Habari za Punde

AHADI YA JPM YA UJENZI WA MRADI WA MAJI WA BILIONI 15 WAZINDULIWA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof.Kitila Mkumbo akipata maelezo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji katika wilayani missenyi 

Na Allawi Kaboyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof.Kitila Mkumbo amezindua ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa zaidi ya shilingi Bilioni 15.1 utakao sambaza maji kwenye miji ya Kyaka na Bunazi kwa kuwahudumia wahudumia wananchi zaidi ya elfu 50 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mhe.Rais John Magufuli wakati wa ziara yake mwezi julai 2019,wilayani missenyi Mkoani Kagera.
Hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi imefanyika katika wilayani missenyi  juni 01,2020 ambapo katibu mkuu amesema kuwa wizara ya maji imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji hapa nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi  ya chama cha mapinduzi.
Kitla amesema kuwa Mhe. Rais Magufuli alipofika Kyaka akitokea Karagwe alipokea kilio cha wananchi wa wilaya hiyo ambnao walimuomba kuwatatulia kero ya maji ambayo imekuwa ni kero ya kudumu tangu inchi inapata uhuru na ndipo Rais Magufuli aliahidi kuwajengea mradi mkubwa wa Maji  na sasa utekelezaji wake utaanza mara moja.
Ameongeza kuwa wizara kupitia Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imengia mkataba na mkandarasi kampuni ya  China Civil Engineering contractions corporation ambapo amesema kuwa mradi wa maji Kyaka-Bunazi utagarimu shilingi Bilioni 9.4.
“Fedha kwaajili ya utekelezaji wa mradi huu zinatolewa na Serikali ya Tanzania kupitia mfuko wa maji, hivyo kwadhati kabisa ninachukua fursa hii kwaniaba ya wizara ya maji pamoja na wakazi wote wa Kyaka-Bunazi kumshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha anamtua mama ndoo kichwani.” Amesema Prof.Kitila.
Aidha amezitaka mamlaka za wilaya ya Missenyi chini ya mkuu wa wilaya na kamati ya ulizi na usalama kuhakikisha wanafatilia mradi huu kwa ukaribu na kwa kila hatua ili agizo la Mhe. Rais Magufuli linatekelezwa kwa wakati na ukamilifu.
“Ili kuhakikisha utekelezaji wa kazi za mradi kwa ufanisi na kwa haraka tayari tumetuma shingi milioni 650 kwa BUWASA na MWAUWASA, hivyo natoa maelekezo kwa mamlaka hizo kuweka mikakati ya kuhakikisha kazi za mradi zinatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na ndani ya muda.” Amesema katibu mkuu.
Akiongea kwa niaba ya wananchi wa wilaya missenyi, mwenyekiti wa halmashauri hiyo Projestus Tegaamaisho amesema kuwa wananchi wa wilaya hiyo wanayochangamoto kubwa ya maji  hali inayowapelekea wanaume kuamka asubuhi sana kwenda kuchota maji kwenye mito ambayo pia sio salama ili kuwasaidia wake zao na wengine kulazomika kununua maji kwa gharama kubwa.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo utawasaidia sana wananchi kuachana na kero ya maji hasa wa miji ya Kyaka na Bunazi  ambao maisha yao yote hutegemea maji ya chumvi na wengine maji ya mto Kagera ambayo sio salama kwa afya zao.
Kwaupande wake meneja wa wakala wa maji vijijini na mijini ambao ndio washauri wakuu wa mradi mhandisi Emakulata Nshange amesema kuwa tayari usanifu wa mradi huo umekamilika  na kuainisha kuwa mkandarasi atatumia shilingi bilioni 9.4 na wataalamu wa ndani watatumia shilingi bilioni 5.7 kwa ulazaji wa mabomba ambapo ukamilikaji wake kwa mujibu wa mkataba ni miezi 13.
Emakulata ameongeza kuwa wakati mkandarasi anatekeleza mradi huu wanatakiwa kuonyesha ushikiano  na kuongeza kuwa mradi ukikamilika wananchi watatakiwa kuchangia huduma ya maji kwa kulipia bili.
Katika hatua nyingine katibu mkuu amemwagiza mkandarasi kuhakikisha anatoa ajira kwa vijana wa wilaya ya missenyi  wakati wote wa utekelezaji wa mradi huu kwa shughuli zote ambazo sio za kitaalamu zaidi ili iwe fursa kwa wakazi wa missenyi, na kutoa wito kwa wananchi ambao mradi huu utakuwa unapita kwao wapishe mradi na wasiwe chanzo cha kukwamisha mradi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.