Habari za Punde

Eric Yuan, Bilionea Aliyetajirika Kutokana na Corona na Kwa Nini Aliomba Msamaha

Eric Yuan aliingia katika orodha ya Forbes ya mabilionea akiwa na takriban thamani ya dola bilioni 7.8.

Wiki chache zilizopita usingemjua . Ama pengine sio sasa, lakini kulikuwa na uwezekano kwamba wakati wa karantini uliweza kuwasiliana na rafiki zako kwa sababu yake .
Na hilo linakupatia faida nzuri. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake Eric Yuan , mwanzilishi wa programu mpya ya mawasiliano Zoom , aliorodheshwa katika orodha ya Forbes ya mabilionea akiwa na mali yenye thamani $ 7.8 billion .
Mwana huyo wa muhandisi , Yuan alizaliwa katiika mkoa wa Shandong nchini China. Baada ya kusomea uhandisi chini China , alielekea kufanya kazi nchini Japan kwa miaka minne kabla ya kununua tiketi ya ndege kuelekea Marekani.
Akivutiwa na Bill Gates changamoto yake kuu ni kuwasili katika taifa hilo tajiri zaidi duniani ili kutumia fursa ya uvumbuzi ambayo ilikuwa inazidi kuimarika katika miaka ya 90 katika jimbo la California.
Hawakuwa wakimsubiri kwa kumfungulia milango , hatahivyo. Visa yake ilikataliwa mara nane kabla ya kupata ruhusa kuishi na kufanya kazi nchini humo.
Hivi ndivyo jinsi mwaka 1997 Yuan alifikisha umri wa miaka 27 kuanza maisha mapya katika eneo la Silicon Valley.
Ijapokuwa alizungumza kiingereza kidogo, haikuchukua muda mrefu kwa yeye kupata mahali ambapo angeimarisha ujuzi wake.
Alianza kufanya kazi kama msimamizi wa programu katika kampuni ya Wev Ex. Muongo mmoja baadaye kampuni hiyo ilinunuliwa na Cisco Systems , ambapo Yuan alipanda ngazi na kuwa makamu wa rais wa uhandisi katika kampuni hiyo.
Mwaka 2011, muhandisi huyo aliwasilisha mradi wake wa kuvumbua programu ya mawasiliano ambayo itafanyakazi katika tarakilishi na pakatalishi na pia katika simu.
Wazo hilo lilikataliwa na Yuan akajiuzulu katika kampuni hiyo ili kuanzisha biashara yake: Zoom.

Je alipata vipi wazo hilo?

"Mara ya kwanza nilipofikiria kuhusu Zoom , ni wakati nilipokuwa mwanafunzi wa Chuo kikuu nchini China na nilikua nikipanda treni kila siku kwenda kumuona mchumba wangu ambaye sasa ni mke wangu'', alisema Yuan katika mahojiano na ''chombo cha habari.
'Nilikerwa na safari hizo za mara kwa mara na nikaanza kufikiria njia nyengine za kumtembelea mchumba wangu bila ya kusafiri''.
'Ndoto hizo hatimaye zilitimia na kuwa kampuni ya Zoom Foundation'' ,, alisema mfanyabishara huyo.
Changamoto za kupata wawekezaji
Baada ya kujiuzulu katika kampuni ya Cisco , ilikuwa vigumu kupata wawekezaji ambao waliamini mradi wake.
Tatizo lilikua kwamba biashara hiyo ilikuwa imefanywa na wengi. Na kulikuwa hakuna nafasi ya mshindani mwengine.
Alilazimika kuomba fedha kutoka kwa marafiki na watu wa familia ambao waliamini mradi wake kulingana na gazeti la Financial Times.
''Unapoanza bishara wakati ni muhimu sana'' , aliambia gazeti hilo akielezea kwamba upanuzi wa simu aina ya smartphone na teknolojia ya kuhifadhi ulitoa mazingira ya Zoom kuwanzishwa.
Hata mkewe hakuamini., Yuana aliandia Forbes.
"Nilisema najaua ni ndefu na safari ngumu sana , lakini iwapo sitajaribu , nitajuta.'"
Hivo ndivyo jinsi safari hiyo ya kibiashara ilivyomsaidia kuanzisha ukumbi uliolenga kurahisisha mikutano ya mbali ya kibiashara katika sekta yenye ushindani mkubwa.
Kampuni iliimarika wakati wa virusi vya corona
Kampuni yake ilianza kukua hadi ilipofunguliwa katika soko la hisa mnamo mwezi Aprili mwaka uliopita.
Hadi wakati huo , hisa za Zoom zilikuwa na mojawapo ya ufanisi mkubwa katika orodha ya programu kwa kuweza kudumisha bei ya US $ 62 hata wakati sekta hiyo iliposhuka katika soko la hisa mwezi Septemba.
kampuni hiyo sasa inasema kwamba ina zaidi ya wateja milioni 300
Mwishoni wa mwaka uliopita mambo yalianza kwenda vyema , lakini hali ikabadilika ghafla wakati mlipuko wa virusi vya corona ulipoanza kusambaa kote duniani.
Katikati ya mlipuko huo ,masoko ya kifedha yalishuka huku hisa za Zoom zikipanda hadi asilimia 14 mwaka huu.
Mwezi Disemba kampuni hiyo ilikuwa na wateja milioni 10 kwa siku na ilipofikia mwezi Machi ilikuwa na wateja milioni 200 na kufikia mwezi Aprili wateja waliongeza hadi milioni 300 kulingana na data yake.
Takwimu za masoko zinaonyesha kwamba thamani ya Yuan itaongezeka zaidi ya dola bilioni nne katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na amri ya kutotoka nje ya kukabiliana na virusi vya corona.

'Ni rahisi kutumia'

Ni kwanini ilizishinda kampuni kubwa kama vile Microsoft Skype ama Google Hangouts ?

Wataalam wa teknolojia wanakubaliana kwamba ukubwa wa bidhaa unatokana na sababu ya kwamba bidhaa hiyo ni rahisi kuitumia , na haimuhitaji mtumiaji kujisajili , na hadi watu 100 wanaweza kujiunga katika mawasiliano na kwamba ni bure kwa simu hadi dakika 40.
Lakini kama msumeno unaokata pande zote , uwezo huohuo wa kuitumia ulisababisha kashfa ya kiusalama na faragha.
'Poleni sana'
Baada ya Zoom kuwa chombo kinachotumiwa na watu wa matabaka yoyote badala ya kuwa chombo cha kibiashara kampuni hiyo ilishambuliwa.
Vyombo vya habari viliripoti mashambulizi na kuifanya programu hiyo kuonakana kutokuwa salama.
Vyombo vya habari viliripoti kuhusu wadukuzi ambao waliingia katika mawasiliano hayo ya kanda za video na kuchapisha matusi ama hata kuchapisha kanda za ngono zilizojulikana kama "zoombombing" .
Na ilikuwa wazi kwamba rekodi hizo za mikutano hazikuwa salama kwa kuwa watu wengine wangeweza kuingia na kusikiliza kilichokuwa kikiendelea bila ruhusa.
Yuan alisema kwamba huduma hiyo ilitengenezwa kwa mahitaji ya kampuni na kwamba hakutarajiwa atapata wateja chungu nzima.
Alikiri kwamba hakuangazia masuala ya usalama na faragha wakati wa ubunifu wake .
''Naomba msamaha'' , alisema mfanyabiashara huyo katika taarifa wakati akitangaza kuidhinishwa kwa mikakati kadhaa kutatua suala hilo.
Kile kisichojulikana ni iwapo ufanisi wa zoom katika kiwango cha juu utaruhusu kuongeza idadi ya wateja wake .
Ni mikakati gani itakayowekwa na washindani na ni kiwango gani cha mahitaji ya programu hiyo yatahitajika baada ya mlipuko wa virusi vya corona.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.