Habari za Punde

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 24.04.2020: Werner, Willian, Sancho, Vertonghen, Dalot, Coutinho

Timo Werner asema yupo tayari kuhamia Liverpool
Mshambuliaji wa RB Leipzig, Timo Werner,24, yuko tayari kujiunga na               Liverpool iwapo italipa pauni milioni 52 ya kuvunja mkataba wake na RB. (Sky Sports)                                                                                                                                           
Kiungo mchezeshaji wa Chelsea na Brazil Willian,31, yuko kwenye mazungumzo na Liverpool kuhusu uhamisho wake, mkataba wake utakapokwisha. (Sport - via Mirror)
Manchester United wanafikiria kumuuza mchezaji wa nafasi ya ulinzi Diogo Dalot, 21, kwenda Paris St-Germain. (Daily Mercato)
Dortmund kumpatia fedha zaidi Sancho ili kubaki klabuni hapo.
Borussia Dortmund wako tayari kumfanya winger Jadon Sancho kuwa mchezaji wao wa pili anayelipwa pesa nyingi ili aendelee kubaki kwenye klabu hiyo, licha ya kutolewa macho na Manchester United na Chelsea. (Forbes)
Philippe coutinho anaweza kurejea katika kiwango chake kama mchezaji huyo,27, kiungo ataondoka Barcelona na kujiunga na Chelsea, kwa mujibu wa Rivaldo. (Sun)
Liverpool wamemwambia Coutinho hawana nia ya kumnunua tena kutoka Barcelona. (Sport Witness)
                               Coutinho anamezewa mate na Chelsea
Mchezaji wa zamani wa nafasi ya ulinzi kikosi cha Liverpool na Chelsea Glen Johnson amewataka the Blues kumsajili Coutinho (Talkssport-via Express).
Leicester wanajiandaa kuchuana na Manchester United kumfukuzia mshambuliaji wa Borussia Monchengladbach Alassane Pea, 27. (Le10 Sport - via Leicester Mercury)
                                Jack Grealish kuitosa Villa na kwenda United?
Manchester United watamchezesha kiungo wa Aston Villa Jack Grealish, 24, kama winga wa kulia ikiwa watamaliza makubaliano ya kumnyakua mchezaji huyo. (Athletic - vial Birmingham Mail)
Juventus wanapima kuingia mkataba na mshambuliaji wa Poland na Napoli Arkadiusz Milik,26. (Calcio Mercato)
Henrikh MkhitaryanKiungo wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan, 31, ana matumaini kubaki Italia na kikosi cha Roma msimu ujao.
Wakati mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya Manchester United Chris smalling ,30, pia ni sehemu muhimu ya mipango ya timu inayocheza Serie A.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.