Habari za Punde

ZECO washauriwa kuwashirikisha wananchi wanapotaka kuweka miundombinu

Takdir Suweid, 
Wilaya ya Magharibi ‘’B" 

 Watendaji wa Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) wameshauriwa kuwashirikisha Wananchi wakati wanataka kuweka miondombinu yao ili kunusuru mizozo inayoweza kujitokeza kati yao.

 Akizungumza katika kikao Cha Wananchi wa Shehia ya Pangawe ‘’Plan’’ na Shirika hilo, Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe Khamis Juma Maalim amesema Mikutano ya pamoja itasaidia Zeco kuibua matatizo Wananchi na kuyapatia ufuimbuzi jambo ambalo litawawezesha kufanya kazi kwa Ufanisi. 

 Amesema Wananchi Wanahitaji kupatiwa huduma ya Umeme lakini ni vyema kuwashirikisha na kuangalia Usalama wao kabla ya kuchukuwa maamuzi ya kuweka Miondombinu hiyo.

 Aidha amewaomba Wananchi kushirikiana na Zeco wakati wanapotafuta sehemu ya kuweka Miondombinu kama vile Nguzo na Transfoma ili kuliwezesha Shirika kutoa huduma bora kwa Wananchi. 

 Kwa upande wake Meneja Mahusiano huduma kwa Wateja Shirika la Umeme Zanzibar Zeco Salum Abdallah Hassan amesema tatizo kubwa linalowakabili ni Idadi kubwa ya Wateja,Uharibifu wa Miondombinu na maeneo ya kuweka Transfoma wakati wanapohitaji. 

 Hivyo amewaomba Wananchi kushirikiana na Shirika hilo katika kuyapatia Ufumbuzi matatizo hayo. 

 Nao Wakaazi wa Pangawe Plan Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ wamewapongeza Viongozi wa Jimbo na Zeco kwa kukubali maamuzi ya kubadilisha eneo la kwanza walilotakwa kuweka Transfoma ya Umeme na kuhamishia sehemu nyengine waliyokubaliana ambayo ni Salama kwa Wananchi na Mali zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.