Habari za Punde

Mwakilishi wa kuteuliwa aitaka jamii kuendeleza utamaduni na silka za Mzanzibari

Na Takdir Suweid Mkoa wa Mjini Magharibi.                                                      .
Mwakilishi wa kuteuliwa na Rais, Ahmada Abdulwakiil Shaa ameitaka Jamii kupendana na kusaidiana katika masuala mbalimbali ili kuendeleza Utamaduni na Silka za Mzanzibar.
Ameyasema hayo huko kwa Mchina Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ wakati alipokuwa akikabidhi msaada wa vyakula kwa wafanya kazi wake na wasiojiweza.
Amesema ameamua kutoa Mchele, Sukari, Sabuni na mafuta ya kupikia ili waweze kujikimu katika kipindi cha Skuu ya Idilfitri na Corona.
Amesema Zanzibar imepata hesma kubwa ndani na nje ya nchi kutokana na Wananchi wake kuwa  na ukarimu na Uzalendo hivyo unahitaji kuendelezwa kwa kizazi cha sasa na kijacho.
 Nao baadhi ya waliopatiwa msaada huo wamesema umeweza kuwasaidia kwani wanaishi katika maisha magumu na yakubahatisha hasa katika cha Maradhi ya Covid 19.
Hivyo amewaomba Wenye uwezo kuwasaidia wasiojiweza ili waweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha walionayo katika familia zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.