Habari za Punde

Zantel Yazindua Ofa Maalum Katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Ofa. Wateja kuwasiliana kwa gharama nafuu na kupatataarifa mbalimbali za mfungo

    Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa Zantel, Bi. Rukia Mtingwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ofa maalumu ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan leo jijini Dar es Salaam. Ofa hiyo mpya itawapa wateja uhuru zaidi wa kuwasiliana pamoja na kupata taarifa muhimu kuhusu kipindi cha mfungo kama nukuu za Quran, pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa Swala, kufturu na mwisho wa kula daku.     
  
Zanzibar.23 Aprili 2020.Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, leo imezindua ofa maalumu yamwezi mtukufu wa Ramadhan kwa wateja wake ili kuwawezesha kufanya mawasiliano kwa gharama nafuu pamoja na kupata taarifa mbalimbali zenye kujenga imani zao katika mwezi huu mtukufu

Ofa hiyo inawapa wateja uhuru wa kuwasiliana zaidi pamoja na kupata taarifa muhimu kama vile nukuumbalimbali za Koran takatifu pamoja na jumbe za kuwakumbushamuda wa swala na ujumbe wa sauti utakaoingia kwenye simu zao kama simu nyakati za iftar na nyakati za daku

Akizindua ofa hiyo mjini Zanzibar, Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussaalisema ofa hiyo itawasaidia waumini wa dini ya kiislamu kuimarisha zaidi mahusiano baina ya ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki cha mfungo.

“Zantel inapenda kuwatakia waislamu wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunatambua mwezi huu ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki hivyo ofa hii itahakikisha kwamba wateja wetu wanawasiliana bila mipaka na pia kuwapa taarifa zitakazosaidia kujiimarisha kiimani ili kufanikisha funga zao,” alisema Mussa.

Naye, Meneja bidhaa na huduma wa Zantel, Aneth Muga alisema ofa hiyo itawazawadia wateja watakaojiunga na vifurushi vilivyoboreshwa zaidi vya siku, wiki na mwezi ambapo mbali na muda wa maongezi watajipatia nukuu za Koran takatifu pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala tano.

“Tumeboresha zaidi vifurushi vyetu ili kuwapa wateja sababu zaidi za kuwasiliana msimu huu.Kwa wateja watakaojiunga kifurushi cha siku kwa Shilingi 1,000/- watajipatia dakika 150, SMS 100 pamoja na nukuu moja ya Koran, jumbe tano za kukumbusha muda wa swala,” alisema Muga.

Vilevile, kwa kifurushi cha wiki cha Shilingi2,000 mteja atapata dakika 250, SMS 200 huku kifurushi cha mwezi cha Shilingi 10,000/- atapata dakika 1,250, SMS 500 pamoja na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takataifu, jumbeza kuwakumbusha muda wa kufuturu pamojaza kukumbusha muda wa swala.

Ili kujiunga na ofa hii mteja wa Zantel apige *149*15# na kuchagua namba 1 ambayo ni Ramadhani ofa na atajiunga na kifurushi anachohitaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.