Habari za Punde

UONGOZI WA MACHINGA WALIA NA VIBAKA IRINGA

Katibu mkuu wa umoja wa wajasiliamali wadogo wadogo mkoa wa Iringa Joseph Mwanakijiji akiongea na waandishi wa habari baada ya kutokea wimbi la vibaka manispaa ya Iringa kwa kuwaibia wajasiliamali.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga manispaa ya Iringa wameendelea kuathirika na wizi unaofanywa na vibaka kwa kuvunja stoo na kuiba mali za wajasiliamali hao.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu wa machinga mkoa wa Iringa Joseph Mwanakijiji alisema kumekuwepo na wimbi kubwa la vibaka ambao wanavunja ofisi za wajasiliamali wadogo wadogo na kuiba Mali za wajasiliamali.

Alisema kuwa vibaka wameongezeka katika kipindi hiki cha Corona kutokana na kuongezeka kwa matukio mbalimbali ya wizi unaotokea kwa wajasiliamali wadogo wadogo wa manispaa ya iringa.

Mwanakijiji alisema siku za karibu zaidi ya wajasiliamali kumi na tano walivunjiwa stoo zao na kuibiwa mizigo na Mali zote zilizokuwemo ndani na kupelekea hasara kubwa kwa wajasiliamali hao.

"Wajasiliamali wengi mitaji yao bado midogo na wanamikopo katika taasisi za kibenk au kwa watu binafsi hasa wenye maduka makubwa hivyo unapo muibia mjasiliamali huyu unamrudisha nyuma kibishara na kumfanya awe maskini kabia"alisema mwanakijiji

Alisema kuwa uongozi wa machinga mkoa wa Iringa uliunda kamati maalum ya kuwatafuta vibaka hao kwa ushirikiano mkubwa na serikali ya wilaya ya Iringa na kufanikisha kuwakamata baadhi ya vibaka wakiwa na mizigo ya wizi.

"Tulifanya kazi vizuri kushirikiana mkuu wa wilaya Richard kasesela na jeshi la polisi Iringa tukafanikiwa kukamata baadhi ya bidhaa zilizokuwa zimeibiwa  kwenye stoo za wajasiliamali wadogo wadogo hapa manispaa" alisema mwanakijiji

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.