Habari za Punde

BANK OF AFRICA TANZANIA YAFANIKISHA MKAKATI WAKE WA KUIMARISHA NA KUBORESHA BIASHARA ZAKE NCHINI

Bank of Africa Tanzania Limited, imeeleza  kuwa iko madhubuti kutekeleza mpango wake wa kuendesha biashara zake kwa ufanisi zaidi nchini sambamba na kutoa huduma bora na za kisasa na kuishukuru serikali, na wadau wote  ambao imekuwa ikishirikiana nao kwa  katika kipindi chote cha miaka 13 tangia benki yetu ianze kutoa huduma za kibenki nchini

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, benki hiyo ilikuwa na mtaji wa kutosha unaotakiwa kwa kutoa huduma za kibenki nchini.Hesabu za benki zlionyesha ilikuwa na mtaji wenye uwiano wa asilimia 17% dhidi ya unaotakiwa na mamlaka ya udhibiti wa mabenki wa asilimia 14.5%, katika kipindi cha mwaka jana wamiliki wa benki waliongeza mtaji wa shilingi  Bilioni 22.9 kwa lengo la kuiwezesha kutoa huduma ya mikopo na kuboresha huduma.

 Benki ina mzunguko mzuri wa mtaji unaofikia uwiano wa asilimia 33% dhidi ya mtaji unaotakiwa na mamlaka ya udhibiti wa asilimia 20%.

Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo,Mr. Joseph Iha,amesema mtaji wa jumla wa benki ulikua kwa asilimia 23% katika kipindi cha mwisho wa mwaka 2019 na kufikia Shilingi Bilioni 564, mafanikio hayo yalitokana na ongezeko la akiba za wateja  na huduma za mikopo.

Huduma za mikopo zilikua kwa asilimia 4.4% na kufikia Shilingi Bilioni 277 mwishoni mwa mwaka. Mikopo mingi iliyotolewa ililenga kuwezesha makundi ya biashara ndogo na za kati, lengo likiwa ni kufanikisha kukuza uchumi wa nchi. Ongezeko la akiba za wateja lilikuwa kwa asilimia 17.5% na kufikia Shilingi Bilioni 390 na ongezeko la  fedha za mtaji kutoka kwa wamiliki wa Benki uliongezeka kutoka Shilingi Bilioni 68 mwaka 2015 na kufikia Shilingi Bilioni 74 mwaka 2019.

Alisema,hadi mwishoni mwa mwaka 2019, benki ilipunguza  uwiano wa mikopo chechefu kufikia Shilingi Bilioni 12 ambayo ni asilimia 9.2% kulinganisha na asilimia 16% ya mikopo hiyo iliyokuwa nayo katika kipindi cha  kufikia mwishoni mwa  mwaka 2018, kiwango hiki kiko  chini ya kilichozoeleka kwenye soko cha asilimia 10%.Mikopo chechefu hadi mwishoni mwa mwaka ilipunguzwa kwa zaidi ya asilimia 90%.

Benki imekuwa ikipata faida katika kipindi cha miaka 5 kuanzia mwaka 2015.Faida iliyopatikana baada ya kulipa kodi ni kiasi cha shilingi Bilioni 12 katika kipindi cha miaka 3 kuanzia 2015 hadi 2017, ambayo ilitokana na ukuaji wa uendeshaji wa huduma za kibenki kila mwaka kwa asilimia 9% au Shilingi Bilioni 47.Katika kipindi cha mwaka 2018 na 2019,benki ilifanya jitihada za kuhakikisha huduma za mikopo zinaboreshwa,mchakato huo katika kipindi hicho cha mpito uliathiri faida ya benki”alisema Inya.

 
Aliongeza kuwa kwa kuelewa umuhimu wa kujumuisha wanachi kiuchumi, Bank of Africa Tanzania Limited, mwaka jana ilifanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya dola  za Kimarekani milioni moja katika miundombinu yake ya Teknolojia ya Habari (TEHAMA) kuwezesha huduma zake kupatikana kwa wateja kwa urahisi. Benki imeweka kufunga mashine za kutolea fedha (ATM) za kisasa katika mtandao wa matawi yake yote nchini,i meanzisha huduma za kibenki za kidigitali na kuimarisha utunzaji wa taarifa zake kwa njia za kisasa zaidi.

Bank of Africa Tanzania Limited, ambayo iko chini ya kampuni mama ya  Bank of Africa Group, yenye mtandao wa biashara za mabenki katika nchi 18 za Afrika, itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake wa makundi mbalimbali kuanzia makampuni makubwa,wafanyabiashara wadogo na wa kati kupitia mtandao wake wa matawi 25 yaliyopo katika mikoa 11 nchini Tanzania. Bank of Africa Group, imekuwa ikishiriki kukuza biashara barani Afrika kuanzia mwaka 1985 na Bank of Africa Tanzania Limited itaendelea kufanikisha ajenda hiyo kupitia mpango mkakati wake wa miaka mitatu unaoanzia mwaka 2019-2021.

Baada ya kufanikiwa kuichukua benki iliyokuwa ikijulikana kama EURAFRICAN Bank, mnamo mwaka 2007, Bank of Africa imewekeza kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania,na kubuni huduma za kisasa za wateja zinazokubalika nchini kote.

Benki inajivunia kuendelea kupata mafanikio kutokana na kuwa chini ya kampuni mama kubwa ya BMCE BANK OF AFRICA, ambayo inaendesha shughuli za kibenki kwa mafanikio katika nchi 18 za Afrika. Kampuni ya Bank of Africa Group, imekuwa katika biashara kwa miaka ipatayo 36 sasa kiwa na mtandao wa matawi zaidi ya 560 na mtaji wa rasilimali unaofikia Euros Bilioni 7.6 ambao umekuwa ukikua mwaka hadi mwaka pia kampuni mama imekuwa na mikakati  ya kuendesha biashara zake katika nchi 18 ilipowekeza  kwa mafanikio ikiwemo nchini Tanzania. Mtaji uliotolewa na wanahisa wa benki kwa BOA Tanzania, mwezi Septemba mwaka 2019,kunadhihirisha dhamira yak mkakati wake wa kukuza biashara zake nchini. 

Dira na Mkakati wa kampuni mama ni kuendeleza wadau wake mbalimbali inaoshirikiana nao kibishara,kuleta msukumo wa kukuza uchumi katika nchi inazofanyia biashara zake,kutoa huduma za kisasa kwa wateja wake na kuhakikisha inakuwa benki bora katika masoko yake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.