Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akisalimiana na
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, Hasna Mwilima, nje ya Ukumbi wa Bunge, jijini
Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akijipaka kitakasa
mikono (Sanitizer) nje ya Ukumbi wa Bunge, jijini Dodoma, leo, kabla ya kuanza
kwa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Kikao cha Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, leo. Wizara
iliwasilisha katika kikao hicho Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa
Fedha 2020/21. Katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Salim Mwinyi Rehani,
na kulia ni Katibu wa Kamati hiyo, Ramadhani Abdalla.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Christopher Kadio (kulia), na Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wanja
Mtawazo, wakipanga nyaraka kwa ajili ya kuziwasilisha katika Kikao cha Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, leo. Wizara
iliwasilisha katika kikao hicho Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa
Fedha 2020/21.
Wakuu
wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Waziri wa Wizara
hiyo, George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa anazungumza katika Kikao
cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto) akimsikiliza Katibu wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Ramadhani Abdalla
(kulia) alipokuwa anamfafanulia jambo kabla hya kuanza kwa Kikao cha Kamati
hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa, Bungeni jijini
Dodoma, leo. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio,
na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wanja Mtawazo.
Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment