watanzania wote wametakiwa kuzingatia kwamba wanaingia ndani ya Mwaka Mpya wa 2020 wakiwa na dhamira ile ile ya kuwaunga Mkono Viongozi Wakuu wa Kitaifa katika kuendelea kutunza Amani na Utulivu unaobakia kuwa kigezo kwa Mataifa mengine Ulimwenguni.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika salamu zilizotolewa kwa niaba yake na Mshauri wake wa masuala ya Siasa Ndugu Vuai Ali Vuai kwenye tafrija maalum ya kuuaga Mwaka 2019 na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2020.
Tafrija hiyo ambayo huwa akifanya kila Mwaka huwaandalia Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi yake na kufanyika Nyumbani kwake Mtaa wa Kama nje kidogo ya Kaskazini mwa Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema wakati Watanzania wanasherehekea Mwaka Mpya wa 2020 baadhi ya Binaadamu katika Mataifa tofauti Duniani wamejificha ndani ya Mahandaki kufuatia vurugu zilizosababishwa na kuichezea Amani katika Mataifa hayo.
Alisema Wananchi lazima wailinde lulu hiyo kwa nguvu zao zote hasa katika kipindi hichi ambacho Taifa la Tanzania linaingia kwenye Uchaguzi Mkuu ifikapo Mwezi Oktoba Mwaka huu.
“ Hii ni faraja pekee  na kubwa waliyoipata Watanzania ambayo lazima wajitahidi katika kuichunga”. Alisisitiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Alisema Viongozi Wakuu wanaomalizia Muda wao wa Utumishi wa Umma wataona farari pale Kijiti cha jukumu hilo la Uongozi kitakabidhiwa kwa Vijana na Wananchi waliobeba Uzalendo wa kukubali kuutumikia Umma wakati wowote ule.
Balozi Seif alitanabahisha na kuwataka Wananchi zikiwemo Taasisi za Kijamii kujikita katika kuzidisha upendo, Umoja na Mshikamano wa Taifa bila ya kujali, rangi, kabila au dini ya Mtu au kikundi cha Watu.
Tafrija hiyo Maalum ya Kuuaga Mwaa 2019 na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2020 iliambatana na Burdani mahsusi ya Taarab na Beni { Maarufu Mbwa kachoka}.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.