Habari za Punde

HOTUBA YA BAJETI YA WAZIRI WA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE, MHESHIMIWA MAHMOUD THABIT KOMBO (MBM) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA, KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 A.UTANGULIZI 

1. Mheshimiwa Spika, naomba nianze hotuba yangu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu na ardhi, kwa kutujaalia afya njema na kuweza kutukutanisha tena katika Baraza lako Tukufu ili tuweze kuzungumza mambo ya msingi ambayo yatachangia katika kuleta maendeleo ya Nchi yetu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuongoze kutekeleza shughuli zetu kwa hekima, busara na uadilifu pamoja na kutujaalia uwezo wa kufanikisha majukumu yetu kwa manufaa ya wananchi wa Zanzibar.

2. Mheshimiwa Spika, kwa idhini yako, naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako Tukufu sasa likae kama Kamati ili ipokee, ijadili na hatimaye ikubali kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

3. Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa ustadi wa hali ya juu anaoutumia katika kuiongoza nchi yetu. Chini ya uongozi wake, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kuitekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015-2020. 

Utekelezaji wa Ilani hiyo umejikita zaidi katika kuwaletea maendeleo makubwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba. Aidha, tumeshuhudia Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 2 kwamba nchi yetu imeendelea kuwa na amani, utulivu na mshikamano mkubwa baina ya wananchi.

4. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, naomba kumpongeza kwa dhati Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, kwa ujasiri anaouonesha wakati wa kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Aidha, napenda kumpongeza kwa jitihada zake za kumsaidia na kumshauri ipasavyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, katika kutekeleza majukumu ya kila siku pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

5. Mheshimiwa Spika, vile vile, napenda kukushukuru wewe binafsi na wasaidizi wako wote wakiwemo Naibu Spika, Wenyeviti wa Baraza, Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Wajumbe wa Baraza, Maofisa na wafanyakazi wote wa Baraza kwa kazi nzuri za kuliendeleza Baraza hili.

6. Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii adhimu kuipongeza Kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ikiongozwa na Mwenyekiti wake shupavu, Mheshimiwa Mwantatu Mbaraka Khamis na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Mussa Foum Mussa na wajumbe wake wote kwa maelekezo, miongozo na ushauri makini wanaotupa wakati wa kutekeleza majukumu na miradi ya Wizara. Mimi binafsi na watendaji wenzangu wote tunafarijika sana kuwa nao pamoja na kushirikiana vizuri katika utekelezaji wa kazi zetu. 

7. Mheshimiwa Spika, kwa udhati kabisa, naomba nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuweka mikakati Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 3 madhubuti ya kupambana na maradhi mabaya ya Homa ya Mapafu kwa kitaalamu inaitwa COVID 19 (Corona) ambayo inaitikisa Dunia nzima kwa sasa. Kwa kweli sote ni Mashahidi na tunajionea kupitia vyombo mbali mbali vya habari jinsi maradhi haya yanavyoangamiza mamia na maelfu ya watu katika Mataifa mengine Duniani.

Niendelee kutoa wito kwa wananchi wote wa Unguja na Pemba kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kufuata maelekezo ya Serikali na Wataalamu wa Afya katika kupambana na maradhi haya. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuondoshee maradhi haya Nchini mwetu na Duniani kwa ujumla, ili shughuli za wananchi za kujitafutia maendeleo ziendelee kama kawaida. Aidha, kwa namna ya pekee, ninatumia fursa hii kuwapa pole sana wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki kutokana na mtihani huu wa maradhi ya Corona, tunamuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema Peponi, Amiin.

8. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale imeundwa na taasisi 14 zifuatazo:-

i. Idara ya Uendeshaji na Utumishi 
ii. Idara ya Mipango, Sera na Utafiti 
iii. Idara ya Utalii 
iv. Idara ya Habari Maelezo 
v. Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale 
vi. Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) 
vii. Shirika la Magazeti ya Serikali (SMS)
viii. Chuo cha Uandishi wa Habari (ZJMMC)
ix. Tume ya Utangazaji Zanzibar 
x. Kampuni ya Usambazaji Maudhui (ZMUX) Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na          Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 4
xi. Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar (ZAGPA)
xii. Kamisheni ya Utalii Zanzibar 
xiii. Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu
xiv. Ofisi Kuu Pemba 9. Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kwa muhutasari kueleza kwa ujumla jinsi Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale ilivyotekeleza malengo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020 katika kipindi cha uongozi wa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kutaja mambo machache kabisa ambayo yatabaki kuwa ni historia katika awamu za uongozi zijazo.

Hii ni kwa sababu huu ni mwaka wa mwisho wa awamu hii ya uongozi na kwa msingi kuwa mimi Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale nakhitimisha pia muda wangu wa uongozi katika Wizara hii. Aidha, kwa vile mara nyingi Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amekuwa akihimiza utekelezaji wa Ilani, maelezo haya machache yatatoa mwanga juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo utekelezaji wake unategemea sana bajeti inayopangwa na kupitishwa na Baraza lako hili tukufu. SEKTA YA HABARI 

10.Mheshimiwa Spika, katika sekta ya habari, mambo kadhaa yametekelezwa ikiwemo kuanzisha gazeti la Kiingereza liitwalo “Zanzibar Mail” ambalo limezinduliwa rasmi tarehe 03/11/2019. Gazeti hili linalotoka wiki mara moja limekusudiwa hasa kuwapasha habari wageni wanaoingia nchini kufahamu habari na matukio yanayotokea hapa kwa kila siku na kufahamu fursa zilizopo katika sekta za Utalii, uwekezaji na maendeleo ya nchi. 

Gazeti kama hili la Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 5 Serikali lilikosekana Zanzibar kwa karibu nusu karne hivi sasa baada ya gazeti la mwisho la Kiingereza kusita katika miaka ya sabini.

11. Mheshimiwa Spika, kuimarishwa kwa kampuni ya Uunganishaji Maudhui Zanzibar (ZMUX) kumewezesha kuwapatia wananchi wengi matangazo ya televisheni kwa njia ya kidijitali kwa kuuza ving’amuzi vya kisasa ambavyo ni nafuu na vyenye ubora mkubwa ambavyo Matangazo yake hupatikana katika maeneo yote ya Unguja na Pemba. 

12. Spika, katika hatua za kuliimarisha Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), mitambo ya analogia ilizimwa rasmi 31/8/2017 na kuanza kutumika mitambo ya digitali. Aidha, studio za kisasa zilizinduliwa rasmi tarehe 9/1/2018 na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

Studio hizo ni bora miongoni mwa studio bora Afrika Mashariki. Kuimarika kwa studio hizo kumeifanya ZBC kuwa na hadhi ya kuangaliwa na kusikilizwa zaidi kuliko chombo chochote cha habari hapa Zanzibar. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Tume ya Utangazaji mwaka 2017/2018 ZBC Redio inasikilizwa na asilimia 59.9 ya wasikilizaji wote wa redio nchini. 

Aidha, kununuliwa kwa vifaa vya LIVE U viwili ambavyo vinawezesha kurusha matangazo ya moja kwa moja kumeongeza ubora wa matangazo ya chombo hicho cha habari. 

13. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia shughuli za upigaji chapa, mafanikio makubwa yamepatikana ambapo jumla ya Mitambo 35 imenunuliwa na Mitambo 13 imetengenezwa. Kati ya Mitambo iliyonunuliwa ni Mtambo wa kuchapisha madaftari pamoja na wa Indigo. 

Mtambo wa kuchapisha madaftari umegharimu jumla ya Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 6 shilingi 617,320,000/= na wa Indigo umegharimu USD 414,975/=.

Mitambo hiyo imeshafika nchini na itafungwa mara baada ya ujenzi wa jengo la kuwekea Mtambo huo kukamilika mwishoni mwa mwezi wa Mei. Faraja kubwa itayopatikana kwa kufungwa Mtambo wa kuchapisha Madaftari ni kuwa Serikali haitaagiza au kununua tena madaftari ya wanafunzi wa skuli za Serikali nje ya Nchi na hatua hii pia itakiwezesha kiwanda kutengeneza faida ndogo itakayosaidia katika kukiwezesha kujiendesha. 

SEKTA YA UTALII

14.Mheshimiwa Spika, ili kuiendeleza Sekta ya Utalii na kuifanya iwe endelevu na kutoa mchango mkubwa zaidi katika Uchumi wa Zanzibar, Wizara imefanya Mapitio ya Sera ya Utalii ya mwaka 2017 na kusimamia utekelezaji wa Sheria na Kanuni zinazohusiana na sekta hii. Sera ya Utalii ya mwaka 2017 na Kanuni za Utalii za mwaka 2018 zimekamilika na kusambazwa kwa wadau ili waitumie kwa ajili ya kuendeleza juhudi za Serikali za kukuza utalii.

Katika hatua nyengine muhimu ya kuimarisha Sekta ya Utalii, Serikali imo katika Mpango wa kutenganisha shughuli za Uhamasishaji na Utangazaji Utalii na shughuli za Usimamizi wa Utalii kwa kuunda taasisi mbili tofauti ambazo zitakuwa zikisimamia shughuli hizo. 

Tayari rasimu mbili zimeshaandaliwa na hivi sasa zipo katika hatua ya kukusanya maoni ya Wadau na hatimae zitafikishwa kwa mjadala katika Baraza lako hili Tukufu. 

15. Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kuhamasisha Sekta Binafsi kuanzisha miradi ya ujenzi wa Hoteli za Kitalii hususan Hoteli za Daraja la Kwanza, Kamisheni ya Utalii kwa kushirikiana na Mamlaka Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 7 ya Uwekezaji ya Zanzibar (ZIPA) zimehamasisha Sekta Binafsi ndani na nje ya nchi kuanzisha miradi ya daraja la juu.

Juhudi hizo zimeanza kuzaa matunda kwa kuanzishwa miradi mikubwa ukiwemo “The Great Vision Adventure” (Uroa), “White Paradise Zanzibar” (Pongwe) na “Zanzi Blue Resort” (Matemwe), “Hot el Verde” na “Madinat Elbahri”.

16. Mheshimiwa Spika, kuimarika kwa ubora wa huduma zinazotolewa katika Sekta ya Utalii pamoja na kuimarisha jitihada za utangazaji kumewezesha kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaokuja Zanzibar mara nne kutoka watalii 133,000 mwaka 2010 hadi watalii 538,264 mwaka 2019.

Lengo lililowekwa katika Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ya watalii 500,000 ifikapo 2020 limevukwa kwa zaidi ya watalii 38,664 kabla ya kufikia 2020. 

17. Mheshimiwa Spika, katika kuihamasisha jamii kushiriki katika utalii wa ndani na kuwawezesha kujiajiri wenyewe kupita Sekta ya Utalii, Idadi ya ajira za moja kwa moja katika Sekta ya Utalii imeongezeka kutoka 11,500 mwaka 2011 hadi kufikia 33,000 mwaka 2019.

Inakadiriwa kuwa ajira zisizokuwa za moja kwa moja zimeongezeka kutoka 46,000 mwaka 2011 hadi kufikia 115,000 mwaka 2019. Kiwango hicho kinafanya jumla ya ajira kufikia 148,000.

18. Mheshimiwa Spika, Wizara imepokea ujio wa ndege kubwa kutoka Russia, ndege kutoka Uganda na ndege kutoka Poland, ndege hizi zinafanya safari za moja kwa moja kutoka nchini mwao na kutua Zanzibar.

Wizara pia iliingia Mkataba na Kampuni ya Touchroad ya China kwa ajili ya kuleta watalii kutoka China ambapo Mipango hiyo imekamilika. Ujio wa ndege hizi utaongeza idadi ya wageni Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 8 wanaotembelea nchini na kuongeza Mapato ya Nchi hasa katika Sekta ya Utalii 

SEKTA YA MAMBO YA KALE

19. Mheshimiwa Spika, Miongoni mwa Miradi mikubwa ambayo Wizara inasimamia kwa sasa ni uendelezaji na Matengenezo ya Makumbusho Beit el Ajaib. Kumbusho hilo hivi sasa linafanyiwa matenegenezo makubwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman, matengenezo hayo yanayotarajiwa kugharimu USD 6,000,000. 

20. Mheshimiwa Spika, katika kuhifadhi taarifa na kumbukumbu za Serikali katika Mfumo wa Kompyuta, taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu imeendeleza kazi za kuhuisha Nyaraka na kuzihifadhi katika Mfumo wa Kidijitali (digitization). Kasi ya kazi ya uhifdhi wa Nyaraka kwa njia ya kompyuta imeongezeka baada ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuingia Mkataba na Serikali ya Oman juu ya kuimarisha taasisi ya Nyaraka kwa kuipatia vifaa vipya na Utaalamu.

Aidha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanikiwa kununa nyumba iliyopo jirani na jengo la Nyaraka kwa lengo la kuimarisha usalama wa nyaraka.

21. Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, sasa naomba uniruhusu kutoa maelezo kuhusu bajeti ya Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka 2020/2021.

Katika maelezo hayo nitatoa uchambuzi wa utekelezaji wa programu tulizoahidi kutekeleza katika mwaka wa fedha 2019/2020. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 9 B. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020

22. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale ilikadiriwa kupata shilingi 19,408,700,000/= kwa ajili ya kutekeleza programu kuu tano na Miradi ya Maendeleo ya Wizara. Kati ya hizo shilingi 14,008,700,000/= kwa kazi za kawaida na shilingi 5,400,000,000/= kwa kazi za Maendeleo.

Aidha, Wizara ilipangiwa kukusanya jumla ya shilingi 5,628,411,000/= zinazokwenda Mfuko Mkuu wa Serikali na shilingi 9,392,000,000/= zinazokusanywa na kutumiwa na Taasisi husika.

23. Mheshimiwa Spika, jumla ya shilingi 9,917,483,943/= zilipatikana kwa kazi za kawaida sawa na asilimia 70.79. 

Aidha, Wizara ilikusanya shilingi 3,762,320,269/= sawa na asilimia 66.85 zilizoingia katika Mfuko Mkuu wa Serikali na shilingi 3,936,583,930/= sawa na asilimia 41.91 ambazo zimekusanywa na kutumiwa na Taasisi za Wizara hadi Machi 2020.

(Tafadhali angalia kiambatisho namba 1A hadi 1C).

C. UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA             2019/2020 

24. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020 Wizara imefanikiwa kutekeleza miradi ifuatayo: - Programu ya kuimarisha na kuendeleza maeneo ya kihistoria 

25. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inachukua jitihada za makusudi za kuimarisha Sekta ya Mambo ya Kale kwa kuitengea fungu maalumu la fedha kwa ajili ya kuyafanyia matengenezo makubwa Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 10 maeneo ya kihistoria yaliyopo nchini.

Kwa moyo wa dhati kabisa, nimshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa maamuzi yake ya kuanzisha sekta hii ya Mambo ya Kale kwani ni kiungo muhimu katika kuongeza idadi ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kupelekea kuongezeka idadi za siku za ukaazi kwa wageni wanapofika nchini. 

26. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi kirefu maeneo ya kihistoria yaliachwa bila ya kuwekewa mkakati maalumu wa kuyaendeleza. Kiujumla Maeneo ya Kihistoria yaliyopo nchini hivi sasa ni 85 ambayo yametangazwa katika Gazeti Rasmi la Serikali. Wizara imejiwekea Mkakati maalumu wa kuyaendeleza maeneo haya ya kihistoria kadri fedha zitakavyopatikana.

27. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020 Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale imetengewa jumla ya shilingi 2,400,000,000/= na hadi kufikia Machi 2020 shilingi 503,000,000/= zimepatikana sawa na asilimia 20.96, kwa ajili ya kuyafanyia matengenezo makubwa maeneo ya kihistoria ya Mwinyi Mkuu kwa awamu ya pili na eneo la kihistoria la Mvuleni yaliyopo Unguja pamoja na eneo la kihistoria la Mkamandume Pujini Pemba kwa awamu ya pili.

28. Mheshimiwa Spika, Kasri ya Mwinyi Mkuu – Dunga, ni Kasri ya mtawala wa kienyeji Zanzibar iliyojengwa na Mwinyi Mkuu Mohammed bin Ahmed kuanzia mwaka 1845 na kukamilika mwaka 1856. Utawala wa Mwinyi Mkuu ambao ndio chimbuko la Mji Mkongwe wa Zanzibar (Shangani) ulihamishia Makao Makuu yake huko Dunga katikati ya Kisiwa cha Unguja baada ya kuanzishwa kwa Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 11 Utawala wa Kisultani uliopora Mamlaka ya Utawala wa Kinyeji hapa Zanzibar.

Kasri ya Mwinyi Mkuu ilipata umaarufu mkubwa kutokana na sifa zake za kipekee kama ukubwa, sanaa yake ya ujenzi na vielelezo vilivyomo kama Mahabusu, Amara, Mahkama na Ofisi ya Utawala.

Ni jengo pekee la Mtawala wa Jadi liliopo katika eneo lote la Kusini mwa Jangwa la Sahara ambalo linaendelea kutumika na lipo imara na katika uhalisia wake.

Kuwepo kwa Kasri hii ni ithibati ya hatua kubwa ya maenedeleo ya Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa iliyofikiwa na Wenyeji wa Visiwa vya Zanzibar kabla ya kuingia kwa tawala za kigeni za Warabu na Wazungu.

29. Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuilinda na kuiendeleza historia katika eneo hilo la Mwinyi Mkuu, ndipo Wizara ikaamua kwa makusudi kulifanyia matengenezo makubwa eneo hili la kihistoria. Matengenezo hayo ya awamu ya pili yanafanywa na Kampuni ya YASIN & SONS COMPANY LTD na yanagharimu shilingi 802,474,304/=. Tayari mjenzi ameshalipwa shilingi 50,610,930/= sawa na asilimia 6.

Mjenzi amekamilisha kujenga ghorofa ya kwanza, kupiga plasta ndani na nje pamoja na kuliezeka jengo hilo. Aidha, mjenzi amesafisha hodhi la asili pamoja na kisima ambavyo vilikuwa vikitumika kwa ajili ya kuhifadhia maji. Hatua ya ujenzi kwa sasa imefikia asimilia 30. 30.Mheshimiwa Spika, nyumba ya Wareno Mvuleni, jengo la Wareno Mvuleni lilijengwa na Watawala wa Kireno katika karne ya 16.

Ni jengo la makaazi ya Maafisa wa Kireno lililojengwa katika eneo la Mji wa Kale wa Fukuchani.

Kujengwa na kuendelea kuwepo kwa majengo haya ni uthibitisho wa kuanzishwa kwa Utawala wa mwanzo wa Wazungu hapa Zanzibar na Afrika Mashariki kwa ujumla. Kumbukumbu za Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 12 makaazi haya ya Wareno pia kunaonesha athari za Maendeleo ya Kibepari wa Kibiashara (mercantilism) kwa Zanzibar kulikopelekea kuimarika kwa biashara ya Utumwa ya Afrika Mashariki, kuanzishwa kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara kama Tumbaku, Mananasi, Mahindi, Mapera, nakadhalika. 

31. Mheshimiwa Spika, mradi wa kuliimarisha eneo la kihistoria la Mvuleni unagharimu shilingi 695,855,383/= na unatekelezwa na kampuni ya ujenzi ya KIN INVESTMENT LTD. Kwa sasa tayari mjenzi amelisafisha eneo lote ndani na nje na amejenga jengo jipya la kutolea huduma (Service Building) na kulipiga plasta.

Aidha, tayari mjenzi ameshafikisha umeme katika eneo hilo ambao utatumika katika kutolea huduma muhimu za eneo hilo la kihistoria.

Vile vile, hatua za kuliimarisha jengo hilo zimeanza. Kwa sasa hatua za ujenzi zimefikia asimilia 25. 32.Mheshimiwa Spika, Kasri ya Mkamandume ni kumbukumbu ya Makaazi ya Mtawala wa Kienyeji aliyekuwa maarufu na mwenye kuheshimika sana katika jamii yake kabla ya uvamizi wa kuanzishwa kwa Utawala wa Wareno Pemba.

Kasri hii ilijengwa na Diwani Abubakar Abdulraman (Mkamandume) mwishoni mwa karne ya 15. Historia inaonesha kasri hii ambayo ilikuwa ya ghorofa ndio jengo lililokuwa kubwa zaidi katika zama zake kuliko majengo yote yaliyokuwepo Kusini mwa Jangwa la Sahara. 

Aidha, kasri hii ya Mtawala wa Kienyeji pia ilisifika kwa kuwa na uzio mkubwa na imara zaidi katika eneo la Mwambao wa Afrika Mashariki.

Ni eneo muhimu sana kihistoria kutokana na kuwa na utajiri mkubwa wa vielelezo vinavyothibitisha Maendeleo na Ustaarabu wa wenyeji Kijami, Kiuchumi na Kisiasa kama vile mabaki ya majengo makubwa, visima, mzimu, mabaki ya kiwanda cha uhunzi, mto wa maji (canal), na kuta kubwa za uzio. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 13

33. Mheshimiwa Spika, mradi wa eneo hili la kihistoria la Mkamandume Pemba kwa awamu ya pili unatekelezwa na Kampuni ya SHAMJO COMPANY LTD, na unagharimu shilingi 878,309,587/=. Tayari mjenzi ameshalipwa shilingi 175,661,917/= sawa na asilimia 20. 

Mjenzi ameanza kujenga jengo jipya la kutolea huduma (Service Building) ambalo litakua likitumika kwa ajili ya kutoa maelezo mafupi ya historia ya eneo la Mkamandume pamoja na kupumzika wageni watakaofika eneo hilo.

Pia, mjenzi ameanza kuyatengeneza maeneo ya kisima cha wivu na mzimu ili kuyakinga na uharibifu wa maji ya mvua. Hatua ya ujenzi kwa awamu hii ya pili imefikia asilimia 30. 

34. Mheshimiwa Spika, napenda kuwajuilisha wajumbe wako kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepata msaada kutoka Serikali ya Oman, kulifanyia Matengenezo makubwa Jumba la Kihistoria ya Beit – Al – Ajaib liliopo Forodhani Mjini Unguja. Mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili kutoka mwaka 2020 hadi mwaka 2022. 

Mradi huu unatekelezwa na Kampuni ya COSTRUZION GENERALI GILARDI kutoka nchini Italy. Mradi huu utahusisha matengenezo ya jengo lote kwa kukarabati wa kuta zote, kurudisha kama awali sehemu ya ubavuni iliyoanguka, kurudishwa kwa “lifti” pamoja na milango na madirisha.

35.  Mheshimiwa Spika, jitihada hizi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya awamu ya saba chini ya uongozi uliotukuka wa Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi za kuyafanyia matengenezo makubwa maeneo ya kihistoria zinakwenda sambamba na dhamira ya dhati ya kukuza utalii wa ndani (Utalii kwa Wote) pamoja na kuongeza vivutio kwa wageni wanaofika Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 14 nchini, kwani kuwepo kwa vivutio hivi kutaongeza idadi ya wageni watakaokuja kutembelea nchini na kukuza mapato ya nchi. 

Programu ya Maendeleo ya Habari, Utangazaji na Uchapaji 

36.  Mheshimiwa Spika, katika programu hii Wizara inatekeleza Mradi wa Ujenzi wa Ofisi na Studio za ZBC Pemba kwa awamu ya pili. Mradi huu unatekelezwa na CHUO CHA MAFUNZO na umepangiwa shilingi 1,500,000,000/=, hadi kufikia Machi 2020 mjenzi ameshalipwa shilingi 344,693,805/= sawa na asilimia 23.

Hatua ya ujenzi kwa awamu hii ya pili imefikia asilimia 35. Kazi zilizokwishafanywa ni kujengwa ghorofa zote tatu za jengo, kupiga plasta ndani na nje ya jengo pamoja na kuweka Milango na Madirisha. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi wa Oktoba 2020. 

Kukamilika kwa jengo hili kutasaidia sana kuondoa tatizo la Ofisi kwa baadhi ya taasisi za Wizara yetu ambapo ghorofa ya tatu ya jengo hili zitakuwepo Ofisi za taasisi hizo. Programu ya Utangazaji na Uhamasishaji wa Utalii

37. Mheshimiwa Spika, programu hii inatekeleza Mradi wa kuimarisha utalii kwa wote ambapo katika mwaka wa fedha 2019/2020 mradi huu umetengewa shilingi 1,500,000,000/=, hadi kufikia Machi 2020 zimepatikana shilingi 1,121,553,418/= sawa na asilimia 74.77.

Mradi huu unatekelezwa kwa awamu ya pili na Kampuni ya QUALITY BUILDING CONTRACTOR ambapo mjenzi tayari amekamilisha ujenzi wa vibanda kwa ajili ya kutolea huduma, vyoo, bustani, ujenzi wa mikahawa na sehemu za maegesho.

Aidha, eneo hilo tayari limeshafikishwa umeme, maji pamoja na kufanywa matengenezo makubwa ya njia kwa kiwango cha fusi. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 15

 D. TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA WIZARA KWA MWAKA              WA FEDHA 2019/2020 

38. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020 Wizara ilipanga kutekeleza programu kuu tano kama ifuatavyo: -

I. Programu ya Maendeleo ya Habari, Utangazaji na Uchapaji. 
II. Programu ya Maendeleo ya Utalii, Makumbusho, Mambo ya Kale na Utunzaji wa                      Nyaraka na Kumbukumbu za Serikali.
III. Programu ya Utangazaji na Uhamasishaji wa Utalii.
IV. Programu ya Kuratibu na Kusimamia Maendeleo ya Utalii.
V. Programu ya Uendeshaji na Mipango katika Sekta ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

I. PROGRAMU YA MAENDELEO YA HABARI, UTANGAZAJI NA UCHAPAJI 

39. Mheshimiwa Spika, lengo kuu la programu hii ni kuwa na jamii iliyoimarika katika Maendeleo ya Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa kupitia habari. Programu hii inaundwa na programu ndogo mbili nazo ni: -

 i. Upatikanaji na Usambazaji wa Habari.
ii. Usimamizi wa vyombo vya Habari, Utangazaji na Uchapaji. Programu Ndogo: Upatikanaji na Usambazaji wa Habari

40. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Upatikanaji na Usambazaji wa Habari inatekelezwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Idara ya Habari Maelezo, Shirika la Magazeti ya Serikali (SMS), Chuo cha Uandishi wa Habari na Kampuni ya Usambazaji Maudhui (ZMUX). Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 16

41. Mheshimiwa Spika, huduma ambazo zinatolewa katika programu hii ndogo ni urushaji wa vipindi kupitia Televisheni na Redio, utoaji wa taarifa, picha, makala, filamu na sinema, uchapishaji wa magazeti, utoaji wa mafunzo ya habari na mawasiliano pamoja na usambazaji wa maudhui ya utangazaji.

UTEKELEZAJI HALISI 

42. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza programu ndogo hii ya Upatikanaji na Usambazaji wa Habari, Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) limefanikiwa kuandaa na kurusha hewani vipindi vya ndani vya ZBC TV 8,721 vikiwemo vya Sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mikutano ya Baraza la Wawakilishi, Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 – 2020 ya CCM, Sala na Baraza la Eid, Unyanyasaji wa kijinsia, Kiswahili lugha yetu, Kutoka jimboni, Zanzibar Wiki hii, ZBC Dokta na Hazina iliyofichika.

Aidha, ZBC TV imerusha hewani jumla ya vipindi 1,282 vya nje vikiwemo Makala na Habari kutoka katika chaneli mbali mbali.

43. Mheshimiwa Spika, Shirika limefanikiwa kurusha vipindi vya ZBC Redio 11,151 vikiwemo vipindi vya Ziara za Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pamoja na Viongozi Wakuu wa Serikali, vipindi vya kuadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mazungumzo ya Asubuhi, Mawio, Badilika, Mswahili na Utamaduni.

Aidha, jumla ya matangazo 13,041 yamerushwa hewani kupitia ZBC Redio na ZBC TV yakiwemo ya matangazo ya vifo, matangazo ya biashara na matangazo maalumu. Pia Shirika la Utangazaji linasimamia redio ya Spice FM ambayo imerusha jumla ya vipindi 540 vikiwemo Sema nao, Dozi nene, Nyumba zetu na Spice watoto.

Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 17 44.Mheshimiwa Spika, Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) linarusha moja kwa moja kipindi cha Kutoka Magazetini kupitia ZBC Redio na ZBC TV

Hapo awali kipindi hicho kilikuwa kikirushwa kupitia ZBC redio pekee, lakini kwa sasa kipindi hicho kinakwenda hewani wakati mmoja kwenye ZBC redio na ZBC TV. Kurushwa moja kwa moja kipindi hicho Kutoka Magazetini kwenye ZBC TV, kumeimarisha ubora wa vipindi vya ZBC TV pamoja na kuwawezesha wananchi wengi kufuatilia kipindi hicho. 

45. Mheshimiwa Spika, Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) limeanzisha ukurasa katika Mtandao wa kijamii wa YouTube ambamo inaweka moja kwa moja taarifa ya habari ya ZBC TV inayosomwa ili kuweza kuwafikia watu wengi ndani na nje ya nchi kwa urahisi zaidi. 

Kuanzishwa kwa mtandao huu kumeongeza idadi ya watazamaji wa ZBC TV duniani. 

46. Mheshimiwa Spika, katika hatua za kutoa habari kwa wananchi kwa wakati, ZBC limeweza kurusha matangazo ya moja kwa moja 196, yakiwemo ya Maadhimisho ya Miaka 
56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mikutano ya Baraza la Wawakilishi, Sala na Baraza la Eid, Misa za Christmas pamoja na Uzinduzi wa Miradi ya Maendeleo ya Kijamii yakiwemo Majengo ya Masoko, Skuli na Barabara Unguja na Pemba.

47.Mheshimiwa Spika, Shirika pia limefanikiwa kuimarisha utendaji kazi kwa kuwapatia wafanyakazi vitendea kazi mbali mbali zikiwemo kamera kumi, video mixer moja, kompyuta 50 vifaa vya kuandikia na Samani za Ofisi. Vitendea kazi hivyo vimesambazwa katika vituo vya ZBC vilivyopo Unguja, Pemba na Dar es Salaam. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 18 

48. Mheshimiwa Spika, katika hatua za kukuza utendaji kazi wa wafanyakazi, ZBC imewapatia mafunzo ya muda mrefu wafanyakazi 12 na mafunzo ya muda mfupi wafanyakazi 12 ndani na nje ya nchi, katika fani za Uandishi, Utayarishaji vipindi, Ufundi, Utangazaji, Usarifu picha, Fedha na Utawala. 

Aidha, wafanyakazi 57 wamepatiwa mafunzo maalumu ya muda mfupi yaliyotayarishwa kwa mashirikiano ya ZBC na wataalamu kutoka China na Korea. Mafunzo hayo yametolewa kwa watayarishaji wa vipindi, Wapiga Picha, Mafundi na Waandishi wa Habari. Shirika pia, limetoa mafunzo ya muda mfupi ya tathmini ya utendaji kazi (Performance Appraisal) kwa wafanyakazi wake wapatao 315 katika vituo vya Dar es Salaam, Pemba na Unguja. 

49. Mheshimiwa Spika, Idara ya Habari Maelezo imefanikiwa kusambaza taarifa 850 zikiwemo zinazohusiana na Ziara za Mabalozi wa SADC, Kongamano la Vijana, Tamasha la sita la Diaspora na uzinduzi wa Miradi mbali mbali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. 

Taarifa hizo zimesambazwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari kama ZBC TV, ZBC Redio, Zanzibar Leo, Chuchu FM, Micheweni FM, Al-Noor FM, Bahari FM, Zenj FM, ZNZ News, Mjengwa Blog, Michuzi Blog, Zanzibar 24, pamoja na Redio za Jamii za Mtegani, Michewani na Tumbatu.

Pia, Idara imeweka kwenye “Display Board” yake iliyopo Kisonge Mjini Unguja taarifa na matukio mbali mbali yanayotokea nchini ili kuwawezesha wananchi walio wengi kujua kwa wakati mambo yanayotokea nchini.

Aidha, Idara imefanikiwa kuonesha sinema katika Shehia na Vijiji 22 ikiwemo Fumba, Kizimkazi Matemwe, Mwambe, Wambaa na Kiuyu juu ya tahadhari ya kujikinga na marardhi ya Kipindupindu na Corona.

50. Mheshimiwa Spika, Idara imeweza kusambaza jumla ya picha za viongozi 656 zikiwemo picha 200 za Mheshimiwa Rais wa Zanzibar Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 19 na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, picha 212 za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, picha 124 Rais Wastaafu na Picha 120 za Baraza la Mawaziri.

51. Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuwawezesha Waandishi wa Habari waliopo nchini kuweza kufanya kazi bila ya vikwazo, Idara imetoa Vitambulisho 350 vya Waandishi wa Habari.

Aidha, Idara imeratibu mikutano 95 ya Taasisi za Umma na Waandishi wa Habari kwa lengo la kutangaza shughuli za Serikali kwa Wananchi. 

Pia, Idara imefanya Mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari na imezungumzia juu ya matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili kwa Wahariri hao pindi wanaporipoti taarifa kwenye vyombo vya habari.

52. Mheshimiwa Spika, Idara imefanikiwa kusajili vijarida vitatu ambavyo ni MAKAMO kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, KASIKI kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) na UNUNUZI WA UMMA kutoka Ofisi ya Mamlaka ya Ununuzi wa Umma. Vile vile, Idara imesajili Gazeti moja liitwalo FUMBA TIMES kutoka Kampuni ya “Custumize Property Solution”.

53. Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuimarisha utendaji kazi kwa wafanyakazi, Idara imefanikiwa kumpatia mfanyakazi mmoja masomo ya muda mrefu ya Shahada ya Pili katika Chuo Kikuu cha Nanjing Normal University nchini China katika fani ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma na wafanyakazi watatu wamepata mafunzo ya muda mfupi.

Aidha wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo wa Unguja na Pemba wamepatiwa mafunzo juu ya Sheria na Kanuni za Utumishi. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 20

54. Mheshimiwa Spika, Shirika la Magazeti ya Serikali (SMS) limefanikiwa kuanzisha gazeti la Kiingereza liitwalo “Zanzibar Mail” ambalo limezinduliwa rasmi tarehe 03/11/2019. Gazeti hili linalotoka wiki mara moja, limekusudiwa kuwapasha habari wananchi na wageni wanaoingia nchini kufahamu habari na matukio yanayotokea hapa kwa kila siku na kufahamu fursa zilizopo katika sekta za utalii, uwekezaji na maendeleo ya nchi.

Pia, Shirika la Magazeti ya Serikali limelirudisha tena gazeti la Zaspoti tarehe 1/12/2019. Gazeti hili linalosheheni habari za Michezo, Burudani na Utamaduni wetu. Magazeti yote hayo huchapishwa wiki mara moja siku ya Jumatatu.

55. Mheshimiwa Spika, Shirika la Magazeti ya Serikali (SMS) limefanikiwa kuchapisha nakala 725,501 za magazeti ya Zanzibar Leo, Zaspoti na Zanzibar Mail na kuyasambaza katika Mikoa yote ya Zanzibar na baadhi ya Mikoa ya Tanzania Bara kwa lengo la kutoa habari, kuelimisha na kuburudisha jamii juu ya masuala mbali mbali ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Pia, Shirika linaendelea kuwafikia wasomaji walio wengi duniani kwa kuweka magazeti yake ukurasa wa YouTube na Twiter na kuongeza idadi ya wasomaji wa magazeti ya Shirika. Aidha, Shirika limefanikiwa kutoa matangazo 821 katika magazeti yake na kuongeza kiwango cha mapato.

56. Mheshimiwa Spika, katika usimamizi wa madeni ya matangazo na mauzo ya magazeti, Shirika la Magazeti kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango wameendelea kusimamia madeni hayo kwa kuhakikisha taasisi zote za Serikali zinalipa kwa wakati kila zinapopatiwa huduma.

Wizara ya Fedha na Mipango imefanikiwa kulipatia Shirika la Magazeti ya Serikali shilingi 200,654,500/= fedha ambazo ni baadhi ya makato kutoka Taasisi mbali mbali za Serikali Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 21 ambazo zinadaiwa na Shirika la magazeti. Fedha hizo zimesaidia sana katika uanzishwaji wa gazeti la Zanzibar Mail pamoja na kulirudisha gazeti la ZaSpoti. 

57. Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuongeza idadi ya wasomaji wa Mjini na Vijijini, Shirika limeongeza idadi ya Mawakala na vituo vya kusambaza Magazeti kwa Unguja, Pemba na Dar es Salaam. Mawakala hao wana jukumu la kuhakikisha Magazeti yanayochapishwa na Shirika la Magazeti Zanzibar yanawafikia wananchi kila siku na kwa wakati.

58. Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuimarisha ubora wa gazeti, Shirika limefanikiwa kuwapa mafunzo ya muda mfupi na mafuzo ya muda mrefu watendaji wake wa kada mbali mbali ili kwenda sambamba na mahitaji ya soko. Shirika pia, limeweza kuwapatia wafanyakazi wake sita stahiki zao zikiwemo posho la likizo na malipo ya muda wa ziada pamoja na kuwalipa waandishi wa kujitegemea.

59. Mheshimiwa Spika, Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma Zanzibar katika mwaka wa masomo 2019/2020 kimeweza kudahili wanafunzi 78 katika fani ya Uandishi wa Habari wakiwemo wanawake 53 na wanaume 25. Aidha, jumla ya wanafunzi 31 wa ngazi ya Cheti na wanafunzi 53 wa ngazi ya Stashahada wamehitimu na kukabidhiwa vyeti ambapo kati ya hao wanawake ni 62 na wanaume 22

60. Mheshimiwa Spika, Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma Zanzibar kimeanzisha Redio ya Chuo inayoitwa Habari FM 94.9. Kuanzishwa kwa redio hii kunatoa fursa kubwa kwa wanafunzi kufanya mazoezi ya vitendo kupitia redio hiyo wakiwa Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 22 Chuoni na wananchi kupata taaluma na burudani kupitia vipindi mbali mbali vinavyorushwa.

Aidha, kuwepo kwa redio hii kumesaidia sana kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi ukilinganisha na wanafaunzi waliokuwepo Chuoni kwa mwaka wa masomo 2019/2020, kwani redio hii pia inatumika katika kutoka matangazo ya mara kwa mara ya kukitangaza Chuo na fani zinazosomeshwa.

61. Mheshimiwa Spika, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la “Internews” chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani, Chuo kimeweza kuwapatiwa mafunzo ya Uandishi wa Habari kwa vitendo juu ya utayarishaji wa vipindi vya Redio kwa Wanafunzi waliopo Chuoni hapo.

Pia, Shirika hilo la Kimataifa la “Internews” limetoa msaada wa vitabu 200 vya Uandishi wa Habari kwa ajili ya Wanafunzi, ambavyo vipo katika Maktaba ya Chuo cha Uandishi wa Habari.

62.Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuendelea na mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi, Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma kimefanikiwa kufanya ziara 18 za kimafunzo kwa wanafunzi waliokuwepo Chuoni katika maeneo mbali mbali, ili kuweza kufanya mazoezi ya vitendo na uandishi wa makala.

63. Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Uunganishaji Maudhui Zanzibar (ZMUX) imeuza jumla ya ving’amuzi 6,533 kwa wananchi wa Unguja na Pemba kati ya ving’amuzi 10,000 vilivyonunuliwa mwaka 2019 kutoka nchini China. Kwa sasa Kampuni inawahudumia wateja 14,485 ambao wanapata huduma za maudhui ya kila siku.

64. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwamba wananchi wanapata Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 23 huduma za maudhui kila siku bila ya kukosa, Kampuni imevipatia vituo vyake vyote saba huduma ya umeme na mafuta. Vituo hivyo ni Raha Leo, Masingini, Muyuni, Nungwi, Bungala, Chake-Chake na Kichunjuu.

65.Mheshimiwa Spika, katika kukuza utendaji kazi kwa wafanyakazi, Kampuni imewalipia mafunzo wafanyakazi watatu, mmoja ni mafunzo ya muda mfupi ya udereva “Advance Grade Two VIP” katika Chuo cha Usafirishaji cha Dar es salaam, wa pili Shahada ya Pili ya Usimamizi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Chuo cha Uhasibu cha Arusha (Institute of Accountancy Arusha, IAA) na wa tatu Shahada ya Pili ya Rasilimali Watu, katika Chuo Kukuu Huria Tanzania.

66.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Programu ndogo hii iliidhinishiwa jumla ya shilingi 7,882,143,680/= kwa kazi za kawaida na hadi kufikia Machi 2020 imefanikiwa kupata shilingi 4,925,604,616/= sawa na asilimia 62.49. Programu imetakiwa kukusanya jumla ya shilingi 2,872,000,000/=, hadi kufikia Machi 2020 jumla ya shilingi 2,163,182,682/= zimekusanywa sawa na asilimia 75.32 (Tafadhali angalia kiambatisho namba 1D na 1E). Programu Ndogo: Usimamizi wa Vyombo vya Habari, Utangazaji na Uchapaji

67. Mheshimiwa Spika, Programu ndogo ya Usimamizi wa Vyombo vya Habari, Utangazaji na Uchapaji inatekelezwa na Idara ya Habari Maelezo, Tume ya Utangazaji na Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 24

68. Mheshimiwa Spika, huduma zinazotolewa katika programu ndogo hii ni udhibiti na usimamizi wa shughuli za habari na utangazaji kupitia Sera na Sheria za Habari na Utangazaji. Shughuli nyengine ni kusimamia shughuli za upigaji chapa kwa Taasisi za Serikali na kutoa huduma za Bohari Kuu ya vifaa vya Ofisi na kuandikia. UTEKELEZAJI HALISI

69. Mheshimiwa Spika, Idara ya Habari Maelezo imefanikiwa kutoa vibali kwa vyombo vya habari 11 vikiwemo DEEMAX TV, BBC East Africa, SEEN Films, TBS News, Arusha Freight Transaprency na Kampuni ya Alfatah Online TV vya kuchukua picha na filamu katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

70. Mheshimiwa Spika, Tume ya Utangazaji Zanzibar imetoa Leseni za Utangazaji sita kwa vyombo mbali mbali vya habari vikiwemo, Mambo Swahili TV na TV za mitandaoni za Pemba Today na SN TV Online.

Aidha, Tume imefanikiwa kufuatilia na kurekodi matangazo ya vituo 23 vya redio za FM na vituo viwili vya redio jamii vya coconut FM, Zenj FM, Spice FM, Alnour FM, Redio Jamii Tumbatu na Redio Jamii Mtegani.

71.Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha maadili ya utangazaji hayakiukwi, Tume ya Utangazaji imeandaa Kanuni za Utoaji Leseni za Utangazaji ambapo kwa sasa Kanuni hizo zipo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kupitiwa. Pia, Tume imeandaa Muongozo wa Kuripoti Habari za Uchaguzi, Muongozo huo tayari umekamilika kwa ajili ya matumizi. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 25 72.Mheshimiwa Spika, Tume imefanikiwa kumpata Mshauri elekezi wa kuandaa na kufunga Mfumo wa Ufuatiliaji Maudhui ya Mitandaoni. Tume tayari imeshatiliana saini na Mshauri Elekezi, Mkataba kwa ajili ya kufunga Mfumo huo. Kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa Mei. Kufungwa kwa mfumo huu kutawezesha kufuatilia kwa karibu habari na matukio yote yanayotokezea katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kudhibiti upotoshwaji wa habari katika mitandao ya kijamii. Aidha, Tume imeanzisha tovuti yake kwa lengo la kutoa taarifa zinazohusu tasnia ya Utangazaji nchini. Tovuti hiyo inajulikana kwa jina la www.tuz.go.tz. 73.Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuimarisha utendaji kazi kwa wafanyakazi, Tume ya Utangazaji imewagharamia masomo wafanyakazi wawili, mmoja ngazi ya masomo ya Shahada ya Pili katika fani ya Uchumi na mmoja mafunzo mafupi katika fani ya Uhasibu. Pia, Tume imelipa haki na stahiki za likizo na muda wa ziada kwa wafanyakazi wake. 74.Mheshimiwa Spika, Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar umefanikiwa kununua mitambo mikubwa miwili mipya ya kisasa nchini China kwa ajili ya kuchapisha Mabuku ya Wanafunzi wa Skuli za Serikali za Unguja na Pemba. Mitambo hiyo tayari ishafika nchini tangu mwezi wa Februari 2020. Aidha, ujenzi wa jengo la Wakala la ghorofa mbili ambalo litatumika kwa ajili ya kuifunga Mitambo hiyo unaendelea. Jengo hilo linategemewa kukamilika mwezi wa Mei na hatua za uchapaji wa Mabuku zinategemewa kuanza mara baada ya kufungwa Mitambo na wataalamu kutoka nchini China. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 26 75.Mheshimiwa Spika, katika hatua za kukiongezea Mtaji Kiwanda hiki ili kiweze kijiendesha wenyewe, tayari Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshatoa idhini kwa Wakala kupatiwa mkopo kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ya shilingi 6,000,000,000/= kwa ajili ya kununua vifaa vya kuandikia kutoka nje ya nchi na kuviuza kwa taasisi zote za Serikali. Hivyo, ninapenda kuzisisitiza taasisi za Serikali kufanya manunuzi ya vifaa vyote vya kuandikia (Stationaries) kwa Wakala ili kuweza kukuza Mapato ya Nchi yetu. 76. Mheshimiwa Spika, Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar umechapisha nyaraka na taarifa zote za Serikali zikiwemo Miswada ya Sheria iliyowasilishwa katika Vikao vya Baraza la Wawakilishi, Sheria, Magazeti Rasmi, Vitabu vya Bajeti kwa Wizara zote, uchapishaji wa Gazeti la kila siku la Zanzibar Leo, Zanzibar Mail na Zaspoti. Kuchapishwa kwa Nyaraka hizi muhimu katika kiwanda cha Serikali kunasaidia sana kukipa hadhi kiwanda pamoja na kudhibiti siri za Serikali kutoka nje ya taasisi za Serikali. Wakala umechapisha baadhi ya kazi za taasisi za watu binafsi, kazi ambazo hufanyika katika hali ya ubora na viwango vinavyohitajika kwa wateja wake. Vile vile, Wakala umeendelea na shughuli zake za kila siku za kuchapisha kazi mbali mbali na baadae kuziuza kwa Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi kwa lengo la kuongeza Mapato. 77.Mheshimiwa Spika, Wakala umezifanyia Matengenezo Makubwa baadhi ya mashine ili ziweze kufanya kazi kwa kiwango cha hali ya juu. Miongoni mwa mashine zilizofanyiwa kazi ni pamoja na mashine ya CTP Codac, Cannon, Accurio, Automatic Closing machine, Duplo Perfect Binding, Morgana, System Binder, Roseback, Web offset, Four Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 27 colour, Horizon Folding Machine na VDP. kufanyiwa matengenezo kwa mashine hizo kumeongeza ubora wa kazi zinazozalishwa na Wakala pamoja na kuongeza idadi ya Wateja wanaohudumiwa na Wakala na kuhimili ushindani. Aidha, Wakala umegharimia upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya kufanya kazi za machapisho ya aina mbali mbali yanayowasilishwa hapo Kiwandani. 78.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020, programu ndogo hii iliidhinishiwa jumla ya shilingi 1,019,000,000/= kwa kazi za kawaida na hadi kufikia Machi 2020 imefanikiwa kupata shilingi 834,757,339/= sawa na asilimia 82.41. Programu hii imetakiwa kukusanya jumla ya shilingi 6,950,261,000/=, hadi kufikia Machi 2020, jumla ya shilingi 2,888,639,021/= zimekusanywa sawa na asilimia 41.56 (Tafadhali angalia kiambatisho namba 1D na 1E). II. PROGRAMU YA MAENDELEO YA UTALII, MAKUMBUSHO, MAMBO YA KALE NA UTUNZAJI WA NYARAKA NA KUMBUKUMBU 79.Mheshimiwa Spika, programu hii ina jukumu la kuhakikisha kuwa maeneo ya kihistoria na Mambo ya Kale yanaendelezwa kwa kuhifadhiwa, kulindwa na kutangazwa, kuwepo kwa usimamizi bora wa kumbukumbu kwa ajili ya matumizi na mawasiliano ya Taifa pamoja na kuratibu na kuendeleza shughuli za utalii. Programu hii imeundwa na programu ndogo tatu ambazo ni: - i. Uendelezaji wa Makumbusho na Urithi wa Mambo ya Kale, ii. Uhifadhi wa Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa. iii. Kuratibu na Kuendeleza Utalii. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 28 Programu Ndogo: Uendelezaji wa Makumbusho na Urithi wa Mambo ya Kale 80.Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Uendelezaji wa Makumbusho na Urithi wa Mambo ya Kale inatekelezwa na Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale. 81.Mheshimiwa Spika, huduma zinazotolewa na programu hii ni Uhifadhi na Uendelezaji wa Makumbusho, Maeneo ya Kihistoria na Mambo ya Kale. UTEKELEZAJI HALISI 82.Mheshimiwa Spika, Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale imelifungua tena rasmi kumbusho la kihistoria la Bi Khole liliopo Bungi, Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kukamilika Matengenezo Makubwa yaliyofanywa na kulirudisha eneo hilo la kihistoria kwenye uasili wake. Kwa sasa eneo hilo linatembelewa na Wageni wa ndani na nje ya nchi na kusaidia kuongezeka kwa idadi ya vivutio vya watalii na kukuza Mapato ya Nchi. 83.Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuyahifadhi na kuyalinda maeneo ya kihistoria, Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale imefanikiwa kufunga Boya katika Mji wa Kale uliozama wa Mkumbuu uliopo Pemba. Kwa mujibu wa wanahistoria ni kwamba katika Mji huu ulikuwa wakiishi watu kama kawaida mwanzoni mwa karne ya kwanza, kabla ya kuongezeka kina cha maji ya bahari na kusababisha mji huu kuzama. Wataalamu wa kuzamia kutoka Shirika la Bandari na Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM) waliyolifunga Boya hilo, wamesema walizamia katika kina cha mita 18 ndipo wakakuta Mabaki ya Mji huo Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 29 kama Kuta, Magae na Kisima, ndipo wakafanikiwa kulifunga Boya hilo. Kufungwa kwa Boya katika eneo hilo kutapelekea kulitangaza eneo hilo na kuongeza idadi ya Wageni watakaotembelea kisiwa cha Pemba kwa kujionea maeneo ya kihistoria. 84.Mheshimiwa Spika, Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale imefanya utafiti mkubwa wa Akiolojia katika maeneo mapya ya Kaskazini Unguja. Maeneo haya yanajumuisha Shehia za Mangapwani, Mafufuni, Makoba, Kiongwe Kidogo, Kidanzini, Muanda na Misufini. Katika utafiti huo, mapango manne yaligunduliwa nayo ni pango la Nawawi, pango la Umundi, pango la Mwenge na pango la Mapopo. Vile vile Idara ilifanya tafiti ndogo katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kusini Unguja kama; Muungoni, Unguja Ukuu, Fumba, Uzi na Pete. 85.Mheshimiwa Spika, katika hatua za kujitangaza na kuwahamasisha wananchi kuyatembelea maeneo ya kihistoria na mambo ya kale, Idara iliweza kuandaa na kushiriki katika maonesho mbali mbali yakiwemo maonesho ya Chakula Kizimbani, maonesho ya Chamanangwe na Maonesho ya Biashara ya kuadhimisha sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar. Pia, Idara ilishirikiana na Wizara ya Utalii na Mali Asili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuandaa Tamasha la Urithi (Urithi Festival) sambamba na kushiriki katika Maonesho ya Utalii (Tourism Show). Idara ilifanikiwa kurusha hewani jumla ya vipindi 29 vikiwemo vipindi vya TV na Redio kupitia ZBC TV vipindi vinane, Zanzibar Cable “ZCTV” vipindi sita, KTV Online vipindi saba, Al-Salaam Island TV kipindi kimoja, Swahiba Radio kipindi kimoja, Mwenge FM vipindi vitano na Hits FM kipindi kimoja. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 30 86.Mheshimiwa Spika, Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale ilipokea jumla ya Wageni 35,391 waliotembelea maeneo ya kihistoria ndani ya visiwa vyetu vya Unguja na Pemba. Kati ya Wageni hao Wenyeji ni 4,083 na Wageni kutoka Mataifa ya nje 9,220. Pia Wageni Maalumu walikuwa ni 268 na idadi ya Wanafunzi ni 21,820. 87.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Programu ndogo hii iliidhinishiwa jumla ya shilingi 3,331,348,980/= kwa kazi za kawaida na hadi kufikia Machi 2020 imefanikiwa kupata shilingi 1,186,445,961/= sawa na asilimia 35.61. Programu imetakiwa kukusanya jumla ya shilingi 270,003,000/=, hadi kufikia Machi 2020, jumla ya shilingi 123,247,371/= zimekusanywa sawa na asilimia 45.65. (Tafadhali angalia kiambatisho namba 1D na 1E). Programu Ndogo: Uhifadhi wa Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa 88.Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Uhifadhi wa Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa inatekelezwa na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu. 89.Mheshimiwa Spika, huduma zinazotolewa na programu ndogo hii ni Kuhifadhi na Kusimamia Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa kwa Serikali na matumizi ya Umma. UTEKELEZAJI HALISI 90.Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu imefanya ukaguzi wa kumbukumbu katika Wizara sita za Unguja na Pemba Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 31 na kutoa ushauri wa uhifadhi na utunzaji bora wa kumbukumbu na kupunguza mrundikano wa Majalada ili kudhibiti upotevu wa Majalada hayo. Aidha, Taasisi ipo katika hatua za kukamilisha kanuni za usimamizi wa Nyaraka, kanuni ambazo zitatoa muongozo juu ya matumizi sahihi ya Taasisi hiyo kwa Wageni na Wenyeji. 91.Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuimarisha Mfumo wa Uhifadhi wa Majalada katika njia za kielektroniki, jumla ya Majalada 16,129 yamehifadhiwa. Aidha, huduma za Utafiti zimetolewa kwa Watafiti 116 wakiwemo Wageni 12 na Wenyeji 86. Vile vile, jumla ya Wanafunzi 18 wa Vyuo mbali mbali walifika Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu na kupatiwa elimu ya vitendo. 92.Mheshimiwa Spika, katika muendelezo wa kukuza utoaji huduma kwa taasisi za Serikali na wananchi kwa ujumla, Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu imewapa mafunzo ya muda mrefu Wafanyakazi wawili na mafunzo ya muda mfupi wafanyakazi sita. Aidh, Taasisi ya Nyaraka imelipa haki na stahiki za muda wa ziada na likizo kwa wafanyakazi wake ili kuimarisha utendaji wa kazi. 93. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Programu ndogo hii iliidhinishiwa jumla ya shilingi 569,171,960/= kwa kazi za kawaida na hadi kufikia Machi 2020 imefanikiwa kupata shilingi 412,902,291/= sawa na asilimia 72.54. (Tafadhali angalia kiambatisho namba 1D). Programu Ndogo: Kuratibu na Kuendeleza Utalii 94.Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Kuratibu na Kuendeleza Utalii inatekelezwa na Idara ya Utalii. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 32 95.Mheshimiwa Spika, huduma zinazotolewa na programu ndogo hii ni Kuratibu na Kuendeleza Shughuli za Utalii nchini. UTEKELEZAJI HALISI 96.Mheshimiwa Spika, Idara ya Utalii imekutana na Kamati za Utalii za Wilaya zote za Unguja na Pemba kwa lengo la kutoa elimu juu ya dhana ya Utalii kwa Wote, Idara imewasisitiza Wajumbe wa Kamati hizo kuchukua jitihada za hali ya juu kutangaza vivutio vya utalii vilivyomo kwenye Wilaya zao. 97.Mheshimiwa Spika, Idara ya Utalii kwa kushirikiana na Kamisheni ya Utalii wameandaa mbio za Marathoni ambazo zimewashirikisha wageni na wanamichezo 400 kutoka mataifa mbali mbali. Mbio hizo zimefanyika katika masafa na umbali tofauti. Kufanyika kwa mbio hizo kunaongeza idadi ya shughuli za kitalii zinazofanyika nchini na kuweza kuwavutia wageni wengi kutembelea nchini. 98.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Programu ndogo hii iliidhinishiwa jumla ya shilingi 171,344,140/= kwa kazi za kawaida na hadi kufikia Machi 2020 imefanikiwa kupata shilingi 72,385,386/= sawa na asilimia 42.25.(Tafadhali angalia kiambatisho namba 1D). III. PROGRAMU YA UTANGAZAJI NA UHAMASISHAJI WA UTALII 99.Mheshimiwa Spika, lengo kuu la programu hii ni kuongeza uelewa kwa wakazi wa Tanzania na jamii ya kimataifa kuhusu bidhaa na huduma za utalii zilizopo Zanzibar. Programu hii inatekelezwa na Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 33 Idara ya Masoko ambayo kwa mujibu wa muundo wa Kamisheni ya Utalii, ndio yenye jukumu la Kuandaa Mikakati ya Utangazaji Utalii ndani na nje ya nchi. 100. Mheshimiwa Spika, huduma inayotolewa ni kuitangaza Zanzibar kiutalii ndani na nje ya nchi ili Zanzibar itambulike zaidi kuwa ni kituo bora cha utalii duniani. UTEKELEZAJI HALISI 101. Mheshimiwa Spika, Kamisheni ya Utalii imeendelea kuhamasisha utalii wa ndani kwa kushirikiana na wadau wa utalii. Mbinu mbali mbali zimetumika kufikisha taarifa za utalii kwa wananchi ikiwemo kushiriki katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba saba) - Dar es Salaam, Maonesho ya Kilimo Nanenane – Kizimbani na Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani – Chamanangwe Pemba. Maonesho mengine ni ya SADC- Dar- es- salaam, Maonesho ya Biashara yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tamasha la Sauti ya Busara, Tamasha la Urithi wa Mtanzania – Zanzibar, Tamasha la ZIFF na Tamasha la Vyakula vya asili Makunduchi na Muungoni. 102. Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuutangaza utalii nchini, Kamisheni ya Utalii imeandaa Maonesho ya Utalii ya Pili ya Zanzibar (2nd Zanzibar Tourism Show) yaliyofanyika katika Hoteli ya Verde – Mtoni na Bonanza la Utalii la Pemba (3rd Pemba Tourisport). Kufanyika kwa Matamasha haya kumeongeza hamasa kwa jamii ya kufanya matembezi katika vivutio vya utalii. Vile vile, kupitia maonesho haya Mawakala wa utalii na wafanya biashara wa utalii wapato 600 wa ndani na nje ya nchi walipata fursa ya kufahamu bidhaa za utalii za Zanzibar na wengi wao wameahidi kuleta wageni wao. Matukio haya yalipata Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 34 fursa ya kurushwa hewani kupitia vyombo mbali mbali vya Redio na Televisheni kama vile ZBC, Azam TV, ZCTV na TBC. 103. Mheshimiwa Spika, Kamisheni ya Utalii imeandaa mashindano ya wazi kwa wanafunzi wa skuli mbali mbali na wanajamii. Lengo la mashindano hayo ni kupima uelewa na ufahamu wa wananchi kuhusu sekta ya utalii Zanzibar. Maswali mbali mbali yaliulizwa na Wanafunzi 45 waliofanikiwa kujibu vizuri walipatiwa zawadi za papo kwa papo na wengine 30 waliandaliwa ziara pamoja na wazee wao katika maeneo ya vivutio vya utalii, ikiwemo Zanzibar Park, Mashamba ya Viungo, eneo la kihistoria la Mangapwani na kwenye Fukwe za Utalii. Vile vile, Kamisheni ya Utalii imeendelea kushajiisha utalii kupitia vyombo vya habari vya Redio na Televisheni, ambapo jumla ya vipindi 87 vimerushwa kati ya hivyo, vipindi 30 ZBC redio, vipindi vinne ZBC TV, vipindi kumi ZCTV, kipindi kimoja TIFU TV, vipindi 27 Chuchu FM), vipindi viwili Times FM, vipindi tisa Bomba FM na vipindi vinne Sauti ya jamii Chokocho. 104. Mheshimiwa Spika, katika kuitangaza Zanzibar kiutalii ndani na nje ya nchi, Kamisheni ya Utalii kwa kushirikiana na sekta binafsi imeshiriki katika maonesha ya “International Mediterranean Tourism Market (IMTM) nchini Israel ambapo kutokana na ushiriki huu zipo kampuni za Utalii za Zanzibar ambazo zimeshaingia mikataba ya kibiashara na Kampuni za utalii za Israel kwa ajili ya kuleta wageni. Aidha, Kamisheni ya Utalii imeratibu safari ya Waandishi wa Habari watatu kutoka Kampuni ya Haedam Media ya Korea ya Kusini na watatu kutoka kampuni ya IPP Media ya Tanzania. Waandishi hawa watatengeneza filamu kwa ajili ya kuvitangaza vivutio vya utalii vya Zanzibar nchini mwao kupitia televisheni ya KBS (Korean Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 35 Broadcasting Services) na Televisheni ya ITV. Vile vile, Kamisheni ya Utalii imeandaa ziara ya Mpishi maarufu kutoka India ambaye alipata fursa ya kutembelea maeneo mbali ya utalii ya Zanzibar na baadae kutengeneza Vipindi vya Utalii vya Mapishi katika Chanali yake. Kupitia waandishi na watu maarufu hawa, Zanzibar itapata fursa ya kutangazwa nchini Korea, India na duniani kote kupitia vyombo vyao vya habari. 105. Mheshimiwa Spika, Kamisheni ya Utalii imeendelea kuandaa na kuchapisha Vielelezo mbali mbali vya kutangaza Utalii na kuvisambaza katika Masoko ya Utalii ambapo Ofisi za Mabalozi wa Tanzania na Watu mbali mbali waliosafiri nje ya nchi wamesaidia sana kusambaza Vielelezo hivyo. Kamisheni ya Utalii imeandaa video za muda mfupi na muda mrefu kwa ajili ya kutangaza vivutio na huduma za Utalii za Zanzibar. Video hizi zitaoneshwa katika mashirika ya ndege ya ndani na nje ya Tanzania ili watu wengi zaidi wapate fursa ya kufahamu bidhaa na huduma za Utalii za Zanzibar. 106. Mheshimiwa Spika, mkazo mkubwa uliwekwa katika kutangaza Utalii kwa njia za kisasa za Kielektroniki ambapo tovuti ya Utalii ya Zanzibar iliimarishwa kwa kuwekwa taarifa sahihi za Utalii kwa wakati jambo ambalo limesaidia sana kutoa taarifa zinazohusu Utalii kwa wageni. Kwa kipindi cha Julai 2019 hadi April 2020 tovuti hiyo tayari imeshatembelewa na watu 632,000 kutoka Mataifa mbali mbali ikiwemo Uingereza, Ujerumani, Itali na Ufaransa. Kupitia programu mpya ya “Virtual Tour” iliyoongezwa katika tovuti hiyo, bidhaa za utalii zinazoonekana moja kwa moja duniani kote. 107. Mheshimiwa Spika, Kamisheni ya Utalii kwa kushirikiana na Kampuni ya Wazalendo imeandaa programu maalumu ya kidigitali Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 36 ya kutangaza utalii ambayo inapatikana kwa lugha tofauti ikiwemo Kiegereza, Kiswahili, Kirusi na Kijerumani. Vituo maalumu vyenye mifumo ya kisasa (digital kiosk) vitajengwa na vitawekwa kwenye mahoteli na maeneo mengine ya utalii ili kuwezesha wageni kununua huduma za utalii wanapokuwa nchini. Aidha, wananchi waliopo katika maeneo ya vijijini watapata taarifa za utalii kwa wakati na hivyo kuwezesha kufanya utalii wa ndani. 108. Mheshimiwa Spika, Kamisheni ya Utalii imeiwezesha Ofisi ya Utangazaji Utalii iliyopo nchini India kufanya kazi za utangazaji kikamilifu kwa kuipatia vielelezo vya utangazaji na kulipia gharama za uendeshaji. Kupitia Wakala huyo, vivutio vya utalii vya Zanzibar vimetangazwa ipasavyo katika soko la India. Wizara imeandaa programu maalumu, 5KPlus, yenye lengo la kuleta angalau watalii 5000 kwa mwaka kutoka nchini India. Utekelezaji wa programu hii utaanza mara tu sekta ya utalii itakaporudi katika hali yake ya kawaida. Vile vile, Wizara imeingia Mkataba na Kampuni ya Touchroad ya China kwa lengo la kuitangaza Zanzibar nchini China na kuleta wageni wapatao 7000 kila mwaka. Utekelezaji wa Mkataba huo ulianza mwezi wa Septemba 2019 na awamu ya kwanza ya kuleta wageni ilikuwa mwezi Februari 2020. Hata hivyo, safari hiyo haikuwezekana kutokana na janga la maradhi ya Korona lililoanza nchini humo. 109. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020 programu hii iliidhinishiwa jumla ya shilingi 573,145,000/= kwa kazi za kawaida na hadi kufikia Machi 2020 imefanikiwa kupata shilingi 292,303,950/= sawa na asilimia 51. (Tafadhali angalia kiambatisho namba 1D). Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 37 IV. PROGRAMU YA KURATIBU NA KUSIMAMIA MAENDELEO YA UTALII 110. Mheshimiwa Spika, lengo kuu la programu ni kuwa na mazingira na rasilimali watu bora katika uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa sera na mipango ya utalii. Programu inatekelezwa na Kamisheni ya Utalii kupitia Idara ya Mipango na Sera, yenye jukumu la kuratibu na kuendeleza utalii pamoja na kujenga uwezo na mazingira mazuri kwa wafanyakazi. UTEKELEZAJI HALISI 111. Mheshimiwa Spika, Kamisheni ya Utalii imeendelea kufanya ukaguzi wa Miradi ya biashara za utalii ili kubaini wanaofanya biashara kinyume cha Sheria ya Utalii, kazi ambayo imefanyika katika Mikoa yote ya Zanzibar. Aidha, kazi hiyo pia imetekelezwa kwenye Vivutio vya Utalii kama vile Jozani na Mashamba ya Viungo - Kizimbani. Katika ukaguzi huo, Miradi ya Utalii 580 imekaguliwa na 20 imebainika kuendesha biashara ya utalii bila ya leseni au vibali husika na kutakiwa kulipia ada ya leseni/ada na faini au kupewa maelekezo kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utalii. Jumla ya shilingi 7,500,000/= zilikusanywa ikiwa ni malipo ya faini kwa waliopatikana na makosa. 112. Mheshimiwa Spika, Kamisheni ya Utalii imeendelea kuwahamasisha Wazanzibari kuwekeza katika sekta ya utalii ikiwa ni utekelezaji wa dhana ya Utalii kwa Wote. Kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Machi 2020 jumla ya Miradi ya Wazalendo 100 imeanzishwa ikiwemo Nyumba za Kulaza Wageni, Kampuni za Kuandaa Misafara ya Watalii, Mikahawa na Kampuni za Michezo ya Baharini. Miradi hii imetoa ajira za moja kwa moja zipatazo 980. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 38 113. Mheshimiwa Spika, Kamisheni ya Utalii imeendesha mafunzo ya utalii kwa wajasiriamali 200 kutoka Wilaya zote za Pemba. Lengo la mafunzo hayo ni kuwapa uelewa wananchi juu ya faida na changamoto za utalii pamoja na bidhaa za utalii za Zanzibar (tourism products/ service). Vile vile, Kamisheni ya Utalii kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) imetoa mafunzo kwa waongozaji watalii (tour guides) 200 ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar za kuwakinga watoto kutokana mambo ya udhalilishaji hasa kwa watalii wanaoingia nchini. 114. Mheshimiwa Spika, Kamisheni ya Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango imekamilisha Mpango Jumuishi wa Utalii (Intergared Strategic Action Plan) ambao umeanza kutekelezwa kuanzia mwezi wa Julai mwaka 2019. Kamisheni ya Utalii inaendelea kutayarisha Mpango wa Utalii kwa wote ambao utaonesha kwa kina muunganiko wa Sekta ya Utalii na sekta nyengine za Kiuchumi na Kijamii. Kukamilika na kutekelezwa kwa Mpango huo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuwa na Utalii uliopangika na usio na Madhara kwa Jamii, Mazingira na Sekta nyengine za Kiuchumi. 115. Mheshimiwa Spika, Kamisheni ya Utalii imeendelea kutoa ushauri kwa wadau mbali mbali wa utalii wa ndani na nje ya nchi kwa lengo kuufanya utalii wetu kuwa wa kisasa, wenye kuhimili ushindani na wenye tija kwa wananchi. Hadi sasa zaidi ya wananchi 420 wameshapatiwa ushauri kuhusu uwekezaji na namna bora ya kuendesha biashara ya utalii. 116. Mheshimiwa Spika, katika kuongeza ufanisi katika kazi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na wadau wa Utalii, Kamisheni ya Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 39 Utalii imewasomesha wafanyakazi watatu katika Vyuo vya ndani na nje ya nchi katika fani za Utalii, Rasilimali Watu, na Usimamizi wa Miradi. Vile vile, jumla ya wafanyakazi wapya watano wameajiriwa kwa lengo la kuongeza kasi ya Maendeleo ya Utalii hususan katika kisiwa cha Pemba. 117. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha upatikanaji wa taarifa za kutosha za Watalii wanapoingia nchini, Kamisheni ya Utalii inaendelea kufanya utafiti wa Utokaji wa Watalii (Tourism Exit Survey 2019) ili kufahamu baadhi ya viashiria muhimu vya upimaji wa ukuaji wa Sekta ya Utalii ikiwemo matumizi ya Mtalii kwa siku pamoja na siku zao za ukazi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa matumizi ya mgeni kwa siku yamefikia dola za kimarekani 263 mwaka 2019 kutoka dola za kimarekani 177 mwaka 2018. 118. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020 programu hii iliidhinishiwa jumla ya shilingi 3,048,855,000/= kwa kazi za kawaida pamoja na kazi za maendeleo, hadi kufikia Machi 2020 imefanikiwa kupata shilingi 2,245,067,628/= sawa na asilimia 73.64. Programu imetakiwa kukusanya jumla ya shilingi 4,876,099,000/=, hadi kufikia Machi 2020, jumla ya shilingi 3,481,989,133/= zimekusanywa sawa na asilimia 71.41. V. PROGRAMU YA UENDESHAJI NA MIPANGO KATIKA SEKTA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE 119. Mheshimiwa Spika, programu hii ina jukumu la kusimamia na kuratibu mipango mikuu, sera na tafiti pamoja na usimamizi na uendeshaji mzuri wa rasilimali watu katika Wizara. Programu hii imeundwa na programu ndogo tatu ambazo ni: Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 40 i. Utawala na Uendeshaji katika Sekta za Habari, Utalii, na Mambo ya Kale ii. Kuratibu na Kusimamia Mipango Mikuu ya Wizara iii. Kuratibu na Kusimamia Utawala, Uendeshaji na Mipango ya Ofisi Kuu Pemba Programu Ndogo: Utawala na Uendeshaji katika Sekta ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale 120. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Utawala na Uendeshaji katika Sekta za Habari, Utalii na Mambo ya Kale inatekelezwa na Idara ya Uendeshaji na Utumishi. 121. Mheshimiwa Spika, huduma zinazotolewa katika programu ndogo ni kujenga uwezo na mazingira mazuri ya kazi kwa wafanyakazi, utayarishaji wa ripoti za fedha na ukaguzi pamoja na mpango wa manunuzi. UTEKELEZAJI HALISI 122. Mheshimiwa Spika, Idara ya Uendeshaji na Utumishi imefanikiwa kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa wafanyakazi 28, waliopatiwa mafunzo hayo katika fani na kada tofauti. Pia, wafanyakazi 178 wamepatiwa mafunzo ya ndani kuhusiana na Sheria ya Manunuzi pamoja na Usimamizi wa Mpango wa Manunuzi na Ugavi na Uandaaji wa Mpango wa Mahitaji ya Mafunzo kwa Wizara. Aidha, Wizara imefanya tathmini ya utekelezaji na mapitio ya Mkataba wa Huduma kwa Umma kupitia vikao na Washirika mbalimbali (Tafadhali angalia kiambatisho nambari 2). Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 41 123. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kufanya mikutano kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa taasisi zake zote za Unguja na Pemba juu ya kuwaelimisha wafanyakazi kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Umma, Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma Zanzibar na Masuala Mtambuka. Pia, Idara imeratibu Mikutano ya Kamati za Uongozi na Kamati Tendaji za Wizara iliyojadili Sera, Sheria, Miongozo na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Wizara. 124. Mheshimiwa Spika, Idara ya Uendeshaji na Utumishi imefanya ziara za kikazi katika Taasisi ziliopo chini ya Wizara kwa upande wa Pemba na Dar- es Saalam. Lengo la ziara hizi ni kusimamia utendaji kazi kwa taasisi hizo pamoja na kufuatilia changamoto ambazo zimejitokeza na kuzitafutia ufumbuzi. Aidha, Wizara imehudhuria katika vikao vya SADC kuanzia ngazi ya maandalizi Arusha, Dodoma, Bagamoyo na Dar-es-Salaam. Pia, Idara imeratibu ushiriki wa Watendaji Wakuu wa Wizara katika Makongamano, Mikutano na Warsha tofauti nchini China, Urusi, Kazakistani na Ufaransa. Kufuatia ziara hizo nchi yetu imefaidika na ongezeko la watalii kutoka nchi hizo, Mashirika ya ndege kuanzisha safari maalumu Zanzibar pamoja na uimarishaji wa Sekta ya Habari. 125. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Programu ndogo hii iliidhinishiwa jumla ya Shilingi 1,734,968,840/= kwa kazi za kawaida, hadi kufikia Machi 2020 imefanikiwa kupata shilingi 1,217,288,117/= sawa na asilimia 70.16. (Tafadhali angalia kiambatanisho nambari 1D). Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 42 Programu Ndogo: Kuratibu na Kusimamia Mipango Mikuu ya Wizara 126. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Kuratibu na Kusimamia Mipango Mikuu ya Wizara inatekelezwa na Idara ya Mipango, Sera na Utafiti yenye jukumu la kupanga, kutayarisha, kufuatilia na kutathmini mipango, sera, tafiti na Miradi ya Maendeleo ya Wizara. 127. Mheshimiwa Spika, huduma ambazo zinatolewa ni uratibu wa sera na tafiti, kuandaa na kuwasilisha bajeti ya Wizara, kuandaa na kusimamia mipango na miradi ya maendeleo ya Wizara. UTEKELEZAJI HALISI 128. Mheshimiwa Spika, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti imefanya utafiti wa kuangalia “Ushiriki wa jamii katika shughuli za utalii”. Matokeo ya utafiti huo yanaonesha kwamba idadi kubwa ya wananchi waliopo karibu na shughuli za utalii wanafaidika kwa kuwepo kwa shughuli hizo za kitalii kwenye sehemu zao kwani hushiriki kwa njia moja au nyengine kwenye shughuli za utalii na kuongeza kipato kwenye shughuli zao za kila siku. 129. Mheshimiwa Spika, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti imeifanyia Mapitio Sera ya Habari ya mwaka 2008 ambayo imepitwa na wakati. Sera hiyo imewasilishwa kwenye Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Wizara kwa ajili ya kujadiliwa kwa kina na hatua inayofuata ni kuwasilishwa kwenye Vikao vya Makatibu Wakuu kwa ajili ya kujadiliwa. Aidha, Idara imewasilisha rasimu ya Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Utalii ya mwaka 2017 kwa Wadau wa Utalii wa Pemba na Unguja. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 43 Lengo la kuwasilishwa rasimu hiyo ni kujadiliwa na kupatiwa maoni mbali mbali ili iweze kutumika kwa usahihi. 130. Mheshimiwa Spika, Idara imefanya Ufuatiliaji na Tathmini juu ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Wizara kwa upande wa Unguja na Pemba. Miradi iliyofuatiliwa ni ujezi wa Ofisi na Studio za ZBC Pemba, kuimarisha eneo la kihistoria la Mkamandume Pemba, kuimarisha eneo la kihistoria la Mwinyi Mkuu Unguja, kuimarisha eneo la kihistoria la Mvuleni Unguja, Mradi wa Utalii kwa Wote Bungi Unguja na Mradi wa ujenzi wa Beit el Ajaib. Aidha, Katika kuadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Idara imeratibu Ufunguzi na Uwekaji wa Mawe ya Msingi katika Miradi mbali mbali ya Wizara ikiwemo Miradi ya kuimarisha maeneo ya kihistoria ya Bi Khole Bungi, Jumba la Wareno Fukuchani, Jengo la Mwinyi Mkuu Dunga, Mradi wa Ujenzi wa Ofisi na Studio za ZBC Pemba pamoja na Mradi wa Utalii kwa Wote Bungi. 131. Mheshimiwa Spika, Idara imeratibu Vikao vya Ushirikiano baina ya Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (SMZ), Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (SMT) na Wizara ya Maliasili na Utalii (SMT). Katika Vikao hivyo mambo mbali mbali yanayohusu na yasiyohusu Muungano kwa sekta za Habari, Utalii na Mambo ya Kale yamejadiliwa na Wajumbe kutoka pande zote mbili za Muungano. Baada ya majadiliano yamepatikana maazimio ambayo yatarahisisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa. 132. Mheshimiwa Spika, Idara imeandaa taarifa za utekelezaji wa malengo na majukumu ya Wizara na kuziwasilisha Tume ya Mipango. Pia, Idara imewasilisha Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, taarifa Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 44 ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa muda wa miaka mitano kuanzia 2015-2020, utayarishaji wa hotuba ya bajeti ya Wizara pamoja na utayarishaji wa ripoti ya Bango Kitika iliyowasilishwa kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. 133. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha ufanisi wa utendaji kazi kwa wafanyakazi wake, Idara imegharimia masomo ya muda mrefu kwa wafanyakazi wake wawili, mmoja kati yao anasoma Shahada ya Pili ya Uchumi nchini China na wa Pili Shahada ya Pili ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Zanzibar (Zanzibar University). 134. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020, programu hii iliidhinishiwa jumla ya shilingi 303,296,860/= kwa kazi za kawaida na hadi kufikia Machi 2020 imefanikiwa kupata shilingi 160,524,182/= sawa na asilimia 52.93. (Tafadhali angalia kiambatisho namba 1D). Programu Ndogo: Kuratibu na Kusimamia Utawala, Uendeshaji na Mipango Mikuu ya Ofisi Kuu Pemba 135. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Kuratibu na Kusimamia Utawala, Uendeshaji na Mipango ya Ofisi Kuu Pemba inatekelezwa na Ofisi Kuu Pemba. 136. Mheshimiwa Spika, huduma ambazo zinatolewa ni uratibu wa Sera, Tafiti na Mipango Mikuu ya Ofisi Kuu Pemba, kuratibu Miradi ya Maendeleo na kujenga uwezo na mazingira mazuri ya kazi kwa wafanyakazi. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 45 UTEKELEZAJI HALISI 137. Mheshimiwa Spika, Ofisi Kuu Pemba, imeratibu shughuli za sera, tafiti pamoja na utekelezaji wa Miradi inayofanyika kwa upande wa Pemba. Aidha, Ofisi Kuu imeratibu Mikutano na Vikao vya Kamati Tendaji kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa Malengo na Majukumu ya Ofisi Kuu ili kuleta ufanisi wa kazi. Pia, Ofisi Kuu Pemba imefanya Mikutano ya Wadau mbali mbali wa Utalii na Mambo ya Kale ikiwa na lengo la kuhamasisha utalii wa ndani, kuyatunza na kuyalinda maeneo ya kihistoria na Mambo ya Kale pamoja na kusaidia katika ukusanyaji wa mapato yake. 138. Mheshimiwa Spika, katika kushajiisha Utalii Pemba, Ofisi Kuu Pemba imefanya tamasha la Kuhamasisha Utalii wa Ndani ambapo miongoni mwa shughuli zilizofanywa ni pamoja na Mdahalo kwa Wanafunzi wa Skuli za Sekondari juu ya dhana ya Utalii kwa Wote. Wanafunzi kutoka Skuli tano za Madungu Sekondari, Fidel Castro, Uweleni, Chasasa na Chuo cha Kiislam Kiuyu walishiriki Mdahalo huo. Aidha, matokeo ya Mdahalo huu yamesaidia kupunguza dhana potofu zinazozungumzwa Mitaani kuwa Utalii ni Uhuni. Pili, Wanafunzi walipatiwa elimu kuhusu maeneo ya kihistoria yaliyopo Zanzibar na umuhimu wa kuyatunza kwa maslahi yao, Taifa na kizazi cha baadae. Pia, Wanafunzi walielimishwa kuhusu historia sahihi ya Viongozi wetu sambamba na faida za Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964, umuhimu wa kuyalinda na kudumisha amani ya nchi yetu. 139. Mheshimiwa Spika, kupitia tamasha hilo, Ofisi Kuu Pemba imeandaa maonesho ya vyakula vya asili vya Pemba sambamba na kutembelea Makumbusho ya Chake Chake, shughuli ambayo ilihudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama cha Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 46 Mapinduzi. Lengo la shughuli hiyo, ni kuendeleza Utamaduni wa kuyatembelea Makumbusho ya Pemba na kuona fursa za kiutalii zilizopo Pemba. Aidha, Ofisi Kuu imeandaa ziara katika Mto wa Asili uliopo Vitongoji kwa lengo la kuibua na kuongeza idadi ya vivutio vya utalii vilivyopo kisiwani Pemba. 140. Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuimarisha utendaji kazi, Ofisi Kuu imemgharamia masomo ya muda mrefu Shahada ya Uzamivu (PhD) mfanyakazi mmoja nchini China. Aidha, Ofisi Kuu imelipa haki na stahiki za muda wa ziada na likizo kwa wafanyakazi wake ili kuongeza ufanisi wa kazi. 141. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020, programu hii iliidhinishiwa jumla ya shilingi 775,425,540/=, kwa ajili ya kazi za kawaida, hadi kufikia Machi 2020 imefanikiwa kupata shilingi 597,450,676/= sawa na asilimia 77.05. Programu hii imetakiwa kukusanya jumla ya shilingi 52,048,000/=, hadi kufikia Machi 2020, jumla ya shilingi 5,820,000/= zimekusanywa sawa na asilimia 11.18. (Tafadhali angalia kiambatisho namba 1D na 1E). E. MIRADI YA MAENDELEO ITAKAYOTEKELEZWA NA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 142. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 imepangiwa kutekeleza Miradi ya Maendeleo ifuatayo: - i. Kuyaimarisha Makumbusho ya Amani na Makumbusho ya Viumbe Hai yaliyopo Mnazi Mmoja Unguja. ii. Kuimarisha nyumba ya kihistoria ya Beit el Ajaib iliyopo Forodhani –Unguja. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 47 iii. Kuliimarisha eneo la kihistoria la Chwaka Tumbe – Pemba. iv. Kuliimarisha pango la Watoro na pango la Wanakijiji yaliyopo Makangale -Pemba. v. Mradi wa Utalii kwa wote wa Kulipendezesha eneo la Bi Khole kwa awamu ya tatu. vi. Ununuzi na Ufungaji wa Vifaa vya Studio ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Mkanjuni – Pemba. F. MWELEKEO WA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 143. Mheshimiwa Spika, kabla ya kuanza kuusoma muelekeo wa bajeti ninaomba kukujuilisha wewe pamoja na Wajumbe wako wote kuwa, katika mwaka wa fedha 2020/2021 Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma hakitakuwepo tena Chini ya Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale na badala yake kinahamishiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, ili kuunganishwa na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Kupelekwa Chuo hiki SUZA ni Mkakati wa makusudi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wa kuhakikisha Chuo hicho kinafanikiwa kutoa Shahada ya Kwanza ya Uandishi wa Habari. Nichukue fursa hii kutoa pongezi za dhati kwa Serikali chini ya uongozi wa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kulifanikisha suala hili. 144. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021, Wizara ya Habari, Utalii, na Mambo ya Kale imepangiwa jumla ya shilingi 20,389,800,000/=. Kati ya fedha hizo shilingi 14,289,800,000/= kwa matumizi ya kawaida na shilingi 6,100,000,000/= kwa utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Aidha, Wizara imepangiwa kukusanya mapato yanayokwenda Mfuko Mkuu wa Serikali shilingi 6,167,604,000/= Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 48 na kukusanya mapato yanayotumiwa na Taasisi husika shilingi 12,472,128,000/=. (Tafadhali angalia kiambatisho namba 1G, 1H, 1I). 145. Mheshimiwa Spika, katika fedha za matumizi ya kawaida ambazo ni shilingi 14,289,800,000/=, shilingi 4,281,200,000/= ni mishahara kwa taasisi za Wizara zisizo za ruzuku, shilingi 3,692,000,000/= kwa ajili ya matumizi mengineyo kwa taasisi za Wizara zisizo za ruzuku. Aidha, shilingi 3,682,400,000/= kwa ajili ya mishahara kwa taasisi za Wizara za ruzuku na shilingi 2,634,200,000/= ni kwa ajili ya matumizi mengineyo kwa taasisi za Wizara za ruzuku. (Tafadhali angalia kiambatisho namba 1F). 146. Mheshimiwa Spika, katika fedha za miradi ya maendeleo shilingi 2,700,000,000/= zimetengwa kwa ajili ya kuimarisha Makumbusho ya Amani na ya Viumbe Hai yaliyopo Mnazi Mmoja Unguja, Kuimarisha eneo la kihistoria la Chwaka Tumbe na Kuimarisha Pango la Watoro na Pango la Wanakijiji yaliyopo Makangale Pemba. Aidha, shilingi 1,400,000,000/= kwa ajili ya Kununua na Kufunga Vifaa vya Studio ya ZBC Pemba. Pia, shilingi 2,000,000,000/= kwa ajili ya Mradi wa Utalii kwa Wote kwa awamu ya tatu. (Tafadhali angalia kiambatisho namba 1F). G. KUWASILISHA BAJETI YA MFUMO WA PROGRAMU (PROGRAM BASED BUDGET - PBB) KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 147. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale itatumia jumla ya shilingi Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 49 20,389,800,000/= kwa ajili ya kutekeleza Programu Kuu tano ambazo ni: - I. Programu ya Maendeleo ya Habari, Utangazaji na Uchapaji. (Shilingi 8,458,062,270/=). II. Programu ya Maendeleo ya Utalii, Makumbusho, Mambo ya Kale na Utunzaji wa Nyaraka na Kumbukumbu. (Shilingi 4,670,769,160/=). III. Programu ya Utangazaji na Uhamasishaji wa Utalii. (Shilingi 602,830,000/=). IV. Programu ya Kuratibu na Kusimamia Maendeleo ya Utalii. (Shilingi 3,512,470,000/=). V. Programu ya Uendeshaji na Mipango katika Sekta ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale. (Shilingi 3,145,668,570/=) (Tafadhali angalia kiambatisho namba 1G). PROGRAMU KUU YA KWANZA: MAENDELEO YA HABARI, UTANGAZAJI NA UCHAPAJI 148. Mheshimiwa Spika, programu ina jukumu la kuhakikisha kuwa na jamii iliyoimarika katika maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa kupitia habari. Aidha, matokeo ya muda mrefu katika programu hii ni wananchi kupata na kutumia habari zenye kiwango bora. Programu hii imepangiwa jumla ya shilingi 8,458,062,270/= na imepangiwa kusimamia programu ndogo mbili ambazo ni: - i. Upatikanaji na Usambazaji wa Habari (Shilingi 7,165,762,270/=). Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 50 ii. Usimamizi wa Vyombo vya Habari, Utangazaji na Uchapaji (Shilingi 1,292,300,000/=). Programu Ndogo: Upatikanaji na Usambazaji wa Habari 149. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Upatikanaji na Usambazaji wa Habari inatekelezwa na Taasisi na Idara nne ambazo ni, Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Idara ya Habari Maelezo, Shirika la Magazeti ya Serikali na Kampuni ya Usambazaji Maudhui (ZMUX). Jukumu la msingi katika Programu ndogo ni Kuarifu, Kuelimisha na Kuburudisha jamii na kuratibu Uchapishaji wa Magazeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Huduma ambazo zinatarajiwa kutolewa ni urushaji wa vipindi kupitia TV na Redio, utoaji wa taarifa picha, makala, filamu na sinema, utoaji wa magazeti na usambazaji wa maudhui ya utangazaji. 150. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 programu ndogo hii inategemea kutekeleza shughuli zifuatazo: - i. Kuongeza idadi na ubora wa vipindi vya Shirika la Utangazaji vinavyozalishwa ndani ya nchi. ii. Kuwafikia wananchi walio wengi wa Mjini na Vijijini kwa kuwapa taarifa, makala, filamu, picha na sinema zinazohusu maendeleo ya nchi kwa kutumia gari la sinema. iii. Kuongeza idadi ya nakala za Magazeti yanayozalishwa na Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar. iv. Kuongeza idadi ya Ving’amuzi vya ZMUX ili kuwauzia wananchi waweze kufuatilia taarifa na matukio yanayotokezea duniani. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 51 151. Mheshimiwa Spika, ili programu ndogo iweze kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya shilingi 7,165,762,270/= kwa kazi za kawaida na Makusanyo ya Shilingi 2,926,611,000/=. Programu Ndogo: Usimamizi wa Vyombo vya Habari, Utangazaji na Uchapaji 152. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya pili ni Usimamizi wa Vyombo vya Habari, Utangazaji na Upigaji Chapa inatekelezwa na Idara ya Habari Maelezo, Tume ya Utangazaji na Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar. Jukumu la msingi katika programu ndogo hii ni kudhibiti na kusimamia Vyombo vya Utangazaji vya Serikali na vya binafsi vinavyoanzishwa nchini ili kwenda sambamba na Sheria ya Habari na Utangazaji pamoja na kukuza viwango vya Machapisho mbali mbali. Huduma ambayo inatarajiwa kutolewa ni udhibiti na usimamizi wa shughuli za habari na utangazaji kupitia Sera na Sheria za Habari na Utangazaji pamoja na kusimamia shughuli za upigaji chapa kwa Taasisi za Serikali na kutoa huduma za Bohari Kuu ya vifaa vya Ofisi na kuandikia. 153. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 programu ndogo hii inategemea kutekeleza shughuli zifuatazo: - i. Kukuza Mfumo wa Kufuatilia na Kurikodia Redio za FM. ii. Kuzitafsiri Kanuni mbali mbali za Utangazaji kwa Lugha ya Kiswahili. iii. Kutoa Huduma ya Uuzaji wa Vifaa vya Kuandikia kwa Taasisi zote za Serikali. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 52 iv. Kuchapisha Nyaraka zote za Serikali pamoja na Magazeti ya Shirika la Magazeti ya Serikali. 154. Mheshimiwa Spika, ili programu ndogo iweze kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya shilingi 1,292,300,000/= kwa kazi za kawaida na Makusanyo ya shilingi 9,928,770,375/=. PROGRAMU KUU YA PILI: MAENDELEO YA UTALII, MAKUMBUSHO, MAMBO YA KALE NA UTUNZAJI WA NYARAKA NA KUMBUKUMBU 155. Mheshimiwa Spika, programu hii ina jukumu la kuhakikisha kuwa maeneo ya Kihistoria na Mambo ya Kale yanaendelezwa kwa kuhifadhiwa, kulindwa na kutangazwa. Aidha, kuwepo Usimamizi bora wa Kumbukumbu na Nyaraka kwa ajili ya matumizi ya Taifa pamoja na Kuratibu na Kuendeleza shughuli za Utalii. Aidha, matokeo ya muda mrefu ya programu hii ni Kuyaimarisha Maeneo ya Kihistoria, Kuwepo kwa Usimamizi Imara wa Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa pamoja na kuwa na Utalii wenye Tija. Programu hii imepangiwa jumla ya shilingi 4,670,769,160/= na itakuwa na programu ndogo tatu ambazo ni: - i. Uendelezaji wa Makumbusho na Urithi wa Mambo ya Kale. (shilingi 3,774,417,000/=). ii. Uhifadhi wa Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa. (shilingi 668,202,460/=). iii. Kuratibu na Kuendeleza Utalii (shilingi 228,149,700/=). Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 53 Programu Ndogo: Uendelezaji wa Makumbusho na Urithi wa Mambo ya Kale 156. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Uendelezaji wa Makumbusho na Urithi wa Mambo ya Kale inatekelezwa na Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale. Jukumu la msingi katika programu ndogo ni Kuimarisha, Kuendeleza na Kuyahifadhi Maeneo ya Kihistoria na Mambo ya Kale yaliyopo nchini. Huduma zinazotarajiwa kutolewa ni Kuendeleza Urithi wa Mambo ya Kale pamoja na Uelimishaji na Ushirikishwaji wa Jamii katika Uhifadhi na Uendelezaji wa Maeneo ya Kihistoria. 157. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 programu ndogo hii inategemea kutekeleza shughuli zifuatazo: - i. Kuanzisha Mfumo Maalumu wa Ukusanyaji wa Mapato katika Maeneo ya Kihistoria kwa Njia ya Kielektroniki. ii. Kufanya Utafiti wa Akiolojia katika Kijiji cha Fukuchani. iii. Kuanzisha Makumbusho ya Historia ya Wareno Fukuchani Unguja na Historia ya Mkamandume Pujini Pemba iv. Kutoa Elimu kwa Jamii juu ya Umuhimu wa Kuyalinda na Kuyahifadhi Maeneo ya Kihistoria yaliyopo Nchini. 158. Mheshimiwa Spika, ili programu ndogo iweze kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya shilingi 3,774,417,000/= kwa kazi za kawaida na Makusanyo ya shilingi 245,031,000/=. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 54 Programu Ndogo: Uhifadhi wa Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa 159. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Uhifadhi wa Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa inatekelezwa na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu ya Taifa Zanzibar. Jukumu la msingi katika programu ndogo hii ni Kuhifadhi na Kusimamia Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa. Huduma ambazo zinatarajiwa kutolewa ni Kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa. 160. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 programu ndogo hii inategemea kutekeleza shughuli zifuatazo: - i. Kuimarisha Uhifadhi na Utunzaji wa Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar. ii. Kufanya Ukaguzi na kutoa Elimu ya Utunzaji na Utumiaji bora wa Nyaraka na Kumbukumbu ili kuongeza ufanisi wa utendaji katika sekta ya Umma. iii. Kuimarisha Uhifadhi wa Nyaraka na Kumbukumbu ili kulinda na kuendeleza Urithi wa Historia na Utamaduni kwa Manufaa ya Taifa. 161. Mheshimiwa Spika, ili programu ndogo iweze kufanya kazi zake katika mwaka wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya shilingi 668,202,460/= kwa kazi za kawaida na Makusanyo ya shilingi 7,094,000/=. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 55 Programu Ndogo: Kuratibu na Kuendeleza Utalii 162. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Kuratibu na Kuendeleza Utalii inatekelezwa na Idara ya Utalii. Jukumu la msingi katika programu ndogo ni Kusimamia na Kuratibu shughuli za Utalii pamoja na Kuwahamasisha wananchi juu ya dhana ya Utalii kwa Wote. Matokeo ya muda mrefu ni kuwa na utalii wenye kuleta manufaa kwa wananchi. Huduma zinazotarajiwa kutolewa ni Uratibu na Uendelezaji wa shughuli za Utalii. 163. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 programu ndogo hii inategemea kutekeleza shughuli zifuatazo: - i. Kuendelea kuwaelimisha wananchi juu ya dhana ya Utalii kwa Wote. ii. Kuwapa elimu Wajasiriamali wadogo wadogo wa kazi juu ya namna bora ya utengenezaji wa kazi za utalii. iii. Kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya Utalii kwa manufaa ya Taifa. 164. Mheshimiwa Spika, ili programu ndogo iweze kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya shilingi 228,149,700/= kwa kazi za kawaida. PROGRAMU KUU YA TATU: UTANGAZAJI NA UHAMASISHAJI WA UTALII 165. Mheshimiwa Spika, programu hii inatekelezwa na Kamisheni ya Utalii kupitia Idara ya Masoko yenye jukumu la Kupanga Mikakati na Kuitangaza Zanzibar Kiutalii ndani na nje ya nchi ili kuleta Tija kwa Maslahi ya Taifa. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 56 166. Mheshimiwa Spika, lengo kuu la programu ni kuongeza uelewa kwa Wakaazi wa Tanzania na jamii ya kimataifa kuhusu bidhaa na huduma za Utalii zilizopo Zanzibar. Matokeo ya muda mrefu katika programu hii ni kuifanya Zanzibar kuwa Kituo Bora cha Utalii chenye kukidhi mahitaji ya jamii na watalii. Huduma inayotarajiwa kutolewa ni kuitangaza Zanzibar ndani na nje ya nchi. 167. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 programu ndogo hii inategemea kutekeleza shughuli zifuatazo: - i. Kuandaa na kushiriki Maonesho, Mikutano na Makongamano ya Utalii ya Kitaifa na Kimataifa ili kushawishi Mawakala wa Utalii, Mashirika ya Ndege, Kampuni za Meli za Kitalii kuleta Wageni Zanzibar, pamoja na kuvutia Wenyeji kutembelea Vivutio vya Utalii vya Zanzibar. ii. Kuwaalika Waandishi wa Habari za Utalii wa Kimataifa, Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii na Watu Mashuhuri ili Zanzibar ipate kutangazwa ndani na nje ya nchi. iii. Kutekeleza programu Maalumu ya Kuitangaza Zanzibar hususan katika Masoko Makuu ambayo yameathirika na Janga la Maradhi ya Corona (COVID-19). iv. Kuandaa Vielelezo vya kutangaza Utalii kwa kushirikiana ipasavyo na Ofisi za Ubalozi za Tanzania. 168. Mheshimiwa Spika, ili programu hii iweze kutekelezwa kwa ufanisi katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya shilingi 602,830,000/= kwa kazi za kawaida. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 57 PROGRAMU KUU YA NNE: KURATIBU NA KUSIMAMIA MAENDELEO YA UTALII 169. Mheshimiwa Spika, programu hii inatekelezwa na Kamisheni ya Utalii kupitia Idara ya Mipango na Sera, ina jukumu la Kuratibu, Kusimamia na Kuendeleza Utalii pamoja na Kuwajengea Uwezo Wafanyakazi na Kuweka Mazingira Mazuri ya Kazi. 170. Mheshimiwa Spika, lengo kuu la programu hii ni Kuongeza Tija ya Sekta ya Utalii na kuweka Mazingira na Rasilimali Watu bora katika Uandaaji, Utekelezaji na Usimamizi wa Sera na Mipango ya Utalii. Matokeo ya muda mrefu katika programu hii ni Kuwepo kwa Utalii Endelevu na Wenye Kuhimili Ushindani. Huduma zinazotarajiwa kutolewa ni Uratibu na Uendelezaji wa Utalii, Kuwajengea Uwezo Wafanyakazi na kuweka Mazingira Mazuri ya Kazi. 171. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 programu ndogo hii inategemea kutekeleza shughuli zifuatazo: - i. Kufanya Ukaguzi wa Miradi ya Utalii na Doria katika Maeneo ya Utalii pamoja na Kuandaa Vigezo na Viwango kwa Mashamba ya Viungo yanayotoa Huduma kwa Watalii. ii. Kuweka Mazingira bora ya kazi na kutoa Mafunzo kwa Wafanyakazi na Wajumbe wa Kamati za Utalii za Wilaya. iii. Kutoa Mafunzo kwa watoa Huduma za Utalii ili Kuimarisha Ubora wa Huduma kwa Wageni. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 58 iv. Kufanya utafiti wa Utokaji wa Watalii (Tourism Exit Survey) ili kufahamu viashiria muhimu vya upimaji wa ukuaji wa sekta ya utalii ikiwemo matumizi ya Mtalii kwa siku pamoja na siku zao za ukazi. 172. Mheshimiwa Spika, ili programu iweze kutekelezwa kwa ufanisi katika mwaka wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya shilingi 3,512,470,000/= kwa kazi za kawaida na Makusanyo ya shilingi 5,492,029,000/=. PROGRAMU KUU YA TANO: UENDESHAJI NA MIPANGO KATIKA SEKTA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE 173. Mheshimiwa Spika, programu hii ina jukumu la Kusimamia na Kuratibu Mipango Mikuu, Sera na Tafiti pamoja na Usimamizi na Uuendeshaji mzuri wa Rasilimali Watu katika Wizara. Matokeo ya muda mrefu ya programu hii ni kuwepo kwa Usimamizi bora wa Mipango na Uendeshaji wa Rasilimali Watu katika Wizara. Programu hii imepangiwa jumla ya shilingi 3,145,668,570/= na itasimamia programu ndogo tatu ambazo ni: - i. Utawala na Uendeshaji katika Sekta za Habari, Utalii na Mambo ya Kale. (Shilingi 1,947,733,970/=) ii. Kuratibu na Kusimamia Mipango Mikuu ya Wizara. (shilingi 353,101,960/=) iii. Kuratibu na Kusimamia Utawala, Uendeshaji na Mipango ya Ofisi Kuu Pemba. (Shilingi 844,832,640/=) Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 59 Programu Ndogo: Utawala na Uendeshaji katika Sekta za Habari, Utalii na Mambo ya Kale 174. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Utawala na Uendeshaji katika Sekta za Habari, Utalii na Mambo ya Kale inatekelezwa na Idara ya Uendeshaji na Utumishi, ambayo ina jukumu la Kusimamia shughuli zote za Utawala, Utumishi, Maendeleo, Wajibu na Maslahi ya Wafanyakazi wa Wizara. 175. Mheshimiwa Spika, lengo kuu la programu ndogo hii ni Usimamizi na Uendeshaji mzuri wa Rasilimali Watu wa Wizara. Huduma zinazotarajiwa kutolewa ni Kujenga uwezo na Mazingira Mazuri ya Kazi kwa Wafanyakazi na Usimamizi wa Mpango wa Manunuzi na Fedha. 176. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 programu ndogo hii inategemea kutekeleza shughuli zifuatazo: - i. Kupima utendaji kazi kwa Wafanyakazi wa Wizara kwa lengo la kuimarisha utendaji wa kazi. ii. Kuhakikisha Wafanyakazi wanapatiwa vitendea kazi vya kutosha ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. iii. Kuimarisha Mashirikiano baina ya Wizara, Taasisi na Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi. 177. Mheshimiwa Spika, ili programu ndogo iweze kutekelezwa kwa ufanisi katika mwaka wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya shilingi 1,947,733,970/= kwa kazi za kawaida. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 60 Programu Ndogo: Kuratibu na Kusimamia Mipango Mikuu ya Wizara 178. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Kuratibu na Kusimamia Mipango Mikuu ya Wizara inatekelezwa na Idara ya Mipango, Sera na Utafiti yenye jukumu la Kupanga, Kutayarisha, Kuratibu, Kufuatilia na Kutathmini Mipango, Sera, Tafiti na Miradi ya Maendeleo ya Wizara. 179. Mheshimiwa Spika, lengo kuu la programu ndogo ni Kusimamia na Kuratibu Mipango Mikuu, Sera na Tafiti za Wizara. Huduma ambazo zinatarajiwa kutolewa ni Uratibu wa Sera na Tafiti, Kuratibu, Kuandaa Bajeti pamoja na Kuratibu na Kusimamia Mipango na Miradi ya Maendeleo ya Wizara. 180. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 programu ndogo hii inategemea kutekeleza shughuli zifuatazo: - i. Kufuatilia na Kutathmini Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Wizara. ii. Kusimamia Sera na Tafiti zinazotekelezwa na Wizara. iii. Kuratibu Vikao vya Ushirikiano kwa sekta za Habari, Utalii na Mambo ya Kale baina ya SMZ na SMT. 181. Mheshimiwa Spika, ili programu ndogo iweze kutekelezwa kwa ufanisi katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla shilingi 353,101,960/= kwa kazi za kawaida. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 61 Programu Ndogo: Kuratibu na Kusimamia Utawala, Uendeshaji na Mipango Mikuu ya Ofisi Kuu Pemba 182. Mheshimiwa Spika, programu ndogo ya Kuratibu na Kusimamia Utawala, Uendeshaji na Mipango ya Ofisi Kuu Pemba, ina jukumu la Kuhakikisha kuwa Majukumu, Malengo na shughuli zote za Wizara zilizopangwa zinatekelezwa kwa ufanisi kwa upande wa Pemba. 183. Mheshimiwa Spika, lengo kuu la programu ndogo ni Kusimamia na Kuratibu shughuli za Utawala, Uendeshaji na Mipango Mikuu ya Wizara katika Ofisi Kuu-Pemba. Huduma ambazo zinatarajiwa kutolewa ni Uratibu wa Sera, Tafiti na Mipango Mikuu ya Ofisi Kuu-Pemba, Kuratibu Miradi ya Maendeleo na Kuwajengea Uwezo Wafanyakazi na Mazingira mazuri ya kazi. 184. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 programu ndogo hii inategemea kutekeleza shughuli zifuatazo: - i. Kuratibu shughuli zote za Wizara kwa upande wa Pemba. ii. Kuandaa Tamasha la Vyakula vya Asili vya Pemba. iii. Kupima utendaji kazi kwa Wafanyakazi wa Wizara Pemba kwa lengo la kuimarisha utendaji wa kazi. iv. Kuwapatia Wafanyakazi vitendea kazi vya kutosha ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 62 185. Mheshimiwa Spika, ili programu hii iweze kutekelezwa kwa ufanisi katika mwaka wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya shilingi 844,832,640/= kwa kazi za kawaida na makusanyo ya shilingi 40,192,000/=. H. SHUKURANI 186. Mheshimiwa Spika, kabla ya kuhitimisha hotuba yangu, naomba kutoa Shukurani za kipekee kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuendelea kuiongoza vyema nchi yetu katika misingi ya haki na utawala bora. Pia, ninamshukuru kwa kutuunga mkono katika shughuli mbali mbali za Wizara ambapo miongozo anayotupa, Wizara imeichukua na kuifanya ndio dira ya utekelezaji wa shughuli zake za kila siku, ninamuombea kwa Mwenyezi Mungu amzidishie ujasiri katika utendaji wake wa kazi. 187. Mheshimiwa Spika, shukurani maalumu ziwaendee waliochangia katika kutayarisha hotuba hii na wasaidizi wangu wa karibu katika Wizara ambao ni Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Bi. Chumu Kombo Khamis, Katibu Mkuu Bi. Khadija Bakari Juma, Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Utalii na Mambo ya Kale Dkt. Amina Ameir Issa na Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Habari Dkt. Saleh Yussuf Mnemo, Afisa Mdhamini Khatib Juma Mjaja. Wengine ni Mshauri wa Rais wa Mambo ya Kale Mheshimiwa Ali Mzee Ali, Mshauri wa Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Nd. Abdallah Mwinyi Khamis, Makatibu Watendaji, Afisa Mdhamini Pemba, Wakurugenzi wa Taasisi za Wizara na wasaidizi wao wote kwa Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 63 kufanya kazi kwa juhudi, maarifa, uadilifu na umakini mkubwa. Kwa kweli wamekuwa wakinisaidia sana kutekeleza majukumu yangu. Pia, nawashukuru Wenyeviti wa Kamati na Bodi mbali mbali kwa kusimamia vyema taasisi zetu na kunishauri kwa hekima na busara. 188. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee naomba kuwashukuru wafanyakazi wote wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Washirika wa Habari, Washirika wa Utalii, Washirika wa Mambo ya Kale na wananchi wote wa Unguja na Pemba kwa michango yao katika kufanikisha shughuli za Wizara. Pia, shukurani maalumu ziende kwa Vyombo vya Habari vya Serikali na Binafsi, kwa kufanikisha kurusha vipindi mbali mbali vya kuelimisha jamii kiuchumi, kijamii na kisiasa. 189. Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hii kuishukuru Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Tume ya Mipango kwa ushirikiano mkubwa waliotupa kwa mahitaji ya fedha na ushauri kwa kipindi chote tunapohitaji. 190. Mheshimiwa Spika, naomba uniruhusu nizishukuru nchi ambazo zimeshirikiana kwa karibu na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale, katika kufanikisha kutekeleza Malengo na Majukumu ya Wizara kupitia sekta zake. Miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na Oman, China, Urusi, Kazakistani, Korea Kusini, India, Ufaransa, IPP Media, Azam Media na TBC. 191. Mheshimiwa Spika, mwisho naomba kukushukuru wewe binafsi, pamoja na Waheshimiwa Wajumbe wote wa Baraza lako Tukufu kwa kunisikiliza kwa Utulivu, Umakini na Usikivu wa hali ya juu. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 64 I. MAOMBI YA FEDHA KWA AJILI YA KUTEKELEZA PROGRAMU ZA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 192. Mheshimiwa Spika, naliomba Baraza lako Tukufu kujadili kwa kina matumizi ya jumla ya Wizara ya shilingi 20,389,800,000/=. Kati ya hizo shilingi 14,289,800,000/= kwa kazi za kawaida na shilingi 6,100,000,000/= kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Katika jumla kuu ya Wizara limo fungu la fedha la Kamisheni ya Utalii ambalo ni shilingi 4,115,300,000/=, kati ya hizo shilingi 2,115,300,000/= kwa kazi za kawaida na shilingi 2,000,000,000/= kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za mradi. Aidha, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe makusanyo ya mapato ya shilingi 6,167,604,000/= kwa fedha zinazoingia katika Mfuko Mkuu wa Serikali. Pia, makusanyo ya shilingi 12,472,128,000/= ambazo hukusanywa na taasisi zilizoruhusiwa kutumia makusanyo hayo. J. HITIMISHO 193. Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima nawaomba Wajumbe wa Baraza lako Tukufu Waipokee, Waijadili, Watushauri, Watuelekeze na baadae Watupitishie bajeti hii ya Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale. 194. Mheshimiwa Spika, Naomba Kutoa Hoja. Mheshimiwa; Mahmoud Thabit Kombo (MBM), Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale. Hotuba ya Bajeti Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2020/2021 65 VIAMBATISH

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.