Habari za Punde

Ifahamu Kampuni ya Simu ya Zantel Tanzania.

 
Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.

Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikianona benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.

Aidha,Miundombinu hiyo  imeiwezesha Zantel kutoa huduma za kimataifa za sauti na data kwa jumla kwa kampuni nyingine na nchi jirani hivyo kuchagiza ukuaji wa teknolojia ya digitali 

Kwa Mawasiliano zaidi kuhusu Zantel tembelea tovuti; www.zantel.co.tz  
Rukia Mtingwa – Manager Brand and Communication 
Mobile: +255 774 55 9999

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.