Habari za Punde

SMZ Yaombwa Kutoa Elimu Kuhusiana na Maradhi ya Corona (COVID -19 ) Kwa Wanawake na Watoto.

Na.Takdir Suweid -Maelezo Zanzibar.
Zanzibar imeombwa kuweka mikakati maalum ya kutoa elimu ya Corona kwa Wanawake na Watoto ili waweze kujikinga.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Viti maalum Sada Ramadhan Mwendwa wakati alipokuwa akitoa Taarifa kwa Vyombo vya habari kuhusiana na maradhi hayo.
Amesema inapotokezea majanga wanaoathirika zaidi ni Wanawake na Watoto hivyo elimu hiyo itawawezesha kupata mbinu za kuweza kujikinga Virusi vya Corona vinavyosababisha maradhi ya COVID 19.
Aidha amewakumbusha wanajamii kufuata maelekezo yanayotolewa na Wataalamu wa Afya katika maeneo yao ikiwemo kuepuka Mikusanyiko ili kuweza kuendelea na shughuli zao na kubaki kuwa salama.
Mbali na hayo amewaomba Waalimu wa Skuli na Madrasa kutii agizo lililotolewa na Serikali la kuwafungia Wanafunzi wao ili kuondosha Msongamano katika maeneo hayo.
Hata hivyo amewakumbusha Wazazi kushirikiana  katika kushughulikia Watoto wao ili kujikinga maradhi hayo ambayo ni Janga la Dunia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.