Habari za Punde

Muonekano wa Jengo Jipya la ZURA Linatarajiwa Kutumika Mwezi Ujao Baada ya Kumalizika Ujenzi Wake.

Muonekano wa Jengo Jipya la Zura kama linavyoonekana pichani baada ya kukamilika Ujenzi wake na kutarajiwa kuanza matumizi yake mwezi ujao kutowa huduma za Kiofisi kwa Wizara husika katika jengo hilo.

Na.Hafsa Golo -Zanzibar leo.
JENGO jipya la Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Maisara, linatarajiwa kutumia mwezi  Juni mwaka huu.
Hadi kukamilika ujenzi jengo hilo umegharimu shilingi bilioni 19.5. Naibu Mkurugenzi wa ZURA, Hemed Salim Hemed, alieleza hayo wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Maisara.
Alisema jengo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha huduma kutokana na kuwepo kwa teknolojia za kisasa.
Aliahidi kwamba kutakuwa na mabadiliko makubwa ya kiutendaji ambayo yatasaidia kuleta ufanisi kwa watendaji wa mamlaka hiyo.
Alisema katika kuhakikisha taasisi hiyo inakwenda na kasi ya mabadiliko ya kiutendaji na kufikia malengo ya serikali, inaendelea kuwajengea uwezo wa kitaalamu wafanyakazi wake ili waweze kutoa huduma bora.
 “Jengo letu ni zuri na litakuwa na samani bora zenye kukidhi mahitaji hivyo lazima tufanye kazi kwa bidii na kwa maslahi ya nchi yetu,”alisema.
Nae Msimamizi wa jengo hilo, Sleyum Mustafa Jumbe, aliwahakikishia watendaji kupata huduma bora na za mfano ambazo zitasaidia kuongeza ufanisi wa kazi.
Aliwashauri wananchi kulitumia jengo hilo kwa kupata huduma na na kutoa maoni yao kuhusu sekta za maji na nishati.
Jengo hilo lina ghorofa saba litatumiwa na ZURA, Wizara ya Ardhi Nyumba, Maji na Nishati, ZPRA,  ZPDC na idara ya nishati.  

NA HAFSA GOLO

1 comment:

  1. Hizo fedha za ujenzi tungepata maji Zanzibar nzima, lkn Leo hii shida tupu, haya hamieni kuleni kipupwe

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.