Habari za Punde

MEYA RYATA: TUMEJIDHATITI KUKABIRIANA NA CORONA MAENEO YA KIBIASHARA.

Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Ryata  akiwa anatekeleza tukio la kupulizia dawa ya kutokomeza virusi vya Corona kwa lengo la kuwapa uhuru wafanyabiashara wadogo kufanya biashara kwa lengo la kukabiriana na maambukizi
 Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Ryata akipulizia dawa kutokomeza virusi vya Corona katika eneo la stand ya Daladala Manispaa ya Iringa.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
WAFANYABIASHARA wadogo wadogo wa soko la Mashine Tatu maarufu kama Machinga mkoani Iringa wameiomba Serikali kupitia wataalam wa Afya kuongeza kasi ya uelimishaji wa namna sahihi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona ili kuwaepusha wafanyabiashara hao na wateja wao kupatwa na maambukizi.

Wakizungumza na blog hii miongoni mwao wameeleza kuwa kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo katika eneo hilo baadhi ya wateja na hata wafanyabiashara wamekuwa wakipuuza baadhi ya maelekezo ya kujikinga na maambukizi hali inayozua hofu endapo akitokea mgonjwa mwenye Virusi vya Corona.

Aidha kwa upande wa katibu mkuu wa Mtandao wa Machinga mkoani Iringa Joseph Kilienyi Mwanakijiji ameipongeza Serikali ya mkoa kwa hatua za awali huku akitoa mwito kwa wadau kuangalia namna ya kusaidia upatikanaji wa vifaa ikiwemo ndoo na sabuni ili viongezwe ili kukidhi mahitaji halisi.

Kirienyi amesema kuwa licha ya Serikali kutoa elimu na kuwapatia baadhi ya vifaa bado uhitaji ni mkubwa hasa katika eneo hilo la soko la mashine tatu kutokana na idadi ya watu wanaoingia na kutoka kwa ajili ya mahitaji mbalimbali kupindukia Elfu sita kwa siku.

Hata hivyo amesema wameendelea kushirikiana na Serikali kwa kuwahimiza wafanyabiashara kuzingatia taratibu zote za msingi ikiwemo ya kuwakumbusha wateja wao kuosha mikono na kuepuga kugusana pamoja na tahadhali nyingine kama Serikali Ilivyoagiza.

Aidha kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Nzala Ryata akizungumzia hatua walizochukua mpka hivi sasa ni pamoja na kuwatumia watu wenye ushawishi zaidi kwenye jamii ikiwemo viongozi wa kidini na wazee wa kimila kwa ajili ya kuelimisha umma kupitia nafasi zao.

Kuhusu maeneo ya kibiashara Ryata amekiri kuwapo kwa changamoto ya elimu na muitikio sahihi hasa maeneo kama ya masoko likiwemo hilo la mashine tatu lakini ameeleza kuwa Manispaa imebandika matangazo yanayoonesha hatua muhimu za kuzingatia kijikinga na Virusi hivyo hatari vinavyosababisha maradhi ya Covid 19.

Aidha Meya Ryata amesisitiza kuwa kwa sasa wameendelea kuwasiliana na Viongozi wa makundi mbalimbali kwa ajili ya kusikia changamoto zilizopo hasa katika kipindi hiki kusikia maoni yao na kuwashari mambo ya kufanya ili kila mmoja awe wa kwanza kujilinda na maambukizi ya corona hatua itakayowaidia kuendelea kufanyabiashara zao huku wakijilinda na hatari ya maambukizi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.