Habari za Punde

Tetesi za soka Jumamosi 30.05.2020: Sane, Hernandez, Hendrick, Bellingham

Hernandez aliwahi kushinda Kombe la Dunia nchini Urusi
Bayern Munich iko tayari kumtoa mchezaji wake mlinzi Lucas Hernandez, 24, kwa Manchester City wakati inapoendelea na azma yake ya kumwinda winga wa Ujerumani, 24, Leroy Sane. (TZ - via Manchest5r Evening News)
Mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 27, anatarajiwa kwamba uhamisho wake hadi Paris St-Germain utakuwa wa kudumu baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya £51.2m na Inter Milan. (Sky Sports)
Aliyekuwa nahodha wa Manchester City Vincent Kompany, 34, amekataa fursa ya kurejea katika klabu hiyo kama msaidizi wa kocha Pep Guardiola muda mfupi baada ya kuondoka ili kutimiza ndoto yake ya kuwa kocha wa Anderlecht. (Sun)
Kufikia mwisho wa January, Sanchez alikuwa amecheza mara saba katika timu ya Inter Milan msimu huu
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer bado anaweza kuachana na mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez msimu huu huku Inter Milan ikifikiria kuongeza mkataba wake wa makubaliano ya mkopo. (Express)
AC Milan imeonesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Burnley na Ireland Jeff Hendrick, 28, katika uhamisho usiokuwa na malipo. (Sky Sports)
Ajenti wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, 21, Achraf Hakimi, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Real Madrid, anasema kipaumbele kwa mchezaji huyo ni kucheza katika klabu ya Uhispania lakini anadai hakuna haraka kwa mchezaji huyo kutoka Morocco kurejea. (Evening Standard)
Leicester City imeimarisha nia yake ya kumsajili mlinzi wa Celtic 22 raia wa Norway Kristoffer Ajer. (Nicolo Schira, via Leicestershire Live)
Kocha wa Birmingham City Pep Clotet anatarajia kwamba angalizo kwa kiungo wa kati kijana Jude Bellingham litaongezeka ikiwa ligi itarejelelewa huku Manchester United na Borussia Dortmund wakihusishwa na mchezaji huyo wa miaka, 16. (Sky Sports)
Arsenal imekamilisha usajili wa winga raia mzaliwa wa Rwanda George Smith, 19, ambaye pia anaruhusiwa kuwakilisha Norway (VG - in Norwegian)
Moussa Dembele ameifungia magoli kumi Lyon msimu huu wa ligi
Aidha, Arsenal imeonesha tena nia kwa mchezaji wa Lyon na mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele, 23, na kuchukua hatua ya kuwasiliana na wawakilishi wake. (L'Equipe - in French)
Manchester United itaongeza hamasa zaidi kwa mshambuliaji wa Lyon vilevile ambaye sasa hivi thamani yake inaweza ikapungua. (Star)
Wakati huohuo, Arsenal inatarajiwa kuwafuta kazi watu 10, waliosaidia kutambua mshambuliaji Reiss Nelson, 20, na winga Bukayo Saka, 18, wakati inapoanza kutekeleza hatua za kubana matumizi kutokana na janga la corona. (Mail)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.