Habari za Punde

Balozi Seif: Kukaa Karantini sio Adhabu


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Umma baada ya kumaliza Mapumziko yake ya Siku 14 zilizomuwajibikia kwa kila Mtu aliyeingia Nchini kutoka Nje ya Nchi ndani ya kipindi cha mtikisiko wa Virusi vya Corona.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amewatahadharisha Wananchi kuzingatia kwamba Karantini wanaowekewa watu walioingia nchini kutoka nje ya nchi sio adhabu  bali ni utaratibu unaozingatia Muongozo wa Wataalamu wa Afya katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona vinavyosababisha Mafua na Homa Kali ya Mapafu. 

Balozi Seif Ali Iddi ametoa tahadhari hiyo huko Nyumbani Kwake Mtaa wa Kama Kaskazini Kidogo ya Mji wa Zanzibar  wakati akitoa Taarifa kwa Umma baada ya kumaliza muda wake wa wa mapumziko ya Siku 14 zinazomuwajibika Kila Msafiri aliyeingia Nchini kutoka nje ya Nchi kwa mujibu wa Wataalamu.

Hata hivyo Balozi Sif alisema kwa mujibu wa Wataalamu wa Sekta ya Afya walimshauri aendelee kuongeza Siku Saba zaidi ili kumaliza vyema Karantini hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Mawaziri wa Afya wa Serikali ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada wanazoendelea kuzichukuwa katika kuipatia Jamii Taarifa sahihi juu ya muenendo mzima wa Virusi vya Corona.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
April 02, 2020

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.