Habari za Punde

Kamati ya Kitaifa ya Mazishi ya Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe. Mkapa.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifga ya Mazioshi ya Marehemu Mzee Mkapa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akityoa heshima mbele ya Jeneza la Marehemu Mzee Mkapa hapo Uwanja wa Taifa.
Mwenyekiti Wa Kamati ya Kitaifa ya Mazshi ya Marehemu Mzee Bendjamin William Mkapa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Vyombo vya Habari wakati akitoa Taarifa ya Mwisho ya Ratiba ya Mazishi.
Wanahabari wa vyombo mbali mbali vya Habari wakiwa kazini kurikodi tukio la Taarifa ya Waziri Mkuu kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Picha na OMPR. 
Na.Othman Khamis.OMPR.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Mazishi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ya Tanzania  Mzee Bendjamin William Mkapa ambae pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Kassim amewashukuru Watanzania waliowengi kwa kutenga muda wao na kushiriki kumuaga Kiongozi huyo aliyefariki Dunia Usiku wa kuamkia Ijumaa.
Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa shukrani hizo wakati akitoa Taarifa ya ratiba ya mwisho  kwa Watanzania kupitia Vyombo mbali mbali vya Habari hapo katika Uwanja wa Uhuru ambapo zoezi la kuuaga Mwili wa Marehemu likiendelea hadi  kesho Jumanne.
Alisema ushiriki wa Watanzania katika kumuaga Marehemu Mzee Bendjamin William Mkapa aliyetoa mchango Mkubwa Kitaifa na Kimataifa umeonyesha upendo mkubwa  unaofaa kuenziwa muda wote.
Mwenyekiti Majaliwa alieleza kwamba Jamii inaposhikamana katika matukio ya furaha na misiba huchangia kuongeza mshikamano unaokwenda sambamba na Utamaduni wa Watanzania ulioongeza tunu ya  Amani inayotamaiwa na Mataifa mengio Duniani.
Akizungumzia rabita ya mwisho ya Kuaga Mwili wa Marehemu Mzee Mkapa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa alifahamisha kwamba  Baadhi ya Viongozi wa Mataifa Rafiki na yale ya Jirani wamethibitisha kushiriki kwenye msiba huo.
Alisema Wageni hao watapata wasaa wa kutoa pole katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam katika siku ya Tatu na mwisho ya kuagwa kwa Mwili wa Marehemu.
Mh. Majaliwa kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti Mwenzake  na Serikali kwa ujumla amevishukuru vyombo vya Dola kwa umakini wake wa kusimamia zoezi hilo lililotoa fursa kwa Wananchi kushiriki vyema.
Aidha amevipongeza Vyomvo vyote vya Habari vilivyoshiriki katika kuwapa Taarifa mbali mbali Wananchi juu ya tukio zima tokea kufariki, harakati za kuagwa kwa mwili pamoja na kuzikwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.