Habari za Punde

Mapokezi ya Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM Kisiwani Pemba leo Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi

Mgombea Urais wa Zanzibarv kwa Tiketi ya CCM Mhe.Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi akivishwa shada la mau baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake Kisiwani Pemba akitokea Zanzibar kwa ajili ya mkutano wa Mapokezi na kutambilishwa kwa Wanachama wa CCM Kisiwani Pemba leo 19-7-2020, mkutano uliofanyika katika viwanja vya Tibirinzi Chakechake.

Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar CCM Mama Maryam Mwinyi akivishwa shada la maua baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Chakechake Pemba akiongozana na Mumewe.

Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Hussein Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa CCM Pemba baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege Chakachake Pemba leo.kwa ajili ya mkutano wa mapokezi yake na kuzungumza na Wanachama wa CCM Pemba katika uwanja wa Tibirinzi Chakechake Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar CCM Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege Chakechake Pemba akitokea Zanzibar kwa ajili ya mkutano wake wa mapokezi na kutambulishwa kwa WanaCCM Pemba katika Uwanja wa Tibirinzi Chakechake Pemba leo.

Waliokua Watia Nia katika kinyanganyiro cha Urais wa Zanzibar kupitia CCM na kufikia Tano Bora wakiwa katika mapokezi ya Mgombea Urais wa Zanzibar CCM Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi, alipowasili katika Uwanja wa Ndege Chakechake Pemba leo, asubuhi.  No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.