Habari za Punde

MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI.

Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson (kushoto) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Mohamed Khamis cheti cha kutambua mchango wa Tume katika kuwawezesha Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kutimiza majukumu yao. Tume imekuwa mdau muhimu wa hospitali hiyo kwa kushirikiana kwa ukaribu katika mambo mbalimbali yanayohusu uboreshaji wa kazi za wauguzi. Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wauguzi Duniani yalifanyika hospitalini hapo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki

Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson (katikati- aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma waliojumuika na Wauguzi wa hospitali hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika hospitalini hapo Mwishoni mwa wiki (Mei 15, 2020). Wa pili kutoka kushoto waliokaa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge.

Picha na Mbaraka Kambona

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.