Habari za Punde

Matukio 37 ya udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa Kusini Unguja


Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya kusini Unguja, Zakaria Fabian Kitindde alipokuwa akizungumza na waandishi wa Tamwa ofisini kwake

 

Jumla ya matukio 37 ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto yameripotiwa katika wilaya ya kusini  Unguja kutoka mwaka 2019 hadi 2020.

Hayo yamesemwa na afisa ustawi wa jamii wilaya kusini Unguja Zakaria Fabian Kitinde wakati alipokua akitoa ripoti ya matukio hayo katika ukumbi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tamwa-Zanzibar.

Alisema matukio hayo yamejumuisha kuanzia mwezi julai 2019 hadi mwezi mei 2020 ambapo yamegawika katika matukio mbali mbali.

Akitoa ufafanuzi wa matukio hayo ni pamoja na watoto kubakwa,kulawitiwa,mimba za umri mdogo na hata kukizana na sharia pamoja na kutoroshwa.

Akitaja sababu za uwepo wa matukio hayo alisema ni pamoja na wanajamii kuwa na elimu ndogo kuhusu madhara ya matendo hayo katika jamii.

Akifafanua zaidi alisema anaamini iwapo jamii ingekfahamu vyema madhara ya matukio ya udhalilishaji katika jamii ni wazi kuwa matendo hayo yengeweza kupungua na hata kuondoka kabisa.

Aidha alisema bado kuna changamoto kubwa wanakabiliana nazo iwapo mtuhumiwa wa matendo hayo atakua mfanya kazi wa taasisi ambazo zinahusika na maswala ya utendeji wa kisheria.

‘’Mtoto anaefanyiwa udhalilishaji si rahisi sana kumbukumbu kufutika kwenye kichwa chake na hubaki muda mrefu hivyo ni wazi inamadhawa makubwa kisaikolojia’’aliongezea.

Nae Ali Haji Adam ambae ni Mwenyekiti wa masheha wilaya ya kusini Unguja  alisema baadhi ya watu wengi kwenye jamii wanashindwa kutoa ushirikiano dhidi ya kesi hizo kutokana na kesi hizo kukaa muda mrefu.

Alisema iwapo Serikali inataka kusaidia wananchi wanapaswa kutafakari kwa kina na kuhakikisha kesi hizo zinaendeshwa kwa haraka zaidi vyenginevyo watu wengi wataka tamaa.

‘’Tunamoyo thabiti wa kusaidia wenzetu lakini kwa kweli wenzetu wanakufa moyo hebu tujiulize kwa mwaka mzima huu kuna kesi ngapi bado zipo kwenye ofisi za mkurugenzi wa mashtaka DPP’’alihoji.

Akizungumzia kuhusu suala la baadhi ya walimu wa madrasa kuhusishwa na matendo hayo kiongozi wa dini ya kiislamu kutokoa wilaya ya kusini Unguja Mwazini Jogoo Hassan  alisema ni kweli baadhi ya walimu wamekua wakiwafanyika matendo hayo watoto wadogo.

Alisema jambo hilo limekua likiinza sura mbaya walimu wa madrasa na vyuoni na kwamba ipo haja walimu wote kubadilika.

Alisema wao wamekua wakifuatilia kwa umakini zaidi suala hilo na iwapo kuna mwalimu atabainika muhusika husimamishwa na kucha mamlaka husika kumchukulia sharia.

Afisa sharia kutoka Chama cha waandishi wa habari wanawake Tamwa-Zanzibar Ulfat Abdi alisema ipo haja jamii kubadilika ikiwemo kukubali kuunga mkono jitihada za wanaharakati.

Alisema anaamini iwapo jamii itaunga mkono jitihada hizo ikiwemo kuacha muhali ni wazi kuwa wanaotenda matendo hayo wote watadhibitiwa pamoja na kuhumiwa kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.