Habari za Punde

UMOJA WA TANZANIA UJERUMANI UMEPANIA KUITANGAZA TANZANIA UMEKUATANA NA BALOZI DKT. ABDALLAH POSSI MJINI BERLIN

Balozi wa  Tanzania nchini Ujerumani Dr.Abdallah Possi akiwa pamoja Mwalimu Bi.Vanessa Upendo Fölsen ambaye ni mwenyeiti wa Umoja wa Tanzania Ujermani 
Mwalimu Bi.Vanessa Upendo Fölsen Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Ujerumani 1)

Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani (UTU ) Mwalimu Bi.Vanessa Upendo Fölsen siku ya jumamosi aliongoza kamati ya uongozi wa umoja huo katika kikao cha kukutana na balozi wa Tanzania nchini ujerumani Mheshimiwa Dkt.Abdallah Possi katika ubalozi wa Tanzania mjini Berlin,ambako ubalozi uliwakaribisha kwa mikono miwili na kufanya mazungumzo nao ambayo Kiongozi wa umoja wa Tanzania Ujerumani amelezea kuwa Umoja huo utaitangaza Tanzania nchini ujerumani kwa nguvu zote kwa maslahi ya Tanzania na watanzania,ususani katika sekta ya Utalii,uwekezaji,afya na elimu ni mojawapo ya mambo yakatayopewa kipau mbele,Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani ndio mwamvuli pekee unawakusanya watanzania waishio nchini ujerumani na moja ya niya yake ni kuleta mshikamano wenye kuleta maslahi kwa watanzania ujerumani na nyumbani Tanzania.Pia kwa upande wake Mheshimiwa Balozi Dkt. Abdallah Possi amewataka watanzania kuungana pamoja kwa maslahi yao na ya Tanzania,pia kujivunia utanzania wao kwa kuitangaza vema Tanzania na vivutio vyake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.