Habari za Punde

WHO ilijua kuhusu virusi vya corona miaka miwili iliopita

Mnamo mwezi februari 2018, kundi la wataalam wa shirika la Afya duniani WHO lilichapisha orodha ya magonjwa ambayo yanapaswa kupewa kipau mbele katika uangalizi na utafiti kutokana na tisho kubwa yanayotoa.
Orodha ya magonjwa manane ilishirikisha Ebola, Zika, homa ya Lasa, Homa ya Rift Valley, Homa ya Crimean Congo, ugonjwa wa nipha na magonjwa ya mapafu ya SARS na MERS,
Lakini ugonjwa mmoja zaidi ulikuwepo na ukapewa jina X.
Ugonjwa huo WHO ilisema kwamba utatoa mlipuko hatari wa kimataifa na utasababishwa na viini vinavyoweza kusababisha maambukizi miongoni mwa binadamu.
Miaka miwili baadaye, tukiwa na ugonjwa uliosababisha maambukizi ya takriban watu milioni 2, swali ni je, tunaishi na ugonjwa X ambao WHO ulitarajia?
''Kweli Covid 19 ndio ugonjwa uliopewa jina X'', alisema Dkt Josie Golding, mkuu wa magonjwa ya milipuko katika shirika la kufanya tafiti mjini London akizungumza na BBC.
''Ugonjwa X lilikuwa wazo ambalo liliwakilisha kitu kisichotarajiwa ambacho hatukukijua'', anaongezea.
Na sasa vile tumeona jinsi visa vya wagonjwa vilivyoongezeka baada ya kutambua na kufanya utafiti kujua ni ugonjwa wa aina gani, nadhani Covid 19 ndio ugonjwa X.
Wakati wa kikao kimoja cha WHO, kilichofanyika mjini Geneva 2018, Kundi la wataalam kutoka kwa mpango wa maandalizi ya WHO walijadiliana na kukubaliana kuhusu ugonjwa unaofaa kupewa kipaombele kwa uangalizi na utafiti.
Watafiti hao walipiga kura kuchagua ugonjwa huo kulingana na Dkt Alfonso Rodrigues Morales, ambaye alikuwa miongoni mwa kamati ya wataalam wa majadiliano hayo na alikuwepo katika kikao hicho cha 2018, aliambia BBC Idhaa ya Mundo.
Kupatikana kwa orodha hiyo kulitegemea vigezo kadhaa vilivyotumika.
''Tulitafuta magonjwa kadhaa ambayo yalionekana kuwa muhimu, na tukaanza na orodha'', alisema profesa huyo wa afya ya umma na maambukizi katika chuo kikuu cha teknolojia cha Pereira, nchini Colombia ambaye pia ni makamu wa rais wa muungano wa magonjwa ya maambukizi nchini Colombia.
Katika orodha hiyo kulikuwa na magonjwa kama vile Chikungunya, magonjwa ya virusi na magonjwa mengine mengi.
Lakini mwishowe kundi hilo la wataalam wa magonjwa lilipiga kura na kulikuwa na orodha fupi ambayo tulipatia ugonjwa X.
Rodriguez Morales alikubaliana na Goldinga kwamba , bila wasiwasi Sars-Cov-2 na Covid 19 yaliorodheshwa katika ugonjwa X , wataalam hao walithibitisha kwa Mundo.
Vigezo vilitaraji kwamba hali ya mlipuko itaweza kukabiliwa licha ya mapungufu yaliopo luhusu makabiliano na vipimo.
Lengo la orodha hiyo ya WHO ni kujiandaa kukabiliana na dharura ya ugonjwa huo.
Na iwapo ilitarajiwa kwamba ugponjwa kama Covid 19 ulikuwa hatari miaka miwili iliopita , je dunia ilijiandaa
''Kuuorodheshwa kwa ugonjwa X katika orodha ya WHO ilikuwa hatua sahihi na ilioshawishi jinsi makampuni yalivyojiandaa kutoa chanjo na tiba'', alisema Dkt. Josie Goldinga wa Wellcome Trust.
Kampuni ziliundwa kukuza uzalishaji wa chanjo na tiba huku mipango ikiwekwa kuchunguza wanyama na kujaribu kutambua viini na virusi tofauti ndani yake.
''Lakini lazima tuangalie nyuma na kusema tungefanya mengi zaidi'' , alikiri kwa BBC Mundo.
''Tungehusika zaidi katika kufadhili juhudi za maandalizi duniani, ikiwemo njia za kugundua viini vipya ambavyo vingezuka'', alisema.
Ni kweli kwamba wataalam wanakubaliana na kwamba kwa jumla makabiliano dhidi ya mlipuko huo hayatoshi.
Kama anavyoelezea Alfonso Rodrigues , hatukufikiria kwamba ugonjwa X ungezuka katika kiwango cha kuwa mlipuko.
Tatizo ni kwamba kabla ya mlipuko huo, watu hawakufikiria kama janga kama hilo linaweza kuzuka, wataalam waliambia BBC Mundo.
Kwasababu kwa bahati mbaya hadi mlipuko unapozuka, watu wengi huwa hawaamnini athari ambazo unaweza kusababisha.
Hili, wanasema wataalam limeonekana katika siku za nyuma wakati wa mlipuko wa Chikungunya 2013 na zika 2015 ambayo ilizuka katika bara la America na kusababaisha athari mbaya.
Maafisa wengi wa afya katika mataifa tofauti duniani hawakutambua ugonjwa wa Chikungunya na haukupewa umuhimu.
Ilidhaniwa kwamba barani Afrika, virusi hivyo havikuwa na athari mbaya na kwamba havingefanya uharibifu wowote Amerika.
Lakini hatuwezi kujua athari zote ambazo zinaweza kusababishwa na mlipuko wa virusi, wanasema wataalam.
Katika kukabiliana na mlipuko wa Covid kumekuwa na mafanikio na makosa kulingana na Dkt Golding.
''Nadhani tungejivunia jinsi virusi hivyo vilivyogunduliwa na kutambulika kwa haraka licha ya kwamba kitu tofauti kilikuwa kikijitokeza katika hospitali za China-mlipuko wa homa ya mapafu isiojulikana''.
Lakini wakati huo makosa yalifanyika katika vifaa vya kutambua ugonjwa huo.
''Tumegundua kwamba inachukua muda kupata kifaa kinachoaminika na ijapokkuwa kulikuwa na vituo kote duniani ambavyo vilifanya kazi nzuri , tumoena kwamba vifaa vingi vya kupima vimehitajika katika vituo kuwaangalia wagonjwa''.
''Kumekuwa na pengo kubwa na pengine tunapoangalia siku za usoni , tutasema tungekuwa tumejiandaa vyema katika vipimo'', anasema Golding.
Chanzo cha Habari.BBC.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.