Habari za Punde

Ndege huyu alisafiri vipi umbali mrefu zaidi duniani?


Safari ya ndege huyu imekuwa ikifuatiliwa kwenye mitandao ya kijamii

Kwa kutumia mbinu ya kumuwekea setilaiti ndege, wanasayansi wamemfuatilia ndege ambaye amepaa zaidi ya maili 7,500 (sawa na kilomita 12,000) kutoka Afrika Kusini hadi katika eneo la kuzalia lililopo Mongolia.
Ndege huyo ameweza kupita na kunusurika baada ya kuvuka maji na upepo mkali wa baada ya kuvuka nchi 16.
Imekua ni "safari ya tembo", wanasema wanasayansi. Setilaiti ambayo huambatanishwa na ndege wawapo safarini (Cuculus canorus), ilipewa jina la Onon baada ya ndege aitwae Mongolian river, kuondoka katika makazi yake ya msimu wa baridi nchini Zambia tarehe 20 Machi.
Onon ni moja ya ndege watano waliofuatiliwa safari zao kwa kuwekewa setilaiti Mongolia wakati wa msimu wa majira ya joto na mradi wa Mongolia Cuckoo - ulioanzishwa kwa ushirikiano baina ya wanasayansi wa eneo hilo na Wakfu wa Uingereza - British Trust for Ornithology (BTO) kwa ajili ya kufuatilia umbali wa safari ambazo ndege wanaweza kufika wanapohama.
Onon amevuka maelfu ya kilomita za Bahari ya Hindi bila kusimama, akipaa kwa wastani wa kasi ya Kilomita 60 kwa saa na kuvuka nchi zilizo mbali mbali kama Kenya, Saudi Arabia na Bangladesh.
Kati ya ndege watano waliowekwa alama, Onon ndiye pekee aliyerekodiwa kukamilisha safari yake ya kurudi ya kushangaza.
Ndege mwingine aliyewekwa alama, kwa jina Bayan, ambaye aliishi sehemu ya muda wake wa majira ya baridi karibu na Mlima Kilimanjaro Afrika Mashariki, alisafiri hadi Yunnan China - lakini anaaminiwa kuwa alikufa kutokana na uchovu au aliuawa kwa ajili ya chakula.
Ramani ya safari ya ndege
Alipaa, kilomita 10,000 katika kipindi cha wiki mbili tu , jambo lililowafanya wanasayansi kuamini kuwa angewasili akiwa mwenye njaa sana na mwenye uchovu na asingeweza kuwa chonjo vya kutosha kuepuka hatari.
Daktari wa wakfu wa (BTO) Dkt Chris Hewson anasema kuwa mradi wa kuwawekea setilaiti ndege umefichua mengi kuhusu uhamiaji wa mbali wa ndege.
"Ninadhani kubwa la kujifunza ni kwamba ndege wan uwezo wa kusafiri mbali sana na mara nyingi kwa kasi ili kuweza kupata mazingira mazuri kwa ajili ya kupata chakula na pia kujua ni wapi pa kwenda kupata kupata pepo zinazowafaa, kwa mfano, kuvuka Bahari ya Hindi ,"alisema.
"Ka hiyo garama ya kuhama sio nzuri kama ilivyodhaniwa kipindi cha nyuma ."
Lakini hatari kwa ndege hawa wanaohama zipo kila wakati, kutoka maadui wakiwemo awindaji haramu,dhoruba , hadi njaa.
Lakini -kama anavyoelezea Dkt Hewson - katika wakati ambapo ni wachache wetu tunaoweza kupaa kokote kutokana na virusi vya corona, kuna kitu kinachotuhakikishia juu ya ndege anayesafiri umbali mkubwa , inatuonyesha kuwa dunia bado inafanya kazi.
Safari za ndege zimekua zikufuatiliwa na wengi katika mitandao ya kijamii. Mmoja wa watumiaji wa mitandao hiyo ali tweet kuhusu kuwasili salama kwa Onon nchini Mongolia: "Nimeipenda hii… kijana mdogo anasafiri safari ambazo hatuwezi kuzifanya! Anatupeleka mahali. Asante kwa kutushirikisha!"

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.