Habari za Punde

Balozi Mdogo wa China Zanzibar Azungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar Kuhusiana na Ugonjwa wa Corona.

Waandishi wa Habari wakiangalia Taarifa za Coronavirus China kupitia TV katika  Mkutano na Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu kuhusiana na maradhi ya Coronavirus yaliotokezea nchini China ambapo mpaka sasa hakuna Mtanzania ambae yuko China aliepata maradhi hayo hafla iliofanyika Ubalozi wa China Mazizini Zanzibar.
Balozi mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na maradhi ya  Coronavirus yaliotokezea nchini China ambapo mpaka sasa hakuna Mtanzania ambae yuko China aliepata maradhi hayo hafla iliofanyika Ubalozi wa China Mazizini Zanzibar. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano na Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu kuhusiana na maradhi ya Coronavirus yaliotokezea nchini China ambapo mpaka sasa hakuna Mtanzania ambae yuko China aliepata maradhi hayo hafla iliofanyika Ubalozi wa China Mazizini Zanzibar.
                                              Na.Yussuf Simai -Maelezo Zanzibar.
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.
Ubalozi wa Mdogo wa China uliopo Zanzibar umesema hakuna Mzanzibari yoyote alieathirika kutokana na maradi ya mripuko ya Corona yalioibuka hivi karibuni katika nchi hiyo.
Hayo yameelezwa na Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mr. Xie Xiawu huko Mazizizini Wilaya ya Magharibi B wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maradhi hayo.
Alisema katika nchi ya china kuna watanzania 4000 kati ya hao 400 ni wanafunzi na wote wapo salama.
 “Wazee wasiwe na hofu kwa watoto wao hadi sasa hakuna mtanzania yoyote alio pata maradhi hayo na wako salama na wanaendelea vizuri kwani Serikali ya China inawaangalia kwa umakini”,alisema Balozi huyo.
Alisema hawapendi kuona maradhi hayo yanaendelea kuathiri wananchi wengine,lakini alisema kuwa iwapo imetokea Mtanazania ameathirika atatibiwa kwa ustadi mkubwa ili kuokoa maisha yake.
Aidha alisema serikali yao ikomakini juu tahadhari ya kuepuka maradhi hayo yasiendelee maeneo mengine nipale serikali yao kujenga hospitali kubwa kwa muda wa siku kumi kwa kuwapeleka waathirika wamaradhi hayo na kuwahudumia kwa matibabu ya hali ya juu kabisa.
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Drk. Juma Muhamed Salum aliwambia amewakumbusha Wandishi wa habari kuandika habari  kwa kuondoa maumivu yawale walio athiriwa na maradhi hayo nasio kushabikia bila ya kueleza ukweli na kutofuta sheria za uandishi.
Alisema waandishi waunge mkono kupigavita ya kushinda maradhi hayo mabaya ambayo madaktari bingwa wamo kuyapatia ufumbuzi kuyashinda.
Mkurugenzi huyo aliipongeza ubalozi huo kwa kuwatoa hofu wazanzibar na watanzania kwa ujumla kwa kusema china iko wazi katika majibu ya mambo yake kwa kutekeleza kwa vitendo kaulizake za uhakika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.