Habari za Punde

Walotia Nia Gombombea Nafasi Mbalimbali za Uongozi Wanapaswa Kuzingatia Maadili na Kanuni za Uchaguzi. - Balozi Seif

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambae pia Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga Kichama  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiwapungia Mkono Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kahama alipofika kuzungumza nao akiwa katika ziara ya siku Tatu Mkoani Shinyanga.
Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kahama alipofika kuzungumza nao akiwa katika ziara ya siku Tatu Mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Shinyanga Mh. Lusya akifafanua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ndani ya Mkoa wa Shinyanga mbele ya Mlezi wa Mkoa huo Balozi Seif  Ali Iddi.
Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa Shinyanga  ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Nd. Gasper Kileo akimkaribisha  Balozi Seif Ali Iddi kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kahama.
 Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kahama wakifuatilia Hotuba ya Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga Balozi Seif Ali Iddi hayupo Pichani.
Na.Othman Khamis.OMPR.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati Taifa linakaribia kuingia katika Uchaguzi Mkuu ifikapo Mwezi Oktoba Mwaka huu wale waliotia nia ya kutaka kugombea nafasi mbali mbali wanapaswa kuzingatia maadili na kanuni za uchaguzi ili wapiti salama kwenye mchakati huo.
Alisema wapo baadhi ya waliotia nia wameanza Kampeni kwa kuwatumia Mawakala wao kumwaga fedha jambo ambalo litawaponza baadae licha ya kushinda kwa kura nyingi kwenye mchakato wao lakini watajikuwa wamefyekwa kabisa.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wajumbe WA Kamati Kuu ya CCM Wilaya ya Kahama akianza ziara ya siku Tatu Mkoani Shinyanga kuangalia hitimisho la Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ndani ya Mkoa huo.
Alisema kitendo cha kumchagua Kiongozi kwa kutumia rushwa hatima yake ni kumpata Mtu asiye ya maadili katika kusimamia Ilani ya Uchaguzi kitendo ambacho Uongozi wa CCM hautakuwa tayari tabia hiyo ifanyike kwa vile itaviza maendeleo ya Taifa.
Balozi Seif akiwa mlezi wa Mkoa wa Shinyanga aliwapongeza Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Serikali wa Mkoa huo kwa jitihada uliochukuwa na kupelekea kupatikana maendeleo makubwa ya Jamii na Taifa kwa ujumla.
Alisisitiza suala la Umoja na Mshikamano baina ya Viongozi, Wanachama pamoja na Wananchi ili kulivua salama Taifa katika mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu Tanzania ikiendelea kujizolea sifa Kimataifa kwa kudumisha Demokrasia ya Vyama vingi vya Sisasa.
Alisema Viongozi pamoja na Jamii inapokaribisha fitna na majungu miongoni mwao dalili ya uhasama inapaswa kueleweka kwamba itatawala miongoni mwa jamii nzima.
Mapema Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Nd. Gasper Kileo alionya kwamba wale watakaotanguliza fedha  kwa ajili ya kujiweka tayari waelewe kwamba wamejichimbia kisima.
Mapema Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Nd. Gasper Kileo alionya kwamba wale watakaotanguliza fedha  kwa ajili ya kujiweka tayari waelewe kwamba wanajichimbia kisima.
Nd. Gasper alisema Rushwa ya uchaguzi imebainika wanayopokea zaidi ni viongozi kuanzia ngazi ya Shina,Tawi, Kata, Jimbo, Wilaya na hata Mkoa na hatimae wanasimamisha  Kiongozi anayepita kwa mgongo wa dhambi hiyo mbaya.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Kahama Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga ambae pia ni Mkuu wa Mkoa huo Mh. Zainab Rajab Telak alisema Miradi yote iliyopangwa kufanyika Mkoani humo imetekelezwa kwa  mafanikio makubwa ya kupigiwa mfano.
Mh. Zainab alisema kazi iliyopo hivi sasa katika ukamilishaji wa Miradi ya Maendeleo ndani ya Halmashauri za Wilaya zilizomo Mkoani  humo itaanza wakati wowote baada ya kuingiziwa Bajeti ya shilingi Bilioni 2.4.
Alimshukuru na kumpongeza Mlezi wao kwa jitihada zake alizochukuwa katika usimamizi wake wa Ulezi ambao umeleta tija kubwa hasa kutokana nay eye binafsi kuunga mkono Miradi ya maendeleo ya Wananchi wa Shinyanga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.