Habari za Punde

Virusi vya Corona: Jinsi damu ya mtu aliyepona corona inavyoweza kuwa tiba

Uingereza inaanza majaribio ya kutumia damu ya waliopona virusi vya corona kuwatibu wagonjwa walio na maambukizi hayo ambao wapo hospitali.
Taasisi ya damu na upandikizaji ya Uingereza inawataka watu waliopona homa ya mapafu, covid-19 kuchangia damu ili waweze kutathimini tiba hii iliyo kwenye majaribio.
Matumaini ni kwamba molekyuli walizozitengeneza zitasaidia kupambana na virusi vilivyo kwa wengine.
Marekani tayari imeanza mradi mkubwa wa utafiti huu, ikihusisha hospitali 1,500.
Mtu anapokuwa na virusi vya corona, mfumo wa kinga hutengeneza molekyuli, ambazo huvishambulia virusi.
Kwa kipindi fulani molekyuli hizi zinaweza kupatikana kwenye plazma, sehemu ya majimaji ya damu.
Taasisi ya damu na upandikizaji sasa inawasiliana watu waliopona Covid-19 kuona kama plazma zao zinaweza kutolewa na kupewa wagonjwa wengine wanaoumwa ugonjwa huo.
Taarifa ya taasisi hiyo imesema: ''tunatafakari uwezekano kwamba hii itatumika awali kama tiba ya Covid-19. ''Ikiwa itaidhinishwa,majaribio yatafanyika kuchunguza kama plazma hizo zitasaidia kuongeza kasi yakuimarisha afya ya mgonjwa aweze kupona haraka.
''Kila majaribio yanapaswa kufuata mchakato wa kuidhinishwa ili kuwalinda wagonjwa na kuhakikisha matokeo ya uhakika yanapatikana. Tunafanya kazi kwa ukaribu na serikali na vyombo vyote vinavyohusika kupitia mchakato wa kupata idhini haraka iwezekanavyo.''
Chanza cha Habari BBC,

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.