Habari za Punde

Wazazi Watakiwa Kuwasimamia Watoto Wao Wenye Ulemavu Kuzurura Mitaani.

Na.Takdir Suweid - Maelezo Zanzibar.
Wazazi na Walezi wa Watoto wenye ulemavu nchini wametakiwa kuwasimamia Watoto wao ili kuhakikisha wanapata elimu na kuepukana na kudhurura mitaani.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar Abeida Abdallah Rashid wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari huko Ofisini kwake Migombani Wilaya ya Mjini.
Amesema katika kupambana na janga la Corona Serikali imeweka mpango wa kutoa elimu kupitia vyombo vya habari hivyo ni vyema Wazazi kuiunga mkono Serikali kwa kuhakikisha watoto wao wanafuatilia na kuweza kupata elimu.
Aidha amesema mpango huo utawasaidia Watoto wa kubakia majumbani kupata elimu na kuepuka mikusanyiko jambo ambalo litaweza kuwakinga na maradhi ya Corona.
Hata hivyo amewaomba Viongozi wa Shehia kuwashajiisha Wazazi ambao hawana mwamko kwa katika kutumia mpango huo ili malengo ya Serikali yaweze kufikiwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.