Habari za Punde

Rais wa Madagascar Rajoelina amewashutumu wakosoaji wa dawa ya mitishamba

Rais wa Magagascar Bwana Rajoelina anasema kwamba taifa la Ulaya lingekuwa limetenegenza dawa hiyo, majibu ya mataifa ya magharibu yangekuwa tofauti

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amesema kwamba wakosoaji wa dawa ya mitishamba ambayo haijajaribiwa ambayo anaipigia debe kuwa tiba ya Covid-19 inaonyesha tabia ya ubwenyenye ya mataifa ya magharbi dhidi ya Afrika.
Shirika la Afya duniani limeonya dhidi ya kutumia dawa ambazo hazijafanyiwa majaribio. Dawa hiyo ya rais Rajoelina haijapitia majaribio ya wanadamu.
Muungano wa Afrika pia umesema kwamba inataka kuona data ya kisayansi kuhusu uwezo na usalama wa dawa hiyo kwa jina Covid-Organics.
''Iwapo ingekuwa ni taifa la Ulaya ambalo liligundua dawa hiyo , je kungekuwa na wasiwasi? sidhani'', bwana Rajoelina alisema katika mahojiano na shirika la habari la ufaransa 24.
Madagascar imeripoti wagonjwa 193 wa Covid-19 na hakuna kifo hata kimoja. Dawa hiyo ilifanyiwa majaribio watu 20 katika kipindi cha wiki tatu, mshauri wa rais huyo aliambia BBC wakati bidhaa hiyo ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita - hatua ambayo haiendani na muongozo wa WHO kuhusu majaribio.
Licha ya madai hayo , mataifa kadhaa ya bara Afrika ikiwemo Nigeria, Guinea-Bissau , Equitorial Guinea na Liberia , tayari yameagiza dawa hiyo inayozalishwa kutoka kwa mmea wa pakanga - mti unaotumiwa kutengeneza dawa ya malaria pamoja na miti mingine ya Malagasy.
WHO imesema kwamba Waafrika wanahitaji kupata dawa ambayo imepitia majaribio ya kuridhisha hata iwapo inatoka katika tiba za kitamaduni.
Katika mahojiano hayo ya runinga, bwana Rajoelina alisema wanasayansi wa Afrika hawafai kudharauliwa.
Lakini kuna ushahidi kuonyesha kwamba dawa ya Covid-Organic ina uwezo.
Mkutano wa wataalam 70 wa dawa za kitamaduni Afrika umeafikiana na kwamba dawa zote zinapaswa kufanyiwa majaribio miongoni mwa binadamu , kulingana na shirika la Afya duniani tawi la Afrika ambalo lilichapisha katika twitter.
Pia kumekuwa na maonyo kutoka kwa wataalam kwamba kinywaji hicho kinaweza kuwadanganya watu kuhusu usalama hatua ambayo inaweza kuwafanya watu kutofuata masharti ya kukabiliana na ugonjwa wa corona.
Wiki iliopita zaidi ya $8bn (£6.5bn) ziliahidiwa kusaidia kubuni chanjo ya virusi vya corona na kufanyia utafiti tiba ya ugonjwa huo.
Makumi ya miradi ya utafiti inayojaribu kutafuta chanjo kwa sasa inaendelea kote duniani.
Wataalam wengi wanafikiria kwamba huenda ikachukua hadi kati ya 2021 takriban miezi 12 -18 baada mlipuko wa virusi hivyo kwa chanjo kupatikana.
Mataifa kadhaa ya Afrika yalichukua hatua za haraka katika harakati ya kujaribu kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuweka amri za kutoka nje .
Lakini amri hizo sasa zinaanza kuondolewa huku serikali zikijaribu kupima maslahi yake ya kiafya na kiuchumi.
Kuondolewa huko kwa masharti hayo ya kutoka nje kumeshinikiza dharura ya kupata tiba ya ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.