Bi Zuwena Salum ndiye aliyekuwa Mtangazaji wa kwanza wa kike Sauti ya Unguja na kwa Afrika Mashariki.
Vipindi maarufu vya Bi Zuwena ni Ladies Club na Muungwana (kipindi kilichogusia Malezi ya Kizanzibari) Vipindi vya Mila, Desturi, Wema, Ihsani, khushui, Akhlaqi na thaqafa za watu wa Visiwani.
Baadaye ndio wakaja Bi Sanura Juma Shakhsy na Zeyana Seif (BBC).
Mazishi yake yalikuwa leo Alkhamis tarehe 18 June 2020 hapo Wireless kwao.
Bi Zuwena alipata mtoto aitwaye Nabil.
Tumuombe Allah amsamehe makosa yake, amuweke mahala pema peponi na awape subra wafiwa.
Allaahumma Amin
No comments:
Post a Comment