Habari za Punde

Mvua za Masika Zaleta Athari Kwa Wananchi Kisiwani Pemba

MKUU wa Mkoa Kusini Pemba Mhe.Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na Wananchi na kuwafariji kutokana na kupata athari za mvua za masika katika Kijiji cha Mwambe zaidi ya nyumba 79  zimeezulia mapaa za nyumba hizo kutokana na upepo.
KUFUATIA mvua kubwa kuendelea kunyesha baadhi ya maeneo nyumba zimeanza kurishai na nyengine kudidimia chini, pichani moja ya nyumba katika kijiji cha Miburani Pembeni ikiwe imewekewa mwega ili ukuta wake usianguke baada ya kuachana kwa mvua
MMOJA ya Paa la Nyumba likiwa chini baada ya kuezuliwa na upepo mkali uliovuma, katika kijiji cha Jombwe na Mkchakwe huko Mwambe wilaya ya mkoani na kuleta taharuki kwa wananchi na kukosa makaazi yao
MMOJA ya nyumba iliyo didimia chini katika kijiji cha miburani shehia ya Pembeni Wete, kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Pemba
MKUU wa Wilaya ya Mkoani Issa Juma Ali, akitoa maeleokezo ya moja ya nyumba iliyoachana sehemu ya chini huku ukuta ukibambuka katika kijiji cha Nanguji shehia ya Kendwa, kwa viongozi wa kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Kusini Pemba ilipofanya ziara ya kuangalia athari za mvua hizo 
MAFUNDI wa kuwezeka wakiwa katika harakati za urudishaji wa sehemu ya moja ya paa la nyumba iliyoathiriwa na upepo mkali uliovuma katika maeneo ya mwambe Mkoani .(PICHA NA ABDI SULEIMAN)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.