Habari za Punde

Wanakaya masikini na wasiojiweza jimbo la Pangawe wapatiwa msaada

Na Takdir Suweid

Wananchi wametakiwa kuitumia vizuri misaada wanayopewa na Wafadhili ili iweze kuwasaidia na kufikia malengo yaliokusudiwa. 

 Wito huo umetolewa na Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Magharibi B Thuwaiba Jeni Pandu wakati alipokuwa akikabidhi msaada wa vyakula kwa kaya Masikini hamsini za Jimbo la Pangawe na Mwanakwerekwe,msaada ambao umetolewa na Viongozi wa Jimbo la Pangawe kwa kushirikiana na Taasisi ya Direct aid. 

Amesema Wafadhili wanatoa Misaada kwa Wananchi kama Vile Unga,Sukari,Mchele na Tende ili iweze kuwasaidia hivyo si vyema kuvifanyia ubadhirifu vyakula hivyo walivyopatiwa. 

 Aidha amewataka baadhi ya Wananchi ambao hawajapata sadaka hiyo kuacha kulalamika kwani inayotolewa ni ndogo ikilinganisha na Idadi ya Watu wanaohitaji kupatiwa. 

 Hata hivyo amesema Viongozi wa wana majukumu mengi ya kifamilia na kiserikali katika kuwatumikia Wananchi wao kwa hivyo hawatoweza kutekeleza majukumu yote ya wananchi lakini wafadhili hao wataweza kuwaunga mkono kwa kuwasaidia. 

 Nao baadhi ya Wanakaya Masikini na Wazee wasijiweza katika Jimbo la Pangawe na Mwanakwerekwe wamesema msaada waliopewa umeweza kuwasaidia na wanahitaji kusaidiwa zaidi kutokana na hali ngumu ya maisha Wanayoishi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.